CCM yaitisha Kamati Kuu kwa dharura

CCM yaitisha Kamati Kuu kwa dharura

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,685
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete ameitisha kikao cha dharura cha Kamati Kuu (CC) kitakachofanyika Kesho mjini Dodoma, huku ajenda kuu ikiwa ni kupitisha majina ya wagombea nafasi ya ujumbe wa Halmashuri Kuu (NEC), zilizo wazi kutokana na sababu mbalimbali, kuanzia ngazi za Wilaya mpaka taifa, na kwamba lazima zijazwe katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu ili kila mtu atimize wajibu wake.

Kwa mujibu wa ratiba ya Chama hicho, Kamati ya Usalama na Maadili itafanya kikao chake Julai 8 na kufuatiwa na Kamati Kuu Julai 9 ambayo inatarajiwa kuchuja wagombea wote waliotangaza nia na kupata watano ambao majina yao yatawasilishwa Halmashuri Kuu ya CCM (NEC) itakayofanyi Julai 10 kuchuja wagombea hao na kubaki watatu watakaopigiwa kura na mkutano mkuu kumpata mmoja. Mkutano huo mkuu utafanyika Julia 11 na 12.

Chanzo: MCL
 
kbm

Sasa jitahidi basi uendelee kuwepo hewani muda wote!
Napenda short and clear phrases kama zako!
Thumb up!😛oa
 
Last edited by a moderator:
kuanzia HEADING mpaka habari yenyewe .......
ipo wazi, haina ushabiki, inaeleweka na si tata.....
tumeukosa sana uandishi wa namna hii.....hongera zako mleta mada
 
Kufuatia kupanda kwa joto la kumsaka mgombea wa Urais wa Tanzania kupitia CCM na songombingo la Zanzibar, Kamati Kuu ya CCM (CC) imeitishwa kwa dharura. Nyaraka za kikao hicho zinaonesha kuwa CC itajadili songombingo la Zanzibar na kuanza kupanga nondo za kuchambua na kuchuja watiania wa CCM. Kikao hicho cha dharura kinatazamiwa kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete na kitafanyika Dodoma.

Kulingana na taarifa nilizonazo,kikao kitafanyika kesho.CC inagusia pia malalamiko ya rushwa toka kwa watiania waliorejesha fomu. Yametolewa malalamiko lukuki yachomayo kama mkuki hasa juu ya wakati wa kusaka wadhamini mikoani. Ni kutoka kwa watia nia wenyewe. Wapo waliowasilisha nyaraka na shahidi nyinginezo kushuhudia rafu za baadhi ya watiania.JF will be the first to know kitakachojiri kikaoni!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Jakaya fanya ufanyavo wa Tanzania hawamtaki Mgombea wako, Rafiki yako, Mwanamtandao wa Zamani na mchezaji mwenzako wa Basket ball, Mjeshi mwenzako mstaafu, mteule wako alieongoza moja ya mihimili ya serikali,Iache Demokrasia ichukue mkondo wake.
 
wana panga majina ya kuwa KATA, mungu jaalia mafisadi wachomolewe !
 
Hiyo CC 'maalum' itakuwa imeitishwa kwa dharura baada ya kuona 'spidi' ya mzee wa mamvi katika safari yake ya matumaini haidhibitiki.

Kwa hiyo wanatafuta 'mwoarobaini' ya namna ya kuli-delete jina lake.
 
Ni matumaini yetu hao wazee wenye ushawishi watakuja na uamuzi wa busara na kuinusuru CCM na taifa kwa ujumla dhidi ya "ubakaji" wa matajiri-haramu. Ni wakati sahihi kupata viongozi wasafi kwa mustakbali wa nchi yetu. Busara za Mwalimu Nyerere zitawaongoza katika hili.
 
Cha ajabu napata taarifa hapa dodoma kama upo nyumba ya wageni na hauhusiki kwenye mkutano unapewa pesa kama ulilipa na kutakiwa kuondoka.
Maana wajumbe na wapambe wa watia nia washalipia guest na hotel zote kwa kipindi cha mkutano.
 
nafikiri pia ratiba haijakaa vizuri,mfano uchaguzi wa wabunge viti maalum ngazi ya mkoa na uchaguzi ww madiwani viti maalum unapishana cku moja!sasa itawezekanaje,wahusika waweze kushiriki kikamilifu? watasafirije kutoka mkoani( kunakofanyika uchaguzi wa wabunge viti maalum) kuwahi the next day kuchagua madiwani viti maalum?! lazima ziongezwe siku hapo kati.ni mawazo yangu tuuuu!
 
kbm

Kutoa leo hadi tarehe hizo July ni mbali kwa hiyo neno dharula halina nafasi . Nilitegemea wasema kikao cha dharula leo asubuhi hii . Waandishi wetu kama TIGO wa Kigoma kwa kweli .
 
Last edited by a moderator:
Kufuatia kupanda kwa joto la kumsaka mgombea wa Urais wa Tanzania kupitia CCM na songombingo la Zanzibar, Kamati Kuu ya CCM (CC) imeitishwa kwa dharura. Nyaraka za kikao hicho zinaonesha kuwa CC itajadili songombingo la Zanzibar na kuanza kupanga nondo za kuchambua na kuchuja watiania wa CCM. Kikao hicho cha dharura kinatazamiwa kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete na kitafanyika Dodoma.

Kulingana na taarifa nilizonazo,kikao kitafanyika kesho.CC inagusia pia malalamiko ya rushwa toka kwa watiania waliorejesha fomu. Yametolewa malalamiko lukuki yachomayo kama mkuki hasa juu ya wakati wa kusaka wadhamini mikoani. Ni kutoka kwa watia nia wenyewe. Wapo waliowasilisha nyaraka na shahidi nyinginezo kushuhudia rafu za baadhi ya watiania.JF will be the first to know kitakachojiri kikaoni!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Mzee Tupatupa usisahau kuwaambia pia hali ya uandikishaji siye walalahoi tunaowapa ulaji si njema na wasidhani wale wawaandikishao kwanza ni lazima wawapigie 'KULA" tunaomba basi kajihaki kadogo tu kakuwapigia "KULA" wanaotakiwa KULA kwa miaka mitano ijayo............:A S-cry::A S-cry::A S-cry::A S-cry:
 
Back
Top Bottom