CCM yamwangukia Bashe!

Sina tatizo na wagombea wote wa UVCCM isipokuwa kwa uchambuzi wa ndani kabisa haiingii akilini kwa wagombea wawili Beno na Kawawa Jnr kugombea nafasi hizo, kwanza wote niliowataja tayari ni wa NEC wakuchaguliwa kupitia kundi la vijana nafasi wanayogombea inampa mshindi nafasi ya kuwa mjumbe wa NEC.

BAshe si mjumbe wa NEC hivi kwa akili ya kawaida kabisa kwa nini wajumbe wasimchague Bashe kwa maana halisi ya kuongeza uwakilishi wa vijana katika NEC?
 
Sina tatizo nawagombea wote wa Uv CCM isipokuwa kwa uchambuzi wa ndani kabisa haiingii akilini kwa wagombea wawili Beno na Kawawa Jnr kugombea nafasi hizo, kwanza wote niliowataja tayari ni wa NEC wakuchaguliwa kupitia kundi la vijana nafasi wanayogombea inampa mshindi nafasi ya kuwa mjumbe wa NEC!!!!!!! BAshe si mjumbe wa NEC hivi kwa akili ya kawaida kabisa kwa nini wajumbe wasimchague Bashe kwa maana halisi ya kuongeza uwakilishi wa vijana katika NEC?

Naungana kabisa na M-bongo kwa maoni ya uchambuzi juu ya nafasi ya makamu mwenyekiti wa UVCCM. Ni dhahiri kabisa kuwa wagombea wote walioteuliwa wana haki kabisa ya kugombea na kuchaguliwa kushika wadhifa huo.

Hata hivyo nadhani ni vema busara ingekutimika zaidi kwa hawa wagombea wengine ambao tayari ni wajumbe wa NEC kwa lengo la kuongeza idadi ya vijana ndani ya kikao muhimu kabisa cha NEC.

Maana hata ukiyasoma majukumu ya nafasi ya makamu mwenyekiti,kwa mwanasiasa makini na mwenye upeo wa kimtazamo,huwezi kutumia nguvu nyingi kuisaka nafasi hii hashwa kwa wale ambao ni waNEC tayari.

Si kila jambo linataka ushindani tu,nadhani hata busara inahitajika ikiongozwa na ukomavu wa kisiasa.
 
Kimsingi kabla mazungumzo hayajaenda mbali niliweke wazi hili, tulipokuwa tukizungumza clouds fm, hatukutaja jina la hussein bashe, na baada ya kusoma hapa naanza kuhisi kuna watu wanakusudia kutumia hili kisiasa maana yanayosemwa juu ya kina benno na ridhiwani ni mawazo binafsi ya aliyendika hapo juu, hebu tuwe wakweli badala ya kumlisha mtu maneno, narudia sina mgombea na wala mimi mpaka sasa sio mpiga kura, haya ni uzushi

Hongera sana Nape kwa kuliweka hili wazi na unafanya vizuri kutokuwa na kambi yoyote. yawezekana una kambi lakini hiyo ni siri yako.
 
Kaka karibu sana hapa katika baraza letu linalojulikana kwa kifupi kama JF;ni vizuri tukasaidiana kuirekebisha jamii na Taifa kwa ujumla.

Mtu/Taasisi/Kiongozi/Viongozi wanapochemsha hapa ndipo tunapokemea makosa waliyoyafanya na nia ni nzuri tu,kwa maslahi ya Taifa letu la Tanzania.

Karibu sana.
 
Kingine nillichozungumza ni swala zima la kufungwa kwa vyuo vikuu nchini....nilisema naamini kinachopigiwa kelele sio SERA YA UCHANGIAJI YENYEWE bali ni UTEKELEZAJI WA SERA, hivyo sioni sababu ya serikali kutumia ubabe kufunga vyuo badala yake wakae chini na wadau kujadili namna bora ya kutekeleza sera hii. Najua kuwa iko katikati ya mwaka wa fedha wa serikali lakini muhimu kukubali kuwa yapo matatizo katika utekelezaji wa sera hii, ili njia bora itafutwe kisha tuwe na utekelezaji bora zaidi mwaka ujao wa fedha. Maghembe aache ubabe si jambo la buisara kila mara kufunga vyuo hivi maana tunaanzisha utamaduni mbovu wa kutojadiliana kumaliza matatizo yetu hili sio jema.....

Hapa ulipeleka ujumbe mzuri kwa Maghembe. Je ulipeleka ujumbe wowote kwa wanafunzi( vijana wenzako) ambao kila semester lazima wapate sababu ya kugoma kwa kutoingia darasani na kufanya fujo, kama jinsi walivyosababisha kifo cha mwenzao semester iliyopita na kumkata na chupa mwenzao mwingine katika mgomo huu.

Je umewakumbusha kuwa wakati wao wanagoma vijana wenzao kwingine duniani wanaingia darasani kubuni mbinu mbalimbali za kuyawezesha mataifa yao kuwa katika nafasi nzuri katika kushindania rasilimali chache zilizopo?

Haya ni mambo ya msingi ambayo vijana wanaogoma kuingia darasani inapaswa waambiwe hata kama they are not popular views, hii ni iwapo maslahi ya taifa yatawekwa mbele ya maslahi ya kisiasa.
 
Maghembe aache ubabe si jambo la buisara kila mara kufunga vyuo hivi maana tunaanzisha utamaduni mbovu wa kutojadiliana kumaliza matatizo yetu hili sio jema.....
Hivi wewe kijana unafanya kazi wapi?kwanini unag'ang'ania siasa,hauwezi kuwaisaidia watanzania mpaka uwe mwanasiasa.

Hivi Tatizo ni magembe au tatizo ni bodi ya Elimu ya juu ambayo inaada hizi sera???Mie naanza kupata wasiwasi na wanasiasa wa aina nako.Wewe bado unaendeleza siasa za makundi ila kwa wakati mwingine unaonekana haupo!punguza jzba na utakuwa bora tu!

Nakushauri usiwe unakurupuka tu kuongea mambo ila anza kujua chanzo ni nini?

Jifunze kutoka kwa Mwanakijiji kwa upande mmoja,ila kw aushabiki wake wa kushadadiia chama flani kipindi flani ndiko mie huwa ananiboa,otherwise,Mzee unaweza
 
Hawa ndio vijana wa Kitanzania wa sasa, eti na wao wanajifanya kukosoa walichofanya kina chifu mangungo na kina hassan waliouza kilwa kwa kipande cha nguo. kweli nyani haoni kundule"
 
Hapa ulipeleka ujumbe mzuri kwa Maghembe. Je ulipeleka ujumbe wowote kwa wanafunzi( vijana wenzako) ambao kila semester lazima wapate sababu ya kugoma kwa kutoingia darasani na kufanya fujo, kama jinsi walivyosababisha kifo cha mwenzao semester iliyopita na kumkata na chupa mwenzao mwingine katika mgomo huu.

Je umewakumbusha kuwa wakati wao wanagoma vijana wenzao kwingine duniani wanaingia darasani kubuni mbinu mbalimbali za kuyawezesha mataifa yao kuwa katika nafasi nzuri katika kushindania rasilimali chache zilizopo?

Haya ni mambo ya msingi ambayo vijana wanaogoma kuingia darasani inapaswa waambiwe hata kama they are not popular views, hii ni iwapo maslahi ya taifa yatawekwa mbele ya maslahi ya kisiasa.

Kwakweli nilichokisema si kwamba tatizo ni la upande mmoja, hapana ni la pande zote mbili, lakini mwenye kuwaleta pamoja pande hizi mbili lazima awe ni aliyeshika mpini. Ungesikiliza mahojiano yale mwishoni nilisema hivi;

NATOA WITO KWA VIJANA KUTAMBUA KUWA HATMA YA TANZANIA IPO MIKONONI MWAO/MWETU VIJANA, TUNA WEZA KABISA KUITENGENEZA LEO TANZANIA TUNAYOITAKA KESHO, BADALA YA KULALAMIKA NA KUPIGA KILELE, MIMI NAAMINI KANZU YA IJUMAA INAFULIWA ALHAMISI ILI IKAUKE NA KUPIGWA PASI VIZURI READY KWA IJUMAA...

HIVYO UZALENDO KWA NCHI YETU LAZIMA UVUKE MIPAKA YA ITIKADI ZETU, NDIPO TUTAKAPOKUWA NA TANZANIA TUITAKAYO....
 
Hivi wewe kijana unafanya kazi wapi?kwanini unag'ang'ania siasa,hauwezi kuwaisaidia watanzania mpaka uwe mwanasiasa.

Hivi Tatizo ni magembe au tatizo ni bodi ya Elimu ya juu ambayo inaada hizi sera???Mie naanza kupata wasiwasi na wanasiasa wa aina nako.Wewe bado unaendeleza siasa za makundi ila kwa wakati mwingine unaonekana haupo!punguza jzba na utakuwa bora tu!

Nakushauri usiwe unakurupuka tu kuongea mambo ila anza kujua chanzo ni nini?

Jifunze kutoka kwa Mwanakijiji kwa upande mmoja,ila kw aushabiki wake wa kushadadiia chama flani kipindi flani ndiko mie huwa ananiboa,otherwise,Mzee unaweza

Swali la kwanza kama nimekuelewa, mimi nafanya kazi CCM makao makuu kama Katibu Msaidizi Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, na pia ni mkuu wa Kitengo cha Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Nikweli si lazima kuwa mwanasiasa ili kuwasaidia watanzania na wala si ng'ang'anii kuwa mwanasiasa, bali ndio chaguo langu nililochagua utumishi wa kisiasa, sijui kazi nyingine kama wengine walivyochagua kazi zingine.

Tofauti na watoto wengine wa "vigogo" mimi nimesoma kama watoto wengine wakawaida kabisa na wakati mwingine kwa shida kuliko wengi wetu hapa. Nikukumbushe BODI YA MIKOPO SIYO WATUNZI WA SERA BALI CHAMA TAWALA NDIO HUTUNGA SERA NA KUZITAFISIRI KWENYE ILANI YA UCHAGUZI, NA KISHA WAKIPEWA RIDHAA NA WANANCHI HUUNDA SERIKALI KUZITEKELEZA HIZO SERA...

Huu ndio utaratibu hivyo bodi iliundwa na serikali kutekeleza sera ambazo tayari zipo ninazoamini hazina matatizo bali mkakati wa kutekeleza hupangwa na serikali ndo maana nikasema, liko tatizo katika utekelezaji wake siyo swala la bodi, Bodi si wapangaji wa SERA , wala MKAKATI WA KUTEKELEZA ni watekelezaji tu.
 
Tofauti na watoto wengine wa "vigogo" mimi nimesoma kama watoto wengine wakawaida kabisa na wakati mwingine kwa shida kuliko wengi wetu hapa. Nikukumbushe BODI YA MIKOPO SIYO WATUNZI WA SERA BALI CHAMA TAWALA NDIO HUTUNGA SERA NA KUZITAFISIRI KWENYE ILANI YA UCHAGUZI, NA KISHA WAKIPEWA RIDHAA NA WANANCHI HUUNDA SERIKALI KUZITEKELEZA HIZO SERA... Huu ndio utaratibu hivyo bodi iliundwa na serikali kutekeleza sera ambazo tayari zipo ninazoamini hazina matatizo bali mkakati wa kutekeleza hupangwa na serikali ndo maana nikasema, liko tatizo katika utekelezaji wake siyo swala la bodi, Bodi si wapangaji wa SERA , wala MKAKATI WA KUTEKELEZA ni watekelezaji tu.

Mkuu Nape,

Hivi sera na ilani vinategemeana?

Pili,
Wewe si nimesikia umemaliza shule tu huko India majuzi?Huko ndiko kusoma na watanzania waliosoma Pale Mlimani,SUA ?
 
Mkuu Nape,

Hivi sera na ilani vinategemeana?

Pili,
Wewe si nimesikia umemaliza shule tu huko India majuzi?Huko ndiko kusoma na watanzania waliosoma Pale Mlimani,SUA ?

Mkuu Gembe,

Nadhani katika kuchangia kwako hapo juu,post zako mbili hapo unaingilia zaidi katika masuala binafsi kuliko kitu chochote.

Pia hoja yako ya kwamba kusoma India ni kama vile kunamuondolea mtu hali ya kuwa mtu wa kiwango cha kawaida,Kuna wengi pia tumesoma huko na wengine tunaendelea kusoma huko tukiwa watoto wa wakulima kabisa.

Pia hadi sasa India kuna watanzania wapo wansomeshwa na bodi ya mkopo,rejea katika vigezo vya kumpatia mkopo.Ni sifa ipi mtu anastahili kuwa nayo ili apatiwe mkopo.Ingawa kwa case kama ya Nape sijui kama alisomeshwa na serikali,chama au yeye mwenyewe lakini ukweli ni kwamba kuna watoto wa wakulima wapo India,China na hata nchi za ulaya

Pia,Gembe sioni mantiki ya wewe kumtaka Nape awatishe vijana eti,muda wanotumia kugoma vijana wengine duniani wako masomoni kutafuta mbinu za jinsi ya kutumia raslimali chache ili kushindanisha mataifa yao.Je kabla hujafikiria haya yote,umejiuliza hali na mazingira ya elimu ya hao wanafunzi wa mataifa mengine ya kitaaluma? Je umejiuliza kwa nini wenzetu hao hawana matatizo kama ya kwetu?

Mkuu Nape,

Naona unajichanganya kiasi kwenye hoja zako.Kwani utekelezaji wa sera ya mkopo unaofanywa na bodi umeenda kinyume na sera yenyewe?

Nadhani lengo lako ni kutaka kulinda stutus quo ya chama lakini kamwe chama na hata Maghembe mwenyewe hawawezi kujinasua kwenye hili tatizo maanke nimeshaona dalili za kuutwisha huu uchafu Bodi ya Mkopo.
 
Wakuu Ben na Gembe, nashukuru kwa hoja zenu na maswali yenu pia.

Nainze na Gembe,

(SERA NI MTAZAMO MZIMA WA KITU UNACHOTAKA KUKIJENGA/KUKIFANYA KWA UJUMLA-si tafisiri rasimi ya sera), kwa lugha nyingine ni tafisiri ya Itikadi.

Sasa uhusiano wa sera na Ilani ni kuwa Ilani inaeleza mabo ya kufanya katika kipindi flani cha makataba wenu na wana nchi, nikama break down ya sera zenu lakini katika uhalisia wa utekelezaji wa sera husika.Wapo wanoiita Ilani kuwa ni mjumuiko wa ahadi za chama flani kwa wananchi kwa kipindi cha uongozi wao.

