CCM yahonga maaskofu Arumeru

Technician

JF-Expert Member
Mar 30, 2010
841
222
Na Mwanadishi Wetu,Arumeru

Katika kampeni za uchaguzi wa mdogo jimboni Arumeru Mashariki,
imebainika kuwa tabia ya chama cha mapinduzi (CCM) YA KUUZA
NA KUNUNUA UONGOZI ,imevuka mipaka.
Safari hii imeingia mahala patakatifu pa watakatifu.

"Ofisa huyo anadaiwa kutoa Sh 20,000 kwa kila mchungaji aliyekuwa
kwenye huo mkutano"

"Aidha,viongozi saba na wachungaji hao walilipwa kiasi cha Sh 100,000
kila mmoja kama Nauli katika mkutano ambao haukuandaliwa na CCM"

source:Gazeti MWANAHALISI
 
Kumbe maaskofu nao huwa wanakula rushwa???? Sasa huwa wanawafundisha nini huko makanisani???????
 
Kumbe source ni Said Kubenea? tuletee source zisizo na mrengo, wengine humu JF hatuna vyama.
 
Ukiona source ni Said Kubenea ujue uongo mtupu, Si juzi tu hapa Mkuu wa Maaskofu amemshambulia Wasira pale SLAA alipogushwa kidogo tu? inawezekana kweli hata mwezi bado, kondoo wake waingie mtegoni? Kubenea jamani hata kama ni mzuri wa kupiga majungu si usome alama za nyakati kwanza? au tindikali imepunguza uwezo wa kutafakari kabla ya kuamua kutenda?
 
Habari iliyoletwa na chanzo cha habari haiusiani na ushabiki wa vyama ila ni uhalisia wa tukio lililotokea wakati huo.
Sasa kama wewe unamchukia Kubenea hiyo ni shauri jingine, ni kweli kikao hicho cha watumishi wa Mungu kilivamiwa na Mungulu na habari ikaletwa humu JF huenda hukubahatika kuisoma, inasemekana alitoa 2m kama wewe una taarifa tofauti utwambie walipewa kiasi gani cha pesa na huyo Mungulu alienda pale kupata sakramenti ya kitubio kwa yale ya Igunga au ameishamchukulia mtu hapo Arumeru mashariki?.

Kweli ni rahisi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano lakini si kwa Maaskofu wa Arumeru kuona ufalme wa mbingu Askofu mwenye kola aliyeenda shule vya kutosha na kula viapo vya kila aina leo anakuwa bwabwa la CCM kuhongwa jumla ya shillingi 20,000 ambayo hata suruali ya maana hata pata
Maaskofu Arumeru acheni hizo munajidhalilisha,tuwaulize munafuata nini kwenye mikutano inayoandaliwa na CCM au hata na wapenzi wa CCM ili kufanya dhuluma,ole wenu mukidhurumu haki nyie
 
hii habari nimeisoma ila kwa kweli imekaa kiumbea zaidi kwanza amechanganya walutheri na wapentekoste, wapentekoste ndio waliopokea hizo laki lakini walutheri na askofu wao hawakupokea chochote na huyu mtu wanasema alienda pale akajitambulisha kama mlutheri na alienda na bahasha kama kukarimu mkutano, kwa nini hii habari ina mapungufu au ni ya kutunga moja kama alienda na fedha na kumkuta askofu mwenyewe pia iweje awe na zawadi ya kalenda kwa ajili ya watumishi wakati hizi zingekuwa zipo hapo dayosisi na ni free kwa sharika zake?haionyeshi kama amepokea bali alimsikiliza tuu huyo muumini wake kisha huyo muumini wake akaenda kwenye kikao kipi?mazingira ya askofu kwa kweli hayaeleweki?na je askofu ni Mungu ajue hii ni rushwa kutokana na huo utambulisho wa huyo mtu, waumini wengi hasa wenye pesa huwa wanatabia ya kuchangia huduma mbalimbali je askofu huyu na wenziwe walitakiwa kuota,

hii stori haijpangwa na inajichanganya sana kama vipi waedit walete vizuri wiki ijayo la sivyo nashauri kanisa liwashitaki kwa kumchafulia jina kiongozi wao? huu ni mtizamo wangu tu. embu wengine mliosoma mseme, ila kwa kweli hili gazeti liangalie kumsema mpakwa mafuta wa Mungu kuna adhari zake. na nashauri kama mtu hujasoma hii stori usichangie kabisa. soma then changia usijechukua laana ya bure bila kujua.
 
Kweli ni rahisi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano lakini si kwa Maaskofu wa Arumeru kuona ufalme wa mbingu Askofu mwenye kola aliyeenda shule vya kutosha na kula viapo vya kila aina leo anakuwa bwabwa la CCM kuhongwa jumla ya shillingi 20,000 ambayo hata suruali ya maana hata pata
Maaskofu Arumeru acheni hizo munajidhalilisha,tuwaulize munafuata nini kwenye mikutano inayoandaliwa na CCM au hata na wapenzi wa CCM ili kufanya dhuluma,ole wenu mukidhurumu haki nyie

usiwe mwepesi kuchangia kama hujasoma habari vizuri wala huna enough data!kwani arumeru kuna maaskofu wangapi?waliotajwa ni wangapi?sometimes pita tu kwenye hizi thread especially zinazohusu watumishi wa Mungu.
 
Ni nalo Gazeti hapa nimesoma taarifa ila natahadharisha huyo askofu na wengine walioko arumeru wa kilutheri kