CCM yajiandaa kuanza kujipenyeza vyuo vikuu

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,013
Date::11/27/2008
CCM yajiandaa kuanza kujipenyeza vyuo vikuu
Salim Said na Zaina Malongo
Mwananchi

WIKI chache baada ya wimbi la migomo na hatimaye wanafunzi wa vyuo vikuu vya umma kutimuliwa huku wakiahidi kukishughulikia Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye uchaguzi mkuu wa 2010, chama hicho mkoani Dar es Salaam kimesema kinaandaa mkakati wa kujiimarisha kwenye shule za sekondari na vyuo hivyo vya elimu ya juu.

Vyuo saba vya serikali vilifungwa zaidi ya wiki moja iliyopita baada ya wanafunzi kugoma kuingia darasani wakishinikiza kufutwa kwa sera ya uchangiaji elimu inayochambua uwezo wa kiuchumi wa familia ya mwanafunzi katika kupata mikopo, na kutaka wapewe mikopo kwa asilimia 100 kuondoa chembechembe za ubaguzi zinazoonekana kwenye mfumo wa sasa (means testing).

Serikali ilijibu mapigo kwa kutimua wanafunzi wote kwa muda usiojulikana, lakini wasomi hao wakaondoka vyuoni na ahadi nyingi kuwa watakishughulikia chama tawala kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Jana, katibu wa CCM mkoni Dar es salaam, Kilumbe Ng'enda alimwambia mkuu wake, Yusuf Makamba kuwa wameandaa mkakati mkubwa wa kujiimarisha zaidi unaowalenga zaidi vijana ambao ndio nguvu na tegemeo la taifa.

"Ndugu katibu Mkuu tuna mkakati wa kuimarisha chama kwa kuhamasisha katika shule za sekondari na vyuo vikuu mkoani Dar es Salaam," alisema Ng'enda.

Pamoja na sheria namba tano ya uendeshaji vyuo kupiga marufuku shughuli za kisiasa vyuoni, katibu huyo alisema mkakati huo utavuna wanachama wengi, ingawa hakueleza mkakati huo utakwepa vipi sheria hiyo.

Hata hivyo, CCM, ambayo iliongoza mabadiliko ya kisiasa kutoka mfumo wa chama kimoja hadi vingi, imekuwa ikifanya shughuli zake za kisiasa pembeni ya miundo mbinu ya vyuo, ambako hufungua matawi yake ili kuikwepa sheria hiyo.

Kuhusu hali ya chama jijini Dar es salaam, Ng'enda alisema CCM inaendelea vizuri mkoani hapa kwa kuwa kinaendelea kupata wanachama wapya, ambao wengi wao wanatoka vyama vya upinzani.

Alisema wameongeza wanachama wapya 4,600 katika mkoa wote wa Dar es salaam na wanachama 643 wanatoka vyama vya upinzani.

Ng'enda alitaja mkakati mwingine wa kuimarisha chama kuwa ni kushiriki katika uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura na kulalamika kuwa jambo hilo limekuwa likiahirishwa mara kwa mara na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Hata hivyo, Ng'enda alisema hatua hiyo ya tume kuahirisha mara kwa mara uboreshaji huo imewasaidia kujipanga vizuri ikiwa ni pamoja na kuandaa mawakala wao ili kuzuia hujuma.

"Katibu mkuu, uahirishwaji wa mara kwa mara wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura mkoani hapa umetusaidia sana kujiandaa ili kuzuia hujuma kutoka kwa wapinzania wetu," alisema Ng'enda.

Alisema vituo 1255 vitatumika katika uboreshaji wa daftari hilo na CCM mkoani imeandaa mawakala kwa ajili ya kila kituo.

Ng'enda pia alifafanua kuwa mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Anna Abdalla atakuwa pamoja nao katika uhamasishaji wa wanachama kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo ili kuhakikisha kwamba wanatumia haki yao ya kidemokrasia.

Katika ziara hiyo Makamba alipata fursa ya kuzuru hospitali ya wilaya ya Temeke ambako aliwataka waganga na wauguzi kuacha urasimu na kauli chafu kwa wagonjwa ili kuwapunguzia matatizo yao.

"Urasimu katika utoaji huduma unachochea rushwa, na mjue kwamba mgonjwa anaweza kupoa kwa maneno matamu bila ya hata kutumia dawa," alisema Mkamba.

Pia aliwataka viongozi wa CCM kutoka maofisini na kwenda kwa wananchi kuzungumzia mafanikio ya chama na serikali yao.

Naye kaimu mganga mkuu wa hospitali hiyo, Gilbert Bubelwa alimueleza Makamba kuwa wana upungufu wa baadhi ya vifaa muhimu vya kusaidia kuhudumia wagonjwa.

"Mheshimiwa katibu mkuu, mtambo wetu wa kupigia picha za x-ray umechakaa, na ni wa zamani... hatuna mashine ya kufulia nguo, mashine ya kusafishia vifaa vilivyotumika na mashine ya kutayarishia maji kwa ajili ya kutiwa wagonjwa," alisema Bubelwa.
 
Date::11/27/2008
CCM yajiandaa kuanza kujipenyeza vyuo vikuu
Salim Said na Zaina Malongo
Mwananchi

WIKI chache baada ya wimbi la migomo na hatimaye wanafunzi wa vyuo vikuu vya umma kutimuliwa huku wakiahidi kukishughulikia Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye uchaguzi mkuu wa 2010, chama hicho mkoani Dar es Salaam kimesema kinaandaa mkakati wa kujiimarisha kwenye shule za sekondari na vyuo hivyo vya elimu ya juu.

Vyuo saba vya serikali vilifungwa zaidi ya wiki moja iliyopita baada ya wanafunzi kugoma kuingia darasani wakishinikiza kufutwa kwa sera ya uchangiaji elimu inayochambua uwezo wa kiuchumi wa familia ya mwanafunzi katika kupata mikopo, na kutaka wapewe mikopo kwa asilimia 100 kuondoa chembechembe za ubaguzi zinazoonekana kwenye mfumo wa sasa (means testing).

Serikali ilijibu mapigo kwa kutimua wanafunzi wote kwa muda usiojulikana, lakini wasomi hao wakaondoka vyuoni na ahadi nyingi kuwa watakishughulikia chama tawala kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Jana, katibu wa CCM mkoni Dar es salaam, Kilumbe Ng’enda alimwambia mkuu wake, Yusuf Makamba kuwa wameandaa mkakati mkubwa wa kujiimarisha zaidi unaowalenga zaidi vijana ambao ndio nguvu na tegemeo la taifa.

“Ndugu katibu Mkuu tuna mkakati wa kuimarisha chama kwa kuhamasisha katika shule za sekondari na vyuo vikuu mkoani Dar es Salaam,” alisema Ng’enda.

Pamoja na sheria namba tano ya uendeshaji vyuo kupiga marufuku shughuli za kisiasa vyuoni, katibu huyo alisema mkakati huo utavuna wanachama wengi, ingawa hakueleza mkakati huo utakwepa vipi sheria hiyo.

Hata hivyo, CCM, ambayo iliongoza mabadiliko ya kisiasa kutoka mfumo wa chama kimoja hadi vingi, imekuwa ikifanya shughuli zake za kisiasa pembeni ya miundo mbinu ya vyuo, ambako hufungua matawi yake ili kuikwepa sheria hiyo.

Kuhusu hali ya chama jijini Dar es salaam, Ng'enda alisema CCM inaendelea vizuri mkoani hapa kwa kuwa kinaendelea kupata wanachama wapya, ambao wengi wao wanatoka vyama vya upinzani.

Alisema wameongeza wanachama wapya 4,600 katika mkoa wote wa Dar es salaam na wanachama 643 wanatoka vyama vya upinzani.

Ng’enda alitaja mkakati mwingine wa kuimarisha chama kuwa ni kushiriki katika uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura na kulalamika kuwa jambo hilo limekuwa likiahirishwa mara kwa mara na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Hata hivyo, Ng’enda alisema hatua hiyo ya tume kuahirisha mara kwa mara uboreshaji huo imewasaidia kujipanga vizuri ikiwa ni pamoja na kuandaa mawakala wao ili kuzuia hujuma.

“Katibu mkuu, uahirishwaji wa mara kwa mara wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura mkoani hapa umetusaidia sana kujiandaa ili kuzuia hujuma kutoka kwa wapinzania wetu,” alisema Ng’enda.

Alisema vituo 1255 vitatumika katika uboreshaji wa daftari hilo na CCM mkoani imeandaa mawakala kwa ajili ya kila kituo.

Ng’enda pia alifafanua kuwa mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Anna Abdalla atakuwa pamoja nao katika uhamasishaji wa wanachama kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo ili kuhakikisha kwamba wanatumia haki yao ya kidemokrasia.

Katika ziara hiyo Makamba alipata fursa ya kuzuru hospitali ya wilaya ya Temeke ambako aliwataka waganga na wauguzi kuacha urasimu na kauli chafu kwa wagonjwa ili kuwapunguzia matatizo yao.

“Urasimu katika utoaji huduma unachochea rushwa, na mjue kwamba mgonjwa anaweza kupoa kwa maneno matamu bila ya hata kutumia dawa,” alisema Mkamba.

Pia aliwataka viongozi wa CCM kutoka maofisini na kwenda kwa wananchi kuzungumzia mafanikio ya chama na serikali yao.

Naye kaimu mganga mkuu wa hospitali hiyo, Gilbert Bubelwa alimueleza Makamba kuwa wana upungufu wa baadhi ya vifaa muhimu vya kusaidia kuhudumia wagonjwa.

“Mheshimiwa katibu mkuu, mtambo wetu wa kupigia picha za x-ray umechakaa, na ni wa zamani... hatuna mashine ya kufulia nguo, mashine ya kusafishia vifaa vilivyotumika na mashine ya kutayarishia maji kwa ajili ya kutiwa wagonjwa,” alisema Bubelwa.

Kujipenyeza vyuoni kwa vipi?.......... sisi tumeishaichoka na wasijidanye kama hawatupi maslahi kama tunavyoomba hawatupati ng'o!
 
Back
Top Bottom