Sasa inapokuja kwenye kuitekeleza Ilani, inahitajika methodolojia ya kuitekeleza ambayo kimsingi hutengenezwa na wataalamu(technoctrats)/ serikali, ndo maana Rais alipounda baraza la mawaziri alipita kila wizara na kuwaagiza watengeneze mpango wa kazi katika kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM, kwani ndio chama tawala kwa kipindi hicho.....Sasa hili la sera ya elimu lipo wazi kwenye Ilani ya uchaguzi kwamba elimu itatolewa kwa kuchangia...namna ya kutekeleza uchangiaji ndipo penye maneno, kwa mfano kwa sasa moja ya kelele kubwa ni kuwa utaratibu wa kuweka makundi katika uchangiaji ni mbovu, na hili la uchangiaji si jipya hata hao waliokuwa wakisemwa kusomeshwa bure na mwalimu haikuwa bure bali walikuwa wanakopeshwa na baada ya hapo wakiajiriwa wanakatwa kwenye mishahara yao, tofauti hapa ni kuwa walikuwa wakilipiwa kwa asilimia mia moja lakini sehemu ni msaada wa serikali na sehemu ndio wanakatwa baada ya kupata ajira.

SO utaona hapa swala nio utekelezaji, NA KWAKWELI SWALA HAPA SIO BODI NI SERIKALI KUWAELEKEZA BODI NAMNA BORA YA KUTEKELEZA SERA HIYOHIYO NA SERIKALI IKAE NA WADAU KUJUA NJIA BORA ZAIDI ILI KUEPUKA UTARATIBU WA KU IMPOSE MAMBO BADALA YA WANANCHI KUTOA WENYEWE NJIA NZURI KULINGANA NA MAZINGIRA....
 
Mkuu Nape,

Hivi sera na ilani vinategemeana?

Pili,
Wewe si nimesikia umemaliza shule tu huko India majuzi?Huko ndiko kusoma na watanzania waliosoma Pale Mlimani,SUA ?

Nadhani Ben kakujibu vizuri juu ya kusoma India na bahati nzuri wakati nasoma India naye alikuwepo. KIFUPI NIMESOMA NA WATOTO WA WAKULIMA KABISA INDIA NA ASILIMIA 60% YA MASOMO YANGU NIMELIPIWA NA BODI YA MIKOPO, MKOPO NA SEHEMU ILIYOBAKI NI MKOPO WA MSHAHARA WANGU CCM, AMBAO BADO NAKATWA DENI MPAKA LEO, NA SEHEMU NDOGO MARAFIKI NA NDUGU WALINICHANGIA.

Lakini nimesoma shule ya msingi Mwanga Singida, kijiji ambacho hata umeme mpaka leo HAKUNA, nikaenda sekondari ya kutwa Ngudu, ambapo tulipanga mtaani tena ni kijijini ili kusoma maji tulichota kisimani tena na kubeba kwa kichwani.

Yapo mengi ndo maana nikasema mimi ni kama watoto wengine wa kawaida wa kitanzania.....
 
Naungana kabisa na M-bongo kwa maoni ya uchambuzi juu ya nafasi ya makamu mwenyekiti wa UVCCM. Ni dhahiri kabisa kuwa wagombea wote walioteuliwa wana haki kabisa ya kugombea na kuchaguliwa kushika wadhifa huo. Hata hivyo nadhani ni vema busara ingekutimika zaidi kwa hawa wagombea wengine ambao tayari ni wajumbe wa NEC kwa lengo la kuongeza idadi ya vijana ndani ya kikao muhimu kabisa cha NEC.Maana hata ukiyasoma majukumu ya nafasi ya makamu mwenyekiti,kwa mwanasiasa makini na mwenye upeo wa kimtazamo,huwezi kutumia nguvu nyingi kuisaka nafasi hii hashwa kwa wale ambao ni waNEC tayari.Si kila jambo linataka ushindani tu,nadhani hata busara inahitajika ikiongozwa na ukomavu wa kisiasa.
Tom, its too cheap to support M-bongo's idea of allow Bashe's nomination simply because other contestants are already NEC members. Bashe's team is required to prove whether their contestant is capable of fulfilling the duties and responsibilities of the post! Tofauti na hivyo mtaendelea kuonekana mnaendeleza 'cheap campaign' kwa huyo mgombea wenu. Haiwezekani kuchagua kiongozi kwa kigezo cha kuongeza uwakilishi hata kama hafai, aje na style nyingine!
 
Nnauye Jr

Bwana kwanza kabisa Pole! Pili Hongera!. Nadhani kati ya political incidences ambazo zimetusaidia waTanzania wengi kutaka mabadiliko ya haraka ni ya Kwako vs UVCCM, MKono Nimrod vs UWZCCM, na Rita Mlaki vs UWT-CCM. Kam Chama Tawala hakiwezi kujenga misingi ya 'Political Evolution' miongoni mwao , hakuna namna yoyote ile watakayo ruhusu any form of Revolution kwa manufaa ya Taifa hili.

Mimi sijali kama utabaki CCM au kutoka almradi you stick to your true political values and instincts, join forces with other like minded characters regardless of their political affiliation to fight for a truly democratic society. It is amazing kwamba ni wewe tuu mpaka sasa ulie raise issue ya Ufungaji wa Vyuo Vikuu kwa visingizio vy a kisisiasa baadal ya kutumia busara kupitia utekelezaji wa sera ya uchangiaji yenyewe. Chiligati anapaswa kufahamu kwamba enzi za invoke Foreign involvement, au Opposition parties ilitumika Miaka ya Rais Mstaafu Mwinyi na Matokeo yake yanafahimika. Serikali hii hii ya CCM ikakamia kuwaadhibu vijana hadi kufikia umauti. Km Kaishoji Bazigiza(RIP), Na Matiko Matare(Sina hakika kama ni Marehemu au la) . I hope kwamba this should not repeat this time round.

Kila MTanzani ana haki ya kuparticipate katika political process katika ngazi yoyote ile bila kubaguliwa. maamuzi yafanywe na wapiga kura na siyo NEC , Katibu Mkuu au the So-Called Vigogo.

Hivyo, msimamo wako ulionyesha umuhimu wake unaweza usionekane leo but perharps in the future. Sisi wengine the bigger picture is the Change not the "Party Politics". Una bahati kwamba japo huna li-post kubwa but nothing you say will not have any significant political impact . Charge ON!!!
 
Comrade Nape,

I think you deserve to be congratulated for the courage shown in standing up for the democratic values you believe in. You may never know the true extent of how your incidence and those of Nimrod Mkono vs UWWZ-CCM, Rita Mlaki vs UWT-CCM, have contribute towards the developing wave for change in Tanzania. I just want to give you a simple piece of advise, Keep focused and steady. We are watching and aware of all that goes on even in the darkest corners of the political arena.

It is also worth noting that you are the only politician attached to CCM who had the courage to raise the fate of University students handled in such an incompetent manner by Maghembe and the Calamitous intervention of the uninformed Chiligati. Hakuna cha Mataifa ya kigeni wala Upinzani kuwatumia Wanafunzi.

Ukweli ni tatizo za sera yenyewe. Natumaini kuwa hiyo speed iliyotumika kumfikisha Some innocent Mtatiro mahakamani , itatumika vile vile kuwafikisha kina Rostam na wenzake waliobaki ili tujue ukweli, hawa na mafisadi ndiyo wenye ajenda ya siri, kwanini Chiligati hakulizungumzia hili kama ana uchungu wa kweli na amani na usalaama wa Taifa letu.

Mimi nadhani nafasi ulionayo Nape usiitumie kujibu allegations na udaku bali tujadiliane namna ya kulet mabadiliko ya kweli Tanzania, Kenya ilibidi watu walio na uchungu wa maendeleo ku-ditch mavyama yao na kuwa na Rainbow coalition , walipoona ujinga unazidi wakatoka na kuunda ODM, matokeo yake mawziri ishirini hawana nafasi hata za ubunge sasa wanataka kubadilisha katiba, na mengine yet wao wana equal chance to contest for political postions. Why not Tanzania, why should a poltical fate ya kijana kama wewe iwe determined by Commander wa Vijana, Makamba na Nchimbi? In whose interest?

Kama umeamua kweli kupambana na hili jinamizi la kisiasa, focust on the bigger picture " Change at any cost" mambo ya kina Beno sijui mzanzibari, sijui wewe ni mlalahoi au kigogo ni diversion siajabu toka humo CCM. Jumuiya zake zote zinalumbana, hat katawi kake uingereza ni ubabe,majungu na starehe tuu. Thsi give you a clear indication of l;ack of any serious agenda, the Real agenda that Mr Chiligat sould be made aware of is "Political Revolution" through people power. Karibu aisee huku kugumu lakini tutafika tuu at any cost.Hivyo umewahi.
 
Ahsante sana sana ndugu yangu Mpendakwao!! Ahsante sana kwa muda wako ulotumia kuandika maneno ya busara na too encouraging, thanks a lot. Nimefarijika kuona wapo vijana na watanzania ambao wanaweza kuwa na uzalendo kwa nchi yao na wasiathiriwe na ITIKADI ZA VYAMA VYAO, MIMI NAAMINI TANZANIA ITAJENGWA NA VIJANA WENYE UZALENDO KWA NCHI YAO, UZALENDO AMBAO INAPOFIKIA MAHALI ITIKADI ZA VYAMA VYAO ZINAPOSHINDWA KUULINDA UZALENDO KWA NCHI YAO WAPO TAYARI KUSIMAMIA UKWELI....

Narudia kukushukuru kwa dhati karibu sasa tujadili mustakabali wa nchi yetu,leteni hoja tujadili naamini katika mijadala hii na tukiwa wak kweli bila unafiki tutafika mahali pazuri...Wazee wetu walodai uhuru walitimiza wajibu wao, kama binadamu pengine walikuwa na mapungufu pia, lakini ni wajibu wetu sasa kuijenga nchi yetu, sisi si wengine na itawezekana tu tukipata watu wasioota ndoto za ukoloni kila wanapoona mabadiliko yananukia.

I STRONGLY BELIEVE THAT CHANGES IN THE POLITICAL ARENA IN TANZANIA ARE INEVITABLE NOW, GIVEN TIME MAENEO YOTE YA MAISHA YA MTANZANIA YATABADILIKA, BUT TUANZE NA SIASA YETU.....NIMEPENDA SLOGAN....CHANGE AT ANY COST....IT SI POSSIBLE, PLAY YOUR PARTY!!
 
Heshima mbele sana bro, haya maneno ni mazito sana na ubarikiwe tu na pia heshima kwako kuchukua muda kuja hapa kutuweka sawa ni matumanini yangu kua viongozi wengine wataiga mfano wako na kuja hapa kubeba misalaba yao, saafi sana kijana.

Ubarikiwe na Mungu Aibariki Tanzania.
 
AJitoe then ajitoe upinzani arudi tena CCM...? Kama ameamua kupambana ndani ya CCM, let it be....

Kwani siasa mapaka uwe ndani ya chama cha kisiasa? Karibu Nape na asante kwa kujibu hoja. Sounds beautiful
 
Nnauye,

Ningependa nikurudishe nyuma kidogo,kwanza kabisa mimi sijui hizi kaiba za vyama ikiwemo ya ccm/umoja wa vijana.

Sasa nilitaka kujua hili la uchaguzi wa vijana,je kuna kalenda ambayo inaongoza hizi chaguzi au kuna utaratibu gani uliokuwepo ambao unaongoza hizi chaguzi.

Nina uliza hivi kwa sababu wewe binafsi swala la umri lilikuwa ajenda ktk kugombea moja ya nafasi ktk chama.

je kigezo cha umri kiaangaliwa siku ambayo uchaguzi utafanyika au siku ambayo fomu zinatolewa,hii ina maana hata kama uchaguzi utaahirishwa au kusogezwa mbele hauta hathiri umri wa mgombea.
 
Back
Top Bottom