Hakuna uhusiano wa
moja kwa moja kati ya hizo timu na hivyo vyama. Lakini wapaswa kujua
kuwa enzi zile za ukoloni harakati za siasa zilikuwa zinafanya kwa
kificho na mojawapo ya sehemu zilizotumika ni klabu za michezo. Kutokana
na asili na historia ya Yanga waasisi wa TANU waliitumia kuendesha
harakati za kudai uhuru. Hivyo naturally, ilitokea waasisi wengi wa TANU
na baadae CCM walikuwa na ushabiki na Yanga kwa sababu ya hiyo
historical connection. Yafaa ujue pia kuwa Yanga ilikuwa timu ya
wazalendo weusi na simba ilikuwa timu ya wageni.
Lakini with time, kumetokea kitu kama vile 'intermarriages' ambapo
waafrika weusi waliingia simba na wageni pia waliishadadia yanga. Na
ndio mix unayoona leo. Kibwagizo cha CCM ni cha zamani zile ambapo chama
kimeshika hatamu na kila mtu alikuwa assumed kuwa CCM maana ndio chama
pekeee. However, Yanga hawatumii tena hicho kibwagizo siku hizi bali ni
simba ili kuwakejeli yanga kama ilivyo kwa yanga wanavyoimba simba,
simba, simba au eeeh kidedea kuwakejeli simba pale yanga inaposhinda.
Juzi kama ulikuwepo uwanjani utaweza ku-prove hili.