CCM yampiga chini Makamba

Ochu

JF-Expert Member
May 13, 2008
975
47
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimemteua mgombea wake wa ubunge jimbo la Mbeya Vijijini na kumwengua katibu wake mkuu, Yusuf Makamba katika safu za mbele za kutetea ushindi katika uchaguzi huo.

CCM inafanya mikakati mizito ya kuhakikisha hakianguki kwa mara ya pili mfululizo baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupata ushindi mkubwa kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Tarime, ambako CCM iliongozwa na Yusuf Makamba.

Kuanguka kwa CCM kulisababisha lawama kubwa dhidi ya Makamba kiasi cha kubashiriwa kuwa mkuu huyo wa zamani wa mkoa wa Dar es salaam angevuliwa ukatibu mkuu wa chama wakati wa mkutano wa Halmashauri Kuu uliofanyika Dodoma karibu mwezi mmoja uliopita.

Makamba aliokoka baada ya kikao hicho kuisha bila ya kumjadili, lakini sasa hataongoza kampeni ya kutetea kiti kilichoachwa wazi na Richard Nyaulawa aliyefariki dunia kutokana na kuugua kwa muda mrefu.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Makamba sasa hatakuwa msimamizi mkuu bali mwangalizi na mwezeshaji wa kampeni.

"Makamba sasa hatajikita moja kwa moja katika usimamizi wa kampeni hizo kama ilivyokuwa Tarime badala yake atakuwa na kazi ya kuangalia na kuwezesha kampeni hizo," alisema Chiligati.

Alisema uamuzi wa kutomuweka Makamba kuwa msimamizi mkuu unatokana na mkakati wa chama hicho kuiachia CCM Mkoa kufanya kazi hiyo, badala ya kuongozwa na CCM Taifa.

"Makamba atakuwa akienda Mbeya kuwezesha kampeni hizo na kurudi," alisema Chiligati. "Kamati ya uchaguzi ya mkoa wa Mbeya ndiyo yenye jukumu la kusimamia uchaguzi huo."

Katika uchaguzi wa jimbo la Tarime, Makamba alilaumiwa kuwa hakufanya jitihada za kuondoa tofauti za makundi yaliyoibuka wakati wa uchaguzi wa mwaka 2005, moja likidaiwa kuongozwa na Kisyeri Chambiri na jingine likidaiwa kuongozwa na Chrisopher Gachuma.

Makamba anadaiwa kuegemea kwenye moja ya makundi hayo na hivyo kuwafanya baadhi ya Wana-CCM kutomuunga mkono mgombea wake, Christopher Kangoye.

Makamba pia alidaiwa kutotumia wazawa wa Tarime kwenye kampeni hizo na badala yake kuwatumia wapiga debe waliojiunga na CCM kutoka vyama vya upinzani, huku lawama nyingine zikielekezwa kwa kada huyo kwa kushindwa kwenye uchaguzi licha ya kuwezeshwa kila kitu, zikiwemo helkopta mbili.

Kuhusu mgombea wa CCM kwenye jimbo hilo la Mbeya Vijijini, Kapteni Chiligati alimtangaza Mchungaji Luckson Mwanjale kuwa ndiye aliyeshinda katika uteuzi huo uliofanywa na Kamati Kuu ya CCM (CC) jijini Dar es Salaam jana.

Alisema Mwanjale amewashinda wenzake kadhaa, akiwemo aliyekuwa mkuu wa majeshi mstaafu, Robert Mboma aliyepata kura 164.

Wengine walioshiriki katika nafasi ya kugombea kuteuliwa ni Allan Mwaigaga, aliyepata kura 259, Adrea Sayile (229), Diovita Diame (162), Petro Mwashusha (28),Flora Mwalyambi(26), Machael Mponzi (23) na Maria Mwambanga(19).

Alisema kampeni za uchaguzi huo wa Mbeya Vijijini zitazinduliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi Januari 4 mwakani.

Uchaguzi mdogo jimbo la Mbeya Vijijini utafanyika Januari 25 mwakani kuziba pengo la aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Richard Nyaulawa aliyefariki dunia Novemba mwaka huu kwa ugonjwa wa saratani.

Wakati CCM imemteua mgombea wake, Chadema ilimteua Sabwee Shitambala kukiwakilisha katika uchaguzi huo utakaohusisha pia Chama cha Wananchi (CUF). Mgombea wa CUF anateuliwa leo kwenye mkutano mkuu wa CUF wilayani Mbeya Vijijini
 
CCM ya sasa bwana ..naungana na maneno ya mama wizi mtupu!
 
Chiligati na Makamba wana tofauti kweli ? Mie naona wote ni wale wale
 
Ni kwamba CCM Mbeya vijijini walipeleka ujumbe usio rasmi kwa JK, kwamba kama anataka wao washiriki kwenye kampeni basi Makamba asikanyage kwenye shughuli hiyo. Wakipinga hilo wao watajua wa kumpa ubunge.
Naona CC CCM imebidi ifyate.
 
Chiligati na Makamba wana tofauti kweli ? Mie naona wote ni wale wale


Mkuu Lunyungu.

Mkuu Chili yeye ana matatzio yake ambayo kw akiasi flani yanafanana na uya mzee Makamba,yeye naye ni mropokaji ila uzuri wake huwa ni mjanja sana akishagundua amekosea.huwa anarudi na kugeuza alichokisema.

Ni watu ambao wanadhani mawazo yao ndiyo yanaweza kufanya kazi.Makamba angeweza kung'oka ila tatizo ni kupata mtu mwingine ambaye atachukua nafasi ya Makamba.

Kuna kipindi Mzee waliwahi kumuomba kinana achukue jahazi ila nadhani aliwakatalia kutokana na political Move yake na mlengo wake saababu hawa bado wana ndoto za urais.

Nina uhakika Wapinzani waapaka taabu sana mwaka huu.Timu ambayo iko chini ya Tinga tinga itasambaratisha kila kitu na nina uhakika jimbo litanyakuliwa.Walifanya makso mwanzoni na sifikirii kama wako tayari kurudia tena kuwapeleka watu wa ina ya Msekwe katika kampeni.

Suala ambalo limenishtua .Nape yumo katika timu ila cha kujiuliza nani alimtuma Nape kuongea maneno ya kipindi kile?Yes anajua wnasiasa wote ni oppotunist ila huyu kijana atakuwa kazidi.Nasikia alitumwa na mkwere kurekebisha khali ya kisiasa na kichama ili inoekane CCM iko makini na kuna watu ambo wanweza kuthubutu kuiponda(hii kuonyesha ukomavu wa demokrasia katika CCM).

anyway 2010 inakuja.Yangu macho ila nina uhakika Mkwere atarudi tena pale magogoni kuendeleza libeneke
 
Ni kwamba CCM Mbeya vijijini walipeleka ujumbe usio rasmi kwa JK, kwamba kama anataka wao washiriki kwenye kampeni basi Makamba asikanyage kwenye shughuli hiyo. Wakipinga hilo wao watajua wa kumpa ubunge.
Naona CC CCM imebidi ifyate.

Je, pamoja na kuwepo dalili za wazi kabisa zinazoonyesha kutokubalika kwa Makamba miongoni mwa viongozi na wanachama wengi wa chama hicho, JK ataendelea kumkumbatia Makamba!? Tusubiri maana 2010 inanyemelea taratibu.
 
Ila jamani Mbeya vijijini siyo Tarime. Hapa CCM wanatetea jimbo. Kwa mujibu wa Siasa za Mbeya, ni CCM tuu na hakuna vuguvugu kubwa la upinzani. Ila pia watu wa mbeya kama ilivyo kwa maharage ya Mbeya ni maji mara moja. Wapenda mageuzi tusieke matumaini makabwa sana ila kushiriki ni muhimu maana ndio demokrasia yenyewe.
 
Mkuu Lunyungu.

Mkuu Chili yeye ana matatzio yake ambayo kw akiasi flani yanafanana na uya mzee Makamba,yeye naye ni mropokaji ila uzuri wake huwa ni mjanja sana akishagundua amekosea.huwa anarudi na kugeuza alichokisema.

Ni watu ambao wanadhani mawazo yao ndiyo yanaweza kufanya kazi.Makamba angeweza kung'oka ila tatizo ni kupata mtu mwingine ambaye atachukua nafasi ya Makamba.

Kuna kipindi Mzee waliwahi kumuomba kinana achukue jahazi ila nadhani aliwakatalia kutokana na political Move yake na mlengo wake saababu hawa bado wana ndoto za urais.

Nina uhakika Wapinzani waapaka taabu sana mwaka huu.Timu ambayo iko chini ya Tinga tinga itasambaratisha kila kitu na nina uhakika jimbo litanyakuliwa.Walifanya makso mwanzoni na sifikirii kama wako tayari kurudia tena kuwapeleka watu wa ina ya Msekwe katika kampeni.

Suala ambalo limenishtua .Nape yumo katika timu ila cha kujiuliza nani alimtuma Nape kuongea maneno ya kipindi kile?Yes anajua wnasiasa wote ni oppotunist ila huyu kijana atakuwa kazidi.Nasikia alitumwa na mkwere kurekebisha khali ya kisiasa na kichama ili inoekane CCM iko makini na kuna watu ambo wanweza kuthubutu kuiponda(hii kuonyesha ukomavu wa demokrasia katika CCM).

anyway 2010 inakuja.Yangu macho ila nina uhakika Mkwere atarudi tena pale magogoni kuendeleza libeneke[/SIZE]

Mkuu hebu tupe story zaidi juu ya hii combination yaani Masauni, Benno na Senetor Nape!!!!!!!! Mbona kama mkubwa anatuma salamu kuwa ni MWENYEKITI WA UVCCM, MAKAMU MKITI NA KATIBU MKUU WAO?? Kama pia hayo ya uhusiano wake na mkwere ni wa kweli maana kwa taarifa niliyokuwa nayo siku moja kabla ya CC mkwere na Nape walikutana ikulu kwa masaa matatu THREE HOURS!!!!!!!!! Nini kinaendelea. N a je huu ndio mwisho wa Makamba????????? maana kama alisimama na kutangaza hadharani kuwa Nape hafai kabisa, leo CC inaona anafaa kuongoza mapambano Mbeya na Makamba abaki mbali, hii inashangaza Na je ni janja ya CCM kumpa Mwandosya kijana wake Nape kufanya naye kazi pale??
 
Tinga tinga ana aminika kwa nguvu za chini chini kuiba kura na kununua shahada.CCM kwa sera jukwaani hawawezi labda kutumia polisi na maguvu .Je akishindwa nako itakuwaje ?
 
Msisahau kuwa jimbo la mbeya liliwahi kuwa chini ya himaya ya NCCR na hawa jamaa wanajua CCM haiwapendi toka Kikwete aingie madarakani, hata akamteua Mwakipesile aliyeshindwa ubunge kyela kuwa RC; Kwa mkoa wa mbeya haya yalikuwa matusi makubwa sana. Juu ya yote hayo watu wa Mbeya hawamo sana katika hii serikali ya awamu ya nne na kiza totoro kutokana na kukosa umeme vyote vikitumika vizuri kuonesha mapungufu ya CCM hata wakimleta tingatinga wapinzani wanaweza kulikomboa jimbo la Mbeya vijijini
 
.....wako gizani baada ya miaka 50 ya uhuru na bado wanaipigia kura CCM? hawa wana deserve kuendelea kula giza mpaka yesu arudi(kama yupo kweli),na tingatinga ndio nani?
 
Ikiwa CHADEMA itashinda Mbeya vijijini, jambo ambalo naliombea kwa akili na nguvu zangu zote,kutakuwa na athari chanya na pana kwa maendeleo ya demokrasi Tanzania.Ndio mgeuko ambao wanaharakati wengi wanausubiria. Tarime ulikuwa mwanzo mzuri lakini leo CCM inafanya jitihada nyingi kuonyesha kuwa lile likuwa jimbo la CHADEMA na wamefanikiwa kulirejesha, wanayasema haya kwa makusudi ya kudhibiti msisimko wa kisiasa miongori mwa jamii, wanajaribu kupunguza nguvu itokanayo na taathira ya matokeo ya uchaguzi wa Tarime kwa minajili ya kulinda hatma na hadhi ya CCM inayoendelea kuchuja kila uchao.

Ikiwa CHADEMA itashinda Mbeya Vijijini kutakuwa na matumaini makubwa sana miongoni mwa wananchi na pengine kutengeneza mazingira ya kushuhudia uchaguzi wa kishistoria mnamo mwaka 2010. Kwa CHADEMA iwe vita ya kufa na kupona, mbeya vijiji ndio kwenye "ufunguo wa maji ya uzima" katika medani za siasa Tanzania.Kutapatapa huku kwa CCM ni kilelelezo cha kutambua umuhimu na pengine ugumu wa jambo wanaloenda kukaribiana nao.

Nikiangalia Safu ya CCM inayokwenda Mbeya naona ni mteremko, sijui ni kwanini hawakutaka kutumia ushawishi wa mwandosya na mwakyemba(mmoja wa mashujaa wa siasa za kileo TZ), Malecela anawakilisha wakati uliopita mvuto wake hauwezi kukaribia alio nao Dr. Slaa sasa, Masauni na Zito ni jua na mwezi, Beno na Mnyika, Mnyika ni mara tatu ya beno, Nape sasa anao mtaji wa kisiasa lakini ubingwa wa Tundu lissu katika kucheza na kupangua hoja utafifisha na kuyeyusha umaarufu wake, hapo Mtuhuru anaendelea kuwa akiba ya ziada kumalizia mapengo ya hapa na pale, kwenye siasa za ardhini ambazo malecela anasifika kuwa bingwa wake sasa atalazimika kupambana na wale vijana matata ambao tayari wamefanya utafiti kule mbeya vijijini( hawa ni unsang hereos) ni engine muhimu sana. Ni mpambano mzuri sana wa kisiasa. Japo kwa hali ya jumla CHADEMA itakuwa inapanda mlima wakati CCM inashuka kiteremko kwa kuwa CHADEMA haijajijenga vya kutosha kule lakini hatuko tayari kupuuza au kuukana uwezekano wa CHADEMA Kuwapa watanzania zawadi ya mwaka mpya. Mda utasema
 
Mkuu Koba, heshima mbele ; Tinga Tinga ni huyu mzee mbunge wa Mtera anayetumiwa na CCM lakini ukifika wakati akichukua fomu kutaka uongozi wa juu wanamwambia ' HACHAGULIKI". Sasa wakiwa na chaguzi zao wanampeleka kwenye kampeni huku CC yao inasema hafai uongozi wa juu. Kichekesho ni kwamba juu ya kudhallishwa huko huyu ajuza bado anakubali kutumiwa. Vituko vya CCM hivyo!!
 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimemteua mgombea wake wa ubunge jimbo la Mbeya Vijijini na kumwengua katibu wake mkuu, Yusuf Makamba katika safu za mbele za kutetea ushindi katika uchaguzi huo.
..................!!!!!!!
Kuanguka kwa CCM kulisababisha lawama kubwa dhidi ya Makamba kiasi cha kubashiriwa kuwa mkuu huyo wa zamani wa mkoa wa Dar es salaam angevuliwa ukatibu mkuu wa chama wakati wa mkutano wa Halmashauri Kuu uliofanyika Dodoma karibu mwezi mmoja uliopita.

......................!!!

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Makamba sasa hatakuwa msimamizi mkuu bali mwangalizi na mwezeshaji wa kampeni.
.............................!!!!!!!!
Makamba anadaiwa kuegemea kwenye moja ya makundi hayo na hivyo kuwafanya baadhi ya Wana-CCM kutomuunga mkono mgombea...

The writting is on the wall.CCM inabidi ijipange upya katika safu yake ya uongozi.Mze Makamba, kada wa siku nyingi wa CCM amelalamikiwa sana na wanachama wenyewe wa CCM kwa kuonyesha udhifu mkubwa katika uongozi wa chama hiki kikubwa kuliko vyote nchini.
Ni ukweli usiopingika kuwa uwezo na Mzee Makamba haulingani kabisa na ule wa akina Msekwa, Mwakawago au na hata Mangula.
Katika nafasi aliyonayo Mzee Makamba mtu anatakiwa kuwa master strategist and foward thinker, kwa kutilia maanani msimamo wa chama chake.
Sijui kama ni katika exposure ya elimu ya kitikadi au upeo tu kwa ujumla.Hata hivyo bla bla zinaonekana kuwa zimefikia ukomo.
Ushauri wa bure kwa CCM ni kuwa come 2010, makundi hasa katika ngazi ya uongozi ndiyo yataipunguzia ushindi.
 
HTML:
[COLOR="Teal"][B][I]Makamba:Sijaenguliwa, ni utaratibu 


Na Jackson Odoyo


SIKU moja baada ya Kamati Kuu ya CCM kumuengua katibu Mkuu wake Yusufu Makamba kuongoza kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Mbeya Vijijini, Yusuf makamba amejitetea kuwa hajaenguliwa, bali huo ndio utaratibu mpya wa chama chake.


Makamba ndiye aliyekuwa kinara wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Tarime ambako CCM iliangushwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), lakini sasa hatasimamia tena kampeni kwenye jimbo la Mbeya Vijijini baada ya Kamati Kuu ya CCM kuamua kuuachia mkoa jukumu hilo.


Kutokana na kushindwa kwa CCM kwenye jimbo la Tarime, Makamba, ambaye ni katibu mkuu wa chama hicho, alilaumiwa sana akidaiwa kushindwa kuzika tofauti zilizoibuka kwenye uchaguzi wa mwaka 2005, kutumia wapiga debe kutoka Dar es salaam ambao walihamia CCM kutoka vyama vya upinzani, na kushindwa kutumia vizuri vitendea kazi alivyopewa, ikiwa ni pamoja na helikopta mbili kwenye uchaguzi huo unaosemekana kuwa ulitumia fedha nyingi.


Lakini Makamba, akiongea na Mwananchi, alisema kuenguliwa kwake kunatokana na CCM kubadilishwa kwa utaratibu, akidai kuwa CCM ina utaratibu wake na mbinu nyingi za kufanya kampeni.


“Huu uliotumika ni moja kati ya taratibu zetu na si kwamba nimeondolewa,” alisema na kuongeza:


“Mimi sijaondolewa ila mimi safari hii ni mwezeshaji katika kampeni hizo na kazi yangu ni kuangalia mahitaji muhimu wakati wa kampeni, mfano kamati ikiniambia niwapelekee flana nitapeleka; wakiniambia wanataka fedha, nitawapa; wakiniambiwa niwape usafiri wa magari ama helikopta, pia nitawapa.


“Tarime tulikwenda na tukakaa huko kipindi chote cha kampeni na huo ulikuwa utaratibu wetu. Safari hii tutakwenda kusaidia kampeni na kurudi, huo pia ni utaratibu wa CCM.


"Mfano mimi ninakwenda Januari mbili, na Januari tatu tutakuwa na mkutano wa kamati ya siasa, January nne ni siku ya uzinduzi baada ya hapo nitaongoza kampeni hadi Januari saba na baadaye nitarejea Dar.”


Alisema baada ya kurudi ataendelea na majukumu mengine ya kazi na akitaka kwenda Mbeya siku yoyote ataenda na kwamba hakuna wa kumzuia kwa sababu yeye ndiye msimamizi.


Makamba pia alirejea kauli yake kuwa alikubali kupokea lawama katika uchaguzi wa Tarime kwa sababu yeye ni kiongozi wa chama na kwamba endapo CCM ingeshinda katika uchaguzi huo, ni yeye ambaye angepongezwa.


Aliongeza kwamba hata katika uchaguzi huo wa Mbeya Vijijini, CCM ikishindwa tena yuko tayari kupokea lawama kwa kuwa ni kiongozi na kwamba wala hawezi kuwazuia wanachama kumlaumu.


“Kulaumiwa ni kitu cha kawaida kwa kiongozi yeyote na ukiogopa lawama huwezi kuwa kiongozi," alisema.


Uchaguzi huo unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Richard Nyaulawa kufariki dunia wiki chache zilizopita.


Katika Uchaguzi huo CCM imemsimamisha Mchangaji Luckson Mwanjale[/I][/B][/COLOR]
.
 
Mkuu hebu tupe story zaidi juu ya hii combination yaani Masauni, Benno na Senetor Nape!!!!!!!! Mbona kama mkubwa anatuma salamu kuwa ni MWENYEKITI WA UVCCM, MAKAMU MKITI NA KATIBU MKUU WAO?? Kama pia hayo ya uhusiano wake na mkwere ni wa kweli maana kwa taarifa niliyokuwa nayo siku moja kabla ya CC mkwere na Nape walikutana ikulu kwa masaa matatu THREE HOURS!!!!!!!!! Nini kinaendelea. N a je huu ndio mwisho wa Makamba????????? maana kama alisimama na kutangaza hadharani kuwa Nape hafai kabisa, leo CC inaona anafaa kuongoza mapambano Mbeya na Makamba abaki mbali, hii inashangaza Na je ni janja ya CCM kumpa Mwandosya kijana wake Nape kufanya naye kazi pale??

Mkuu Achebe,

Siasa za nchi bwana ,na hasa Vyma vyote ambavyo ni vikubwa zinaendeshwa kisanii sana na kizugaji hasa.

Unaweza ukafikiri EL ana umgomvi na Mkwere na magazeti yakapamba sana ugomvi huu na waandishi maarufu(wahariri ambao wanaitwa na kupewa pesa nyingi) ili ionekane hawapendane.

Nape ni mtu wa system muda mrefu sana na wanamtegemea sana katika kampeni zao.Yeye kukemea CCM ilikuwa ni jambo alilotumwa na serikali ili kurudisha imani kwa wananchi.Kumbuka nilishawahi kusema kuna watu walipewa kazi ya kudhibiti khali mbaya ya Serikali.

According to the Dataz ni kuwa Mtoto wa EL alikuwa na Mazungumzo na Beno kabla Benno hajaenda kumalizia kampeni zake huko kanda ya ziwa na haijulikani walikuwa wanazungumza nini ,ila wadadadisi wanaelezea alikuwa akielezwa ni jinsi gani watakavyoshinda.On the other side Benno ni rafiki wa Riz.Now you can know what i mean.

Wapinzani ni hivyo hivyo,utasikia mtu kajitokeza kumng'oa Dr Slaa au Prof Lipumba,ila yote hii ni kupima na kukipa chama umaarufu na watu wasikisahau.

Mpaka leo ukiiuliza watu ambao wanijua sera ya CHADEMA kwa mji mkubwa kama hapo nyumbani Dar e es salaam utakuta ni wachache sana(ukijumuuisha na wanafunzi wa UDSM na vyuo vingine).WAnachojua serta ya CHADEMA ni kuvumbua Ufisadi.ila Je kutokomeza ufisadi ni suluhisho la maendeleo?billion 133 zinaweza kubadilisha khali mbaya ya nchi hii?

Mie nitakuwa tayari kuunga mkono chama ambacho kitakuja na sera nzuri zinazotekelezeka.Tunahitaji watu wa aina ya Mao hapa ili nchi iendelee.Tunao vijana Bora kam Zitto(ila sasa sina imani naye baada ya kupewa kazi ya Kamati ya Madini na hii namuweka kiporo tu).

Ukiangalia sana ,ukipima sana ndiyo maana CCM huwa inashinda kila mwaka kwa kuwa hakuna ambaye anaweza kuleta Mabadiliko katika Nchi!

Hivi Tanzania kuna watu kama Chief Strategistics wa kampeni?au ndiyo wale ambao wanasema tuanzie kwanza kwa mganga pale Bagamoyo
 
Mkuu Gembe sasa umenifungua macho, maana nilikuwa nafuatilia sana sakata la Kijana Nape na kina Mmakamba na wenzake, kilichoniacha hoi ni kuwa kila mara kijana alionekana kuwa jasiri na mtulivu bila wasiwasi huku hali ilikuwa uikionyesha nakwisha kisiasa,ilipofikia at the pick of it, watu TUKAACHWA HEWANI MPAKA LEO HAKIKA SINA UJASIRI WA KUSIMAMA NA KUSEMA NANI HASA NI MSHINDI KATIKA MPAMBANO ULE, lakini kijana kafanikiwa kutengeneza NEW BRAND OF HIM........kumbe kijana wa system so alijua mwanzo mpaka mwisho wa game zima

TAARIFA NILUIZONAZO TINGATINGA LIMEKUBALI KUSHUKA MBEYA VIJIJINI BAADA YA KUHAKIKISHIWA KUWA MAKAMBA HATII MGUU MBEYA....................
 
Mbeya CCM kushinda sijui,ivi wajua mpaka leo mwezi sasa umeme ni wa mgao.
Hao CCM wangerudisha umeme kwanza ndo waingie kwa izo kampeni kwa Amani vinginevyo wameula ni mwendo wa Operation sangara
 
Back
Top Bottom