SautiYaMnyonge
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 439
- 742
Ndugu Shekha Mpemba Fakhi kwa tiketi ya CCM ameibuka mshindi katika uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Konde wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba.
Ikumbukwe Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka kupitia taarifa kwa umma aliyoitoa hapo jana alieleza CCM inauhakika wa ushindi katika jimbo hilo na kata mbili zilizofanya uchaguzi hii leo kwa sababu ya aina ya wagombea iliyowasimamisha, aina ya kampeni walizofanya na mapokeo makubwa yenye hamasa yalioneshwa na wapigakura kwao.
Hili ni Jimbo la tatu (Muhambwe, Buhigwe na Konde) CCM kushinda tangu Sekretarieti mpya ya CCM inayoongozwa na komredi Daniel Chongolo ianze majukumu yake. Kizuri zaidi Jimbo la Konde wanalirejesha kutoka upinzani (mikononi mwa ACT-Wazalendo) lilikodumu kwa miaka 15!
#ChamaImara
#SerikaliImara
#KaziIendelee