CCM yajipanga kuongoza nchi kwa miaka 75 Ijayo

Wakuligo

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
259
105
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya chama katika jimbo la Peramiho linalongozwa na Mh Jenista John Muhagama amewaeleza wanachama na viongozi chama kuwa CCM imeanda mpango wa kuongoza dola kwa miaka 75 kuanzia mwaka 2025. Akizungumza katika mkutano huo,

Polepole amesema kuwa baada ya Rais John Pombe Magufuli kumaliza muda wake mwaka 2025 kuna mpango ambao uko tayari wa vipindi vitatu vya miaka 25 yani 2025 - 2050, 2050- 2075 na 2075 - 2100 kwa CCM kuongoza na kwamba kama kuna mtu anatamani kuongoza nchi hii basi asubiri hadi mwaka 2100!

Source: TBC

Sent using Jamii Forums mobile app
 
naamini kwa 100% hizi ni ndoto alizoota polepole hebu aote haraka haraka tuone yani haiwezekani ccm kutawala mpk huko watu kwasasa wanaakili Sana na ccm inatenda sluggishly mfano hayo mazingaombwe ya kikokotoo yaliyofanyika dar na mwanza ndio yaendelee kwa karne moja ijayo haiwezekani over my dead body yani nasema hivi

1.watanzania tunampango juu yenu ccm

2.Mungu anampango juu yenu ccm

hamtavuka 2030 never kwanza kinachokuja ni kugawana madaraka halafu baada ya hapo kuwafurumusha rasmi na kwasababu baadhi yenu mtakuwa hai kwasababu bado ni vijana kwasasa tutawahesabia hesabu yenu na mtalipwa sawasawa na matendo yenu ya sasa

kwa jina la Mungu aliye hai mtaanguka!!
 
Waruhusu basi vyama vingine vifanye siasa ndio waseme hayo. Bondia unajinasibu kua uko fiti na unanguvu za kumcharaza mpinzani wako kwa knockout ya mapema kabisa lakini kabda ya kutamka hayo umehakikisha mpinzani wako amefungwa kamba mikono na miguu asiweze hata kutembea. Huo ni uwoga wa hali ya juu kabisa
 
Ni jambo linaloweza kutokea iwapo wapinzani wa kweli wasipotokea ....! Wapinzani wanaosimamia misingi na kauli zao.Hawa tulionao hamna kitu ni vigeu geu..!wametuchuuza sana.sasa hivi hatujui hata kauli mbiu ya upinzani ni nini?kikija kikokotoo tumo.. .,suala la ndege tupo kulaumu...tumepoteza muda kushabikia ufipa.
 
wanataka tuwa kama nchi za 'ukomunist' et? Yaan chama kimoja kama china, nakumbuka kuna ck lissu alisema kuna wakti utafka tutaimba wimbo mmoja
 
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya chama katika jimbo la Peramiho linalongozwa na Mh Jenista John Muhagama amewaeleza wanachama na viongozi chama kuwa CCM imeanda mpango wa kuongoza dola kwa miaka 75 kuanzia mwaka 2025. Akizungumza katika mkutano huo, Polepole amesema kuwa baada ya Rais John Pombe Magufuli kumaliza mda wake mwaka 2025 kuna mpango ambao uko tayari wa vipindi vitatu vya miaka 25 yani 2025 - 2050, 2050- 2075 na 2075 - 2100 kwa CCM kuongoza na kwamba kama kuna mtu anatamani kuongoza nchi hii basi asubiri hadi mwaka 2100!

Source: TBC

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni bora kulewa bangi kuliko kulewa madaraka. Ulevi wa bangi unaishia kichwani tu lakini wa madaraka unaenda mpaka kwenye ini, konosho, firigisi, roho, mdomoni, masikioni, machoni, vinyweleo vya ngozi nk.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asisahau kuwa Kuna mwisho wa duniani. Je kama MUNGU akiamua mwisho wa duniani uwe 2020, ataenda kutawala wapi? . Hata jehanum atakuwepo mtawala wake (Ibilisi). Aache kujikinai, ajue Maisha ya hapa duniani yamo katika maamuzi ya yule aliye juu.(The Most High GOD, El Elton).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni jambo linaloweza kutokea iwapo wapinzani wa kweli wasipotokea ....! Wapinzani wanaosimamia misingi na kauli zao.Hawa tulionao hamna kitu ni vigeu geu..!wametuchuuza sana.sasa hivi hatujui hata kauli mbiu ya upinzani ni nini?kikija kikokotoo tumo.. .,suala la ndege tupo kulaumu...tumepoteza muda kushabikia ufipa.
Hii ndio shida ya watanzania hamsomi kabisa.... Unasema hawana agenda ila kitabu cha sera hujasoma.... Ilani yao ya uchaguzi hujasoma.... Bajeti mbadala hujasoma ndio maana mnakaririshwa upinzani hauna agenda

Kma haujasoma hayo maandiko niliyokutajia sishangai kusema hujui wapinzani wanachosimamia!!
 
Back
Top Bottom