CCM yaiangukia CHADEMA; WASSIRA ANYOSHEWA VIDOLE VIWILI

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,794
• WASSIRA ANYOSHEWA VIDOLE VIWILI

na Waandishi wetu, Igunga

logo2.gif
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) katika hali isiyokuwa ya kawaida, jana kiliwatuma viongozi wake watatu kwenda kumwomba radhi Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilibrod Slaa, kutokana na kitendo cha wanachama wake kuwateka nyara na kuwapeleka kusikojulikana vijana watatu wa CHADEMA.
Waliotumwa na CCM kuomba radhi ni wabunge wawili, Januari Makamba (Bumbuli) na Aeshi Hilaly (Sumbawanga Mjini), walioandamana na Mwenyekiti wa Vijana Benno Malisa na Mjumbe wa Baraza Kuu la Vijana Taifa, Hussein Bashe.
Hata hivyo, viongozi hao walikumbana na umati wa vijana wa CHADEMA waliokuwa wakitaka kulipiza kisasi kwa tukio hilo, na kama si busara za Dk Slaa, usalama wa viongozi hao ungekuwa hatarini.
"Waacheni, kwa sababu wamekuja kuomba msamaha, lazima tuwasikilize," alisema Dk Slaa, akiwatuliza vijana hao, ambao hata hivyo walimsihi katibu wao kumwondoa Hilaly kwenye eneo hilo, kwa maelezo kuwa, alitaka kuwaua kwa risasi usiku wa Jumapili iliyopita.
Vijana hao walikubali Makamba na Bashe wabaki wakisema hao ni viongozi waungwana wachache walio ndani ya CCM, na ambao wapo tayari kuwasikiliza.
Akizungumza katika tukio hilo Bashe aliwaomba vijana kuwa watulivu akisema; "Kwanza mimi ni jirani yenu (Nzega), tunataka kampeni ziishe vizuri ili Igunga tuiache salama; tatizo la vijana wenzenu waliokamatwa, tutalimaliza. Tunakwenda kuwatoa," alisema Bashe na kushangiliwa na wafuasi hao wa CHADEMA
Kwa upande wake Aeshi alisema, "lengo la kwenda kwenye hoteli ya CHADEMA ilikuwa kufikia muafaka, lakini kitendo kilichoonyeshwa na baadhi ya vijana wa chama hicho ni utovu wa nidhamu tena mbele ya viongozi wao.
Kikao hicho kilichotumia zaidi ya nusu saa kiliwakutanisha baadhi ya wabunge na makada wenye nafasi za juu ndani ya vyama hivyo kwenye hoteli ya Planet wanakokaa viongozi wa CHADEMA mjini. Pande zote mbili zilikubaliana kuwatuliza vijana wao wakati wote wa kampeni. katika mazungumzo hayo Dk Slaa alikuwa na Susan Lyimo, Kabwe Zitto, Godbless Lema, Tundu Lissu, John Heche.
January Makamba, alisema wamekubaliana kuendelea kuzungumza kila panapotokea kutokuelewana kati ya mashabiki wao na kila upande ujitahidi kuzuia jazba za vijana wao.
Tukio la kutekwa vijana hao wa CHADEMA lilitokea baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uhusiano ya Umma, Stephen Wassira, kuwauliza wananchi waliokuwa katika mkutano wa kampeni wa CCM iwapo kulikuwa na wanachama wa CHADEMA katika mkutano huo.
Wasira alikuwa amewaomba wanachama wa CHADEMA waliokuwapo wanyooshe mikono juu, lakini hakuna aliyefanya hivyo. Baadaye waziri huyo alisema anashukuru kuwa hawapo, na ndipo ziliposikika kelele na miruzi kutoka kila kona ya uwanja huo, huku umati uliokuwa mkutanoni ukinyoosha vidole viwili na kusema ‘peoples...' – ambayo ni kaulimbiu inayotumiwa na CHADEMA.
Walinzi wa CCM hawakufurahishwa na hali hiyo, na ndipo waliwakamata vijana watatu na kuwaingiza kwenye gari lao la ulinzi lenye namba za usajili T 479 ABT Toyota Land cruser Hard Top na kuondoka uwanjani hapo kwa kasi.
Baada ya gari hilo kuondoka, vijana wengi waliondoka mkutanoni hapo na kwenda kufunga barabara iendayo kituo cha mabasi Igunga ili kulizuia gari hilo lililoteka wenzao.
Majira ya saa saba mchana, Naibu Kamishna wa Polisi na Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Makao Makuu ya Upelelezi, Mngulu alisema vijana hao waliokamatwa wamefikishwa kituoni hapo mchana na watu wengine tofauti na waliowakamata.
Yawabembeleza waandishi wa habari
MJUMBE wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana taifa, Hussein Bashe, juzi usiku aliwaita waandishi wa habari waliopo hapa, na kuwaomba wakisaidie chama hicho kuandika habari nzuri zitakazokisaidia kupata ushindi katika uchaguzi.
Bashe ambaye alikutana na waandishi hao kuanzia saa 2:30 hadi saa 5;00 usiku, aliwaambia waandishi hao wa habari kuwa ni vema wakakisaidia chama hicho kutoa sura njema kwa jamii kuliko hivi sasa wanavyoandika na kutangaza habari za kampeni za CCM.
Alisema kuwa haoni sababu ya karibu vyombo vyote vya habari kuandika taarifa zinazoonesha kuwa chama hicho ni kibaya kuliko vyama vingine, na kuwataka kuandika ukweli hata pale CCM inapofanya vema katika mikutano yake.
Hata hivyo, kiongozi huyo wa umoja wa vijana wa CCM, aliomba kikao hicho kisitangazwe popote kwa kuwa alikuwa amekifanya kama rafiki na mwanahabari mwenzao. Bashe ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya New Habari Corporation ya Dar es Salaam
Mbowe aishambulia CCM
MWENYEKITI wa CHAMA cha Demokaria na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema hawatavulimia vitendo vya wizi wa kura au hujuma zozote zitakazofanywa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mbowe amesema kuwa CHADEMA hakitajali cheo cha mtu yeyote atakayejaribu kuibeba CCM ili ipate ushindi katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga.
"CHADEMA ni majasiri, hatuogopi polisi, serikali wala mtu yeyote linapokuja suala la kutafuta haki yetu. Tutamdhibiti Rais, Mkuu wa Mkoa, Polisi na mwingine yoyote yule."
Alisema kama polisi wataamua kuwafungulia mashataka viongozi na wanachama wa CHADEMA watakaokuwa mstari wa mbele kutetea maslahi yao ni vema basi magereza hapa nchini yakaongezwa; "Safari hii hatutaubali kuibiwa kura zetu, yoyote atakayejaribu atakiona, nawatahadharisha wenzetu waache kutuhujumu"
Aliituhumu serikali ya CCM kwa kutumia sh bilioni 10 katika uchaguzi wa Igunga na madiwani zitazofanyika Oktoba 2 mwaka huu.
Mbowe alisema serikali hiyo ni dhaifu na inatumia fedha nyingi katika kuhalalisha ushindi haramu kwenye chaguzi mbalimbali.
Alisema fedha hizo ni nyingi na kama zingetumiwa kwenye masuala ya maendeleo taifa lingeweza kupiga hatua kubwa katika kupambana na umasikini.
Rage apigwa faini
Kamati ya Maadili ya Usimamizi Jimbo la Igunga jana ilimtia hatiani Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini Ismail aden Rage (CCM) na kutakiwa kulipa faini ya shilingi 100,000 kwa kitendo chake cha kupanda jukwaani akiwa na bastola kinyume na maadili ya uchaguzi .
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Msimamizi wa Uchaguzi na Mwenyekiti wa Maadili Jimbo la Igunga Protace Magayane alisema maamuzi hayo yamefikiwa jana katika kikao kilichoketi chini yake na kupita kifungu kwa kifungu nini maadili ya uchaguzi yanasema .
Magayane alisema kwamba kulingana na kanuni za maadili namba 2.2.C "mtu yeyote haruhusiwi kuwa na kupanda jukwaani na silaha yoyote inayoweza kumdhuru mtu katika kampeni na mikusanyiko" alisema.
Magayane alisema iwapo adhabu hiyo isipotekelezwa kwa muda wa siku tatu kuanzia jana atachukuliwa hatua ya kumuondoa Rage kwenye kampeni hizo pamoja na kutoa taarifa kwa kamati ya maadili taifa ambayo ndio yenye mamlaka ya kusimamisha uchuguzi huu wa Jimbo la Igunga.
Chopa za CCM, CUF nazo zatua
Chopa za vyama vya CCM na CUF nazo zimetua jana mjini hapa na kufanya anga la mji wa Igunga kutawaliwa na mingurumo ambayo haikuwahi kuwako tangu kuanza kwa kampeni za ubunge wa jimbo hili.
Helikopta ya CCM ilitua asubuhi wakati ile ya CUF iliwasili jioni. Hata hivyo, CCM iliyokuwa ilete chopa mbili, hadi sasa imeshindwa baada ya kuwepo kwa madai kwamba moja ni mbovu.
Akizungumuza na waandishi wa habari baada ya kutua kwa helikopta hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Julius Mtatiro alisema kuwa, wanatarajia kufanya mikutano 12 kwa siku kwa kwa kutumia usafiri huo.
Alisema kwa siku hizo tatu helikopita hiyo yenye namba za usajili 5Y-BTW itafanya mikutano 36 huku likiongozana na Mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad na Waziri wa Afya wa Serikali hiyo, Juma Haji Duni.
Magufuli atamba
Waziri wa Miundombinu Dk. John Magufuli alitua Igunga jana na kueleza kuwa, atatoa bajeti maalum kwa ajili ya barabara na daraja la Mbutu ambalo limekuwa likilalamikiwa sana na wananchi wa Igunga kwa miaka zaidi ya 10.
Akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni za mgombea ubunge wa CCM jimbo la Igunga Dk Peter Kafumu viwanja vya Sabasaba jana, Dk Magufuli alisema katika mwaka wa fedha wa 2012/2013 Wizara yake itatoa bajeti maalumu ili kuhakikisha barabara za igunga zinatengenezwa na kuwa katika hali nzuri tofauti na ilivyo sasa.
Alisema serikali inayoongozwa na CCM imejitahidi katika upande wa barabara katika Mkoa wa Tabora, na baadhi yake zipo katika matengenezo kwa kiwango cha lami.
"Hawa wenzetu wanashangaza sana, wakati wanasema CCM haijafanya chochote kwa miaka 50, wanatoka Dar es salaam kuja na kupita kwenye barabara hii nzuri ya lami hadi Igunga iliyojengwa na CCM, hawa watu kweli wanasema wanachokiamini?"
"Msiwachague wale ambao katika kupitisha bajeti yeye na wenzake wanatoka, je atajengewaje barabara. Ndugu wana Igunga, achaneni na uongo wa CHADEMA na CUF, leo hii mkichagua CHADEMA, hata wakipata wabunge wengine 10 hawawezi kuitoa CCM madarakani, nawaombeni vyama vyote mpeni kura Dk Kafumu ili akafumue maendeleo ya Igunga," alisema Dk Magufuli na kushangiliwa.
Awali Dk Magufuli aliwaeleza wananchi hao kuwa amekwenda Igunga kama Waziri wa CCM, ambaye ametumwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa wamchague Dk Kafumu kwa sababu ana sifa zote za uongozi.
"Nilisikia kuna mmoja wa wagombea anasema mkimchagua atajenga daraja la Mbutu kwa siku 60, wakati daraja hilo lina kilometa 3, linatakiwa kujengwa tuta kwanza na madaraja mengine matatu, lakini cha kushangaza wakati tunapitisha bajeti hawa wenzetu wa CUF na CHADEMA huwa wanaondoka nje ya Bunge, sasa nawaambia nikitoka hapa nakwenda kukagua daraja la Mbutu," alisema Magufuli.

huna source,unatuletea majungu hapa?
vipi kama source anayo lakini kapitiwa na akasahau kuiweka.. By the way source unayoitaka wewe ni ipi.. Umesoma thread nzima ukilenga kutafuta source sio..kwamba hukuwa na hoja zaidi ya kutaka upewe chanzo..halafu ufanye nini na hiyo source.
Peleka upuuzi wako kwenye Facebook.
 
Bora uchaguzi huu uishe tu, maana mambo hayaendi kisa serikali na watendaji wake wote akili ipo Igunga.
 
• WASSIRA ANYOSHEWA VIDOLE VIWILI

na Waandishi wetu, Igunga

logo2.gif

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) katika hali isiyokuwa ya kawaida, jana kiliwatuma viongozi wake watatu kwenda kumwomba radhi Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilibrod Slaa, kutokana na kitendo cha wanachama wake kuwateka nyara na kuwapeleka kusikojulikana vijana watatu wa CHADEMA.
Waliotumwa na CCM kuomba radhi ni wabunge wawili, Januari Makamba (Bumbuli) na Aeshi Hilaly (Sumbawanga Mjini), walioandamana na Mwenyekiti wa Vijana Benno Malisa na Mjumbe wa Baraza Kuu la Vijana Taifa, Hussein Bashe.
Hata hivyo, viongozi hao walikumbana na umati wa vijana wa CHADEMA waliokuwa wakitaka kulipiza kisasi kwa tukio hilo, na kama si busara za Dk Slaa, usalama wa viongozi hao ungekuwa hatarini.
“Waacheni, kwa sababu wamekuja kuomba msamaha, lazima tuwasikilize,” alisema Dk Slaa, akiwatuliza vijana hao, ambao hata hivyo walimsihi katibu wao kumwondoa Hilaly kwenye eneo hilo, kwa maelezo kuwa, alitaka kuwaua kwa risasi usiku wa Jumapili iliyopita.
Vijana hao walikubali Makamba na Bashe wabaki wakisema hao ni viongozi waungwana wachache walio ndani ya CCM, na ambao wapo tayari kuwasikiliza.
Akizungumza katika tukio hilo Bashe aliwaomba vijana kuwa watulivu akisema; “Kwanza mimi ni jirani yenu (Nzega), tunataka kampeni ziishe vizuri ili Igunga tuiache salama; tatizo la vijana wenzenu waliokamatwa, tutalimaliza. Tunakwenda kuwatoa,” alisema Bashe na kushangiliwa na wafuasi hao wa CHADEMA
Kwa upande wake Aeshi alisema, “lengo la kwenda kwenye hoteli ya CHADEMA ilikuwa kufikia muafaka, lakini kitendo kilichoonyeshwa na baadhi ya vijana wa chama hicho ni utovu wa nidhamu tena mbele ya viongozi wao.
Kikao hicho kilichotumia zaidi ya nusu saa kiliwakutanisha baadhi ya wabunge na makada wenye nafasi za juu ndani ya vyama hivyo kwenye hoteli ya Planet wanakokaa viongozi wa CHADEMA mjini. Pande zote mbili zilikubaliana kuwatuliza vijana wao wakati wote wa kampeni. katika mazungumzo hayo Dk Slaa alikuwa na Susan Lyimo, Kabwe Zitto, Godbless Lema, Tundu Lissu, John Heche.
January Makamba, alisema wamekubaliana kuendelea kuzungumza kila panapotokea kutokuelewana kati ya mashabiki wao na kila upande ujitahidi kuzuia jazba za vijana wao.
Tukio la kutekwa vijana hao wa CHADEMA lilitokea baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uhusiano ya Umma, Stephen Wassira, kuwauliza wananchi waliokuwa katika mkutano wa kampeni wa CCM iwapo kulikuwa na wanachama wa CHADEMA katika mkutano huo.
Wasira alikuwa amewaomba wanachama wa CHADEMA waliokuwapo wanyooshe mikono juu, lakini hakuna aliyefanya hivyo. Baadaye waziri huyo alisema anashukuru kuwa hawapo, na ndipo ziliposikika kelele na miruzi kutoka kila kona ya uwanja huo, huku umati uliokuwa mkutanoni ukinyoosha vidole viwili na kusema ‘peoples...’ – ambayo ni kaulimbiu inayotumiwa na CHADEMA.
Walinzi wa CCM hawakufurahishwa na hali hiyo, na ndipo waliwakamata vijana watatu na kuwaingiza kwenye gari lao la ulinzi lenye namba za usajili T 479 ABT Toyota Land cruser Hard Top na kuondoka uwanjani hapo kwa kasi.
Baada ya gari hilo kuondoka, vijana wengi waliondoka mkutanoni hapo na kwenda kufunga barabara iendayo kituo cha mabasi Igunga ili kulizuia gari hilo lililoteka wenzao.
Majira ya saa saba mchana, Naibu Kamishna wa Polisi na Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Makao Makuu ya Upelelezi, Mngulu alisema vijana hao waliokamatwa wamefikishwa kituoni hapo mchana na watu wengine tofauti na waliowakamata.
Yawabembeleza waandishi wa habari
MJUMBE wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana taifa, Hussein Bashe, juzi usiku aliwaita waandishi wa habari waliopo hapa, na kuwaomba wakisaidie chama hicho kuandika habari nzuri zitakazokisaidia kupata ushindi katika uchaguzi.
Bashe ambaye alikutana na waandishi hao kuanzia saa 2:30 hadi saa 5;00 usiku, aliwaambia waandishi hao wa habari kuwa ni vema wakakisaidia chama hicho kutoa sura njema kwa jamii kuliko hivi sasa wanavyoandika na kutangaza habari za kampeni za CCM.
Alisema kuwa haoni sababu ya karibu vyombo vyote vya habari kuandika taarifa zinazoonesha kuwa chama hicho ni kibaya kuliko vyama vingine, na kuwataka kuandika ukweli hata pale CCM inapofanya vema katika mikutano yake.
Hata hivyo, kiongozi huyo wa umoja wa vijana wa CCM, aliomba kikao hicho kisitangazwe popote kwa kuwa alikuwa amekifanya kama rafiki na mwanahabari mwenzao. Bashe ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya New Habari Corporation ya Dar es Salaam
Mbowe aishambulia CCM
MWENYEKITI wa CHAMA cha Demokaria na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema hawatavulimia vitendo vya wizi wa kura au hujuma zozote zitakazofanywa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mbowe amesema kuwa CHADEMA hakitajali cheo cha mtu yeyote atakayejaribu kuibeba CCM ili ipate ushindi katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga.
“CHADEMA ni majasiri, hatuogopi polisi, serikali wala mtu yeyote linapokuja suala la kutafuta haki yetu. Tutamdhibiti Rais, Mkuu wa Mkoa, Polisi na mwingine yoyote yule."
Alisema kama polisi wataamua kuwafungulia mashataka viongozi na wanachama wa CHADEMA watakaokuwa mstari wa mbele kutetea maslahi yao ni vema basi magereza hapa nchini yakaongezwa; “Safari hii hatutaubali kuibiwa kura zetu, yoyote atakayejaribu atakiona, nawatahadharisha wenzetu waache kutuhujumu”
Aliituhumu serikali ya CCM kwa kutumia sh bilioni 10 katika uchaguzi wa Igunga na madiwani zitazofanyika Oktoba 2 mwaka huu.
Mbowe alisema serikali hiyo ni dhaifu na inatumia fedha nyingi katika kuhalalisha ushindi haramu kwenye chaguzi mbalimbali.
Alisema fedha hizo ni nyingi na kama zingetumiwa kwenye masuala ya maendeleo taifa lingeweza kupiga hatua kubwa katika kupambana na umasikini.
Rage apigwa faini
Kamati ya Maadili ya Usimamizi Jimbo la Igunga jana ilimtia hatiani Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini Ismail aden Rage (CCM) na kutakiwa kulipa faini ya shilingi 100,000 kwa kitendo chake cha kupanda jukwaani akiwa na bastola kinyume na maadili ya uchaguzi .
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Msimamizi wa Uchaguzi na Mwenyekiti wa Maadili Jimbo la Igunga Protace Magayane alisema maamuzi hayo yamefikiwa jana katika kikao kilichoketi chini yake na kupita kifungu kwa kifungu nini maadili ya uchaguzi yanasema .
Magayane alisema kwamba kulingana na kanuni za maadili namba 2.2.C “mtu yeyote haruhusiwi kuwa na kupanda jukwaani na silaha yoyote inayoweza kumdhuru mtu katika kampeni na mikusanyiko” alisema.
Magayane alisema iwapo adhabu hiyo isipotekelezwa kwa muda wa siku tatu kuanzia jana atachukuliwa hatua ya kumuondoa Rage kwenye kampeni hizo pamoja na kutoa taarifa kwa kamati ya maadili taifa ambayo ndio yenye mamlaka ya kusimamisha uchuguzi huu wa Jimbo la Igunga.
