mfalmeselemani
Member
- Sep 30, 2014
- 95
- 47
Na Mwandishi Wetu
HALI ya sintofahamu inazidi kugubika ushindi wa Jackson Kangoye kwenye kura za maoni katika jimbo la Tarime Mjini, baada ya viongozi wa Chama wilaya kukiuka taratibu na kumbeba Kangoye.
Taarifa za kuaminika ilizozipata zilidai kuwa Kangoye ametumia fedha lukuki ikiwemo kutoa sh. laki moja kwa kila mjumbe.
Rushwa imeifanya ofisi ya wilaya ya CCM kushindwa kuikemea huku Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wilayani humo ikidaiwa imeikalia kesi ya Kangoye kukamatwa na rushwa.
Inaelezwa siku moja kabla ya uchaguzi mshindi huyo wa kura za maoni alikamatwa na rushwa na TAKUKURU na cha kushangaza aliachiliwa kwa dhamana na hadi leo kesi haijapelekwa mahakamani.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Jackson ambaye amekuwa akishirikiana na Katibu wa CCM wa wilaya ya Tarime aliyefahamika kwa jina la Mkarukwa wamesambaza mamilioni ya shilingi kuhakikisha Jackson anakuwa mgombea wa CCM wilayani humo.
Alipotafutwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara, Samwel Kiboye maarufu namba tatu simu yake ya mkononi ilikuwa haipokelewi huku taarifa za ndani zikieleza kuwa kumeanza mashinikizo ya kutosimamia maadili ndani ya Chama.
Mjumbe wa mkutano mkuu wa wilaya kutoka Kata ya Turwa, ambaye hakupenda jina lake liandikwe alisema uchaguzi Tarime Mjini haukuwa wa haki kutokana na rushwa kubwa iliyokuwepo.
" Uchaguzi huu si haki na haupaswi kabisa kuungwa mkono maana rushwa ilikuwa kubwa na ni hatari sana. Chama kisimame imara na ikiwezekana iufute mbali na hata kuwaondoa wanachama waliotoa rushwa wasiwepo kwenye uchaguzi mkuu" alisema mwanachama huyo.
Inaelezwa kuwa Jackson na wapambe wake walikuwa wanagawa fedha kwenye hoteli ya Goldland, ambaye inamilikiwa na rafiki wa baba yake, Mzee Kangoye, ambaye anajulikana kwa jina la Mseti ambapo walikuwa wanatoa hela kwa wajumbe ya shilingi 100000 huku akiwaahidi kuwapa elfu 80 baada ya kumpigia kura.
Kitendo ambacho kimeleta fedheha kubwa kwa wajumbe ambao baadhi walionekana kulalamika hadharani kutopatiwa fedha katika baa ya LaKairo ambapo walikuwa wanakutakana kupongezana kwa kugawa fedha vizuri kwa watu mbali mbali.