CCM yamgwaya Dk. Slaa

issenye

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
3,781
5,205
Na Chalila Kibuda

SIKU moja baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kumfungulia kesi Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, Nape Nnauye, CCM imesema haina mpango wa kukishtaki chama hicho kutokana na kudai kinaingiza silaha nchini. Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, Nape alisema chama hicho hakitafanya hivyo kwa kuwa kinaendelea kukijenga chama.

"Hutuendi mahakamani kuishtaki CHADEMA kwa kile walichodai kuwa CCM inaingiza silaha nje ya kanuni zilizowekwa na nchi," alisema Nnauye.
Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Salaa, akiwa mkoani Morogoro alinukuliwa akisema CCM imeingiza silaha nchini bila kibali, ili zitumiwe na vijana wao kukabiliana na wapinzani.
 
Anajua atashindwa kesi ndio maana hawezi kwenda kuifungua!
 
huyu dogo nape kigeugeu sana, iko wapi kauli yake ya kumshtaki Dr slaa na kudai bilioni kadhaa na shilingi moja? viongozi wa aina ya nape ni hatari sana!
 
Nape alisema atafungua kesi dhidi ya slaa kwa kusema ccm inaingiza slaa.kwa maneno haya ya nape ni dhahiri kamgwaya Dr.
 
Siku hizi CCM hawana uhakika sana na mahakama kama zamani. Lissu kawaumbu majaji vihiyo waliokuwa katika taasisi nyeti kama mahakama kwa faida ya CCM.

Kina Nape ni mpaka wawe wameandaa "timu yaoya majaji/mahakimu" ndio wanaweza kwenda mahakamani. Cheki tu ishu yao na Dr. Kafumu huko Igunga.
 
Kukijenga chama ni pamoja na kukisafisha na kashfa kama hizi ili kurudisha imani ya wanachama iliyopotea kutokana na kashfa hii kama walivyofanya cdm na kashfa ya mabilioni.
 
Kwa maonin haya nimeamini chadema ni genge la matahaira. Hivi kweli mtu na akili zake atahangaika na kauli za slaa?? Alikwisha dai anataka kuuwawa halafu akadai eti kuna kontainer zima la kupigia kura kutoka afrika ya kusini liliingia nchini. Sasa hata mtoto wa chekechea hawezi kuamini eti ccm iagize silaha. Hizo silaha zina kaa wapi kama si utahaira. Huyu babu kweli kwa kauli ya nape anazeeka na anapoteza kumbukumbu. Juzi tu alijikanyaga huku anamshtaki nape kwa kusema chadema inafadhiliwa kwenye kikao ambacho pia anakili chama cha kikristo cha ujerumani kinawafadhili. Ni chakubanga tu huyu. Kama ingekuwa cuf imefadhiliwa na chama cha waislamu ungesikia kelele za maaskofu itv. Unaweza kuachana na kichaa watu waone tofauti lakini kutokuburuzwa mahakamani hakumaanishi kuwa unanga umehalalishwa
 
Kama hujui kaa kimya,yu kwapi Imran kombe,Kolimba na etc.
 
Na Chalila Kibuda

SIKU moja baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kumfungulia kesi Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, Nape Nnauye, CCM imesema haina mpango wa kukishtaki chama hicho kutokana na kudai kinaingiza silaha nchini. Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, Nape alisema chama hicho hakitafanya hivyo kwa kuwa kinaendelea kukijenga chama.

“Hutuendi mahakamani kuishtaki CHADEMA kwa kile walichodai kuwa CCM inaingiza silaha nje ya kanuni zilizowekwa na nchi,” alisema Nnauye.
Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Salaa, akiwa mkoani Morogoro alinukuliwa akisema CCM imeingiza silaha nchini bila kibali, ili zitumiwe na vijana wao kukabiliana na wapinzani.

Edit heading yako,Sema Nape amgwaya Dk.Slaa.
 
Kwa maonin haya nimeamini chadema ni genge la matahaira. Hivi kweli mtu na akili zake atahangaika na kauli za slaa?? Alikwisha dai anataka kuuwawa halafu akadai eti kuna kontainer zima la kupigia kura kutoka afrika ya kusini liliingia nchini. Sasa hata mtoto wa chekechea hawezi kuamini eti ccm iagize silaha. Hizo silaha zina kaa wapi kama si utahaira. Huyu babu kweli kwa kauli ya nape anazeeka na anapoteza kumbukumbu. Juzi tu alijikanyaga huku anamshtaki nape kwa kusema chadema inafadhiliwa kwenye kikao ambacho pia anakili chama cha kikristo cha ujerumani kinawafadhili. Ni chakubanga tu huyu. Kama ingekuwa cuf imefadhiliwa na chama cha waislamu ungesikia kelele za maaskofu itv. Unaweza kuachana na kichaa watu waone tofauti lakini kutokuburuzwa mahakamani hakumaanishi kuwa unanga umehalalishwa

Na yeye mwenyewe Nape kuachia ngazi.
 
CCM kwenda mahakamani yaweza kuwa mwanzo wa aibu maana utakapotolewa ushahidi yaweza kuwa balaa kubwa kwa wahusika.
 
Nadhani hakuna haja ya wanasiasa kukimbilia mahakamani. Jibuni hoja tu mkianza huu mtindo kesi mahakamani zitarundikana bila sababu ya msingi. Kuropoka ni sehemu ya siasa. Kudhibitisha ni hatua nyingine. Ukiona mtu anakimbilia mahakamani jua ukweli umemchoma anatafuta pa kujisafisha. Nani asiyejua kwamba CHADEMA inafadhiliwa?? Nashauri wafute tu hiyo kesi isije ikawaumbua zaidi na kuwazibia riziki huko Conservative Union na kwa wakina RENAMO na Democratic Union of Africa. Wapo vijana wanaopata mafunzo kila mwaka kwenda nje ya nchi kupitia CHADEMA kama motisha wa kupata vijana wa elimu ya juu sasa haya yoote si vibaya na yapo kwa hiyo CHADEMA kioneshe ukomavu na kukubali kukosolewa
 
Kwa maonin haya nimeamini chadema ni genge la matahaira. Hivi kweli mtu na akili zake atahangaika na kauli za slaa?? Alikwisha dai anataka kuuwawa halafu akadai eti kuna kontainer zima la kupigia kura kutoka afrika ya kusini liliingia nchini. Sasa hata mtoto wa chekechea hawezi kuamini eti ccm iagize silaha. Hizo silaha zina kaa wapi kama si utahaira. Huyu babu kweli kwa kauli ya nape anazeeka na anapoteza kumbukumbu. Juzi tu alijikanyaga huku anamshtaki nape kwa kusema chadema inafadhiliwa kwenye kikao ambacho pia anakili chama cha kikristo cha ujerumani kinawafadhili. Ni chakubanga tu huyu. Kama ingekuwa cuf imefadhiliwa na chama cha waislamu ungesikia kelele za maaskofu itv. Unaweza kuachana na kichaa watu waone tofauti lakini kutokuburuzwa mahakamani hakumaanishi kuwa unanga umehalalishwa

Magamba bwana mna shida sana badala ya kuleta hoja unaleta viroja...
 
Nape alisema atafungua kesi dhidi ya slaa kwa kusema ccm inaingiza slaa.kwa maneno haya ya nape ni dhahiri kamgwaya Dr.
Ni kweli nakumbuka, Nape alitamba kuwa kama Slaa hatakanusha kuhusu madai yake kuwa CCM, imeingiza silaha ili iwape vijana wake, kufanya fujo, atamfungulia mashitaka.Sasa kama Nape huyo huyo sasa anasema hawezi kumfungulia kesi Slaa, ni dhahiri amamgwaya Slaa, na anajua itakapofunguliwa hiyo kesi, Dr Slaa atakuja na ushahidi mzito, ambao utawaumbua vibaya magamba!
 
Ndhani rafiki zangu wana CHADEMA hapa muwe makini kidogo. Huu umamuzi wa kukimbilia mahakamani inaweza kuwa mwanzo wa kuumbuka zaidi. Mbona mtu yeyote akinyanuliwa atasema tu kuwa CHADEMA kina vibopa wanakifadhili wa ndani na nje. Wanafahamika, wanafanya siri hasa wa ndani. Lakini wa nje wako waazi kabisa. CHADEMA ni beneficiary wa Conservative Union na Hawa wa Kristo wa Ujerumani na si vibaya sasa kuwakana inatia shaka hapa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom