CCM yapata aibu kubwa huko Temeke


Kumbe hata cdm wakishika dola hawatajenga bali tutajenga watz kwa kodi zetu. Ngoja tu ccm aendelee kuongoza...
 
Aibu gani wamepata hivi kuna aibu kama kupora mke wa mtu na kutelekeza familia au kuzaa nje ya ndoa.
naona unajaribu kuhamisha mada buraza. kubali tu watu wametuchoka. (from a ccm member)
 
Hizo barabara wanajenga kwa pesa yao?
 
Tiba wewe yaelekea siku moja ulitokea Mbagala kwa kukwepa foleni ukapitia Temeke Mikoroshoni ndiko kuna barabara za 2 za lami uchochoroni .Usiwaudh Wandengereko watakuloga
Mimi nnachojua ni kwamaba Mtemvu anawatafutia ajira vijana wa Temeke huko Uarabuni!
 
Kumbe hata cdm wakishika dola hawatajenga bali tutajenga watz kwa kodi zetu. Ngoja tu ccm aendelee kuongoza...
dah! jamiiforums imevamiwa. siamini kama kuna great thinker anaweza kufukiri namna hii. chama cha siasa hakitengenezi pesa, bali huchukua wajibu wa kuongoza serikali, na kusimamia mapato yanayotokana na sasilimali za nchi (ikiwemo kodi zetu) ili kutekeleza sera za kuwakwamua wananchi wake kiuchumi........., ambapo ccm kazi hiyo imetushinda. (ingwa tumejitahidi kwa asilimia 0.00000000001)
 
Aibu gani wamepata hivi kuna aibu kama kupora mke wa mtu na kutelekeza familia au kuzaa nje ya ndoa.
Hivi huyo mwenye mke yuko hai au ni marehemu! Na kama yuko hai je ni Rijali??
 
Acha kutuzugz tuna macho ya kuona ,mbona watu nyomi.Mpaka wamesimama nje ya turubai ambalo ndio ilikuwa makadirio yetu ya awali.Hivyo tumevuka lengo

Pia ukichukulia kuwa hatukusomba watu kwa maroli wala kugawa buku mbili, mbili na ubwabwa kwa maharage!!
 
Mnaizungumzia Temeke ipi jamani,huku ni kama tuko pembezoni mwa Tanzania maji ya Dawasco cjui mara ya mwisho tuliyanywa lini from 1980's daaaaaaa
 
Aibu gani wamepata hivi kuna aibu kama kupora mke wa mtu na kutelekeza familia au kuzaa nje ya ndoa.

Vipi kuhusu aibu ya kumbaka mwanfunzi na kumpa ukimwi kama alivyofanya kada mkongwe wa CCM Mh. Kapuyanga?
 

balaa, yangu macho kuelekea hiyo 2015. Kama kuna mbunge wa ccm atakayerudi bungeni basi ni anne kilango na filikunjombe
 

Temeke Ipi au hata hii ya Kigamboni??!! Maana hali mbaya Kigamboni!!!!
 

Mkuu tuko pamoja. Hakuna mahali nimesema Mtemvu alitoa hela yake mfukoni kujenga barabara. Kama aliweza kupaza sauti za waliomchagua na baraza la madiwani wakatenga fungu kubwa kujenga barabara kwanini asipate credit kwa hilo? Mbona sehemu nyingine za jiji kama Kinondoni na Ilala barabara nyingi bado ni za vumbi tu?

Kwa maoni yangu anastahili pongezi.

Tiba
 
kama TEMEKE yenye vijana wengi wanaoona KARIBU imefanikiwa kujiepusha na CCM , basi hiyo ni hatua nzuri sana ! Huu ndiyo mwisho wa MTEMVU temeke , amewadanganya wapangaji wa nhc kwamba watauziwa nyumba wanazokaa huku akijua kwamba hana uwezo huo , na sasa kila mpangaji anayo NOTISI inayomtaka awe ameondoka kwenye nyumba kabla ya juni 2014 , akafie mbele ! Mtemvu amehakikisha kata ya KURASINI INAMALIZWA KUUZWA KWA BEI RAHISI , kisa ! umasikini wa wakazi wake ! KAMA MBUNGE AMESHINDWA KABISA KUWASAIDIA WANANCHI WA KURASINI , 2015 HATUTAKI LAWAMA .
 
Aibu gani wamepata hivi kuna aibu kama kupora mke wa mtu na kutelekeza familia au kuzaa nje ya ndoa.

Nyani haoni kundule! Huko CCM ndo kuna vibaka wa kutupwa!! Yule jamaa ambaye anamtoto mchanga anayenyonya unasemaje. Ni mwaminifu katika ndoa yake!! masuala ya social ni very sensitive kibinadamu!!
 

Mkuu weka kumbukumbu sawa sema Mtemvu anawasaidia vijana kwenda "utumwani" huko Uarabuni.

Tiba
 

mjomba , nimecheka sana ! Hivi kupiga deki vyoo vya waarabu nayo ni ajira ? Mtemvu bhana !
 
Mtemvu ndiye mbunge pekee wa Dsm atakayerudi mjengoni mwaka 2015

 
Mkuu weka kumbukumbu sawa sema Mtemvu anawasaidia vijana kwenda "utumwani" huko Uarabuni.

Tiba
Mzungu ndiye aliyeleta utumwa angalia mabaki ya watu weusi yako wapi katika mabara ya dunia ?
 
Mzungu ndiye aliyeleta utumwa angalia mabaki ya watu weusi yako wapi katika mabara ya dunia ?

Mkuu sikuzungumzia aliyeleta utumwa, nimezungumzia mazingira wanayofanyia kazi hao wanaopelekwa huko Arabuni na akina Mtemvu. Sasa hivi ni kwamba mtindo umebadilika, badala ya waarabu kuja kuchukua watumwa huku, sisi wenyewe tunatafuta visa, tunatafuta nauli kuufuata huo utumwa.

Tiba
 
Kama kweli alisema tml kuna bara bara nzuri kuliko masaki...basi ccm imekufa kisera
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…