CCM yapata ushindi mkubwa

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
1574489839252.png

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Dodoma kimepita bila kupingwa katika vijiji, mitaa na vitongoji 3,905 kati ya 4,032 vilivyopo sawa na asilimia 96.85. Akizungumza na Habari- LEO Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Jamila Yusuph alisema ushindi huo ni taswira nzuri katika kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.

Alisema ushindi huo walioupata hadi sasa unatokana na wana CCM mkoa huo kuwa na utaratibu wa kufanya tathmini kila baada ya uchaguzi, ili kujikosoa walipokosea na kujisahihisha. Katibu wa CCM alisema hiyo ndiyo siri ya ushindi mkubwa katika mkoa huo kupata viti vingi vya vitongoji, mitaa na vijiji. “Kati ya vijiji 564 vilivyopo, CCM imepita bila kupingwa katika vijiji 533 sawa na asilimia 94, kati ya mitaa 258 iliyopo CCM imepita bila kupingwa mitaa 255 sawa na asilimia 98 na huo ni ushindi mkubwa katika mkoa wa Dodoma,” alisema.

Jamila alitoa rai kwa wanachama wa CCM kutopumzika kwa kuwa wameshapata ushindi bali wanatakiwa kuendelea kutafuta kura katika maeneo yaliyobaki. Alisema hata mahali ambapo CCM imepita bila kupingwa, wanachama wa chama hicho wanatakiwa kwenda kuwashukuru wananchi na kuwaelezea mipango ya serikali katika kuwapatia maendeleo wananchi wanyonge.
 
Unakimbia peke yako bila kuwepo anayekukimbiza halafu unajisifu kua una mbio huo ni ujinga
 
Anasema wakawashukuru wananchi, kwani waloofanya mkakati wa kuengua wagombea wa upinzani ni wananchi? Majanga kweli kweli
 
View attachment 1269798

Hakika ushindi Wa kishindo
 
Anasema wakawashukuru wananchi, kwani waloofanya mkakati wa kuengua wagombea wa upinzani ni wananchi? Majanga kweli kweli

Kuwashuru wananchi ni kuwatusi,ushindi ni juhudi ya awamu ya tano ishukuliwe
 
Kwa mkoa huu kijani na njano watatawala milele mpaka hapo wenyeji wa mkoa huo watakapoamua kuamka.
 
Back
Top Bottom