Chopa za CCM, CUF nazo zatua
Chopa za vyama vya CCM na CUF nazo zimetua jana mjini hapa na kufanya anga la mji wa Igunga kutawaliwa na mingurumo ambayo haikuwahi kuwako tangu kuanza kwa kampeni za ubunge wa jimbo hili.
Helikopta ya CCM ilitua asubuhi wakati ile ya CUF iliwasili jioni. Hata hivyo, CCM iliyokuwa ilete chopa mbili, hadi sasa imeshindwa baada ya kuwepo kwa madai kwamba moja ni mbovu.
Akizungumuza na waandishi wa habari baada ya kutua kwa helikopta hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Julius Mtatiro alisema kuwa, wanatarajia kufanya mikutano 12 kwa siku kwa kwa kutumia usafiri huo.
Alisema kwa siku hizo tatu helikopita hiyo yenye namba za usajili 5Y-BTW itafanya mikutano 36 huku likiongozana na Mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad na Waziri wa Afya wa Serikali hiyo, Juma Haji Duni.
Magufuli atamba
Waziri wa Miundombinu Dk. John Magufuli alitua Igunga jana na kueleza kuwa, atatoa bajeti maalum kwa ajili ya barabara na daraja la Mbutu ambalo limekuwa likilalamikiwa sana na wananchi wa Igunga kwa miaka zaidi ya 10.
Akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni za mgombea ubunge wa CCM jimbo la Igunga Dk Peter Kafumu viwanja vya Sabasaba jana, Dk Magufuli alisema katika mwaka wa fedha wa 2012/2013 Wizara yake itatoa bajeti maalumu ili kuhakikisha barabara za igunga zinatengenezwa na kuwa katika hali nzuri tofauti na ilivyo sasa.
Alisema serikali inayoongozwa na CCM imejitahidi katika upande wa barabara katika Mkoa wa Tabora, na baadhi yake zipo katika matengenezo kwa kiwango cha lami.
“Hawa wenzetu wanashangaza sana, wakati wanasema CCM haijafanya chochote kwa miaka 50, wanatoka Dar es salaam kuja na kupita kwenye barabara hii nzuri ya lami hadi Igunga iliyojengwa na CCM, hawa watu kweli wanasema wanachokiamini?”
“Msiwachague wale ambao katika kupitisha bajeti yeye na wenzake wanatoka, je atajengewaje barabara. Ndugu wana Igunga, achaneni na uongo wa CHADEMA na CUF, leo hii mkichagua CHADEMA, hata wakipata wabunge wengine 10 hawawezi kuitoa CCM madarakani, nawaombeni vyama vyote mpeni kura Dk Kafumu ili akafumue maendeleo ya Igunga,” alisema Dk Magufuli na kushangiliwa.
Awali Dk Magufuli aliwaeleza wananchi hao kuwa amekwenda Igunga kama Waziri wa CCM, ambaye ametumwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa wamchague Dk Kafumu kwa sababu ana sifa zote za uongozi.
“Nilisikia kuna mmoja wa wagombea anasema mkimchagua atajenga daraja la Mbutu kwa siku 60, wakati daraja hilo lina kilometa 3, linatakiwa kujengwa tuta kwanza na madaraja mengine matatu, lakini cha kushangaza wakati tunapitisha bajeti hawa wenzetu wa CUF na CHADEMA huwa wanaondoka nje ya Bunge, sasa nawaambia nikitoka hapa nakwenda kukagua daraja la Mbutu,” alisema Magufuli.Watu wengine bana huwa wanakurupuka tu sijui huwa wametoka wapi, hii habari jana ililetwa jana humu JF na watu waliichangia , mtu anatoka kwenye chang'aa anaileta tena
 
Hivi CCM wamekosa watu wa kusaidia kampeni hadi aende wassira, sote tunajua mtu anaesinzia hovyo tena mchana, akikurupuka usingizini anaweza kuropoka "ZIMA TAA" wakati ni mchana kweupe, siasa za wassira za utayson zilifaa 1995, enzi za watanzania mbumbumbu,leo hazifai ndo maana mzee huyu anaambulia aibu kila kona
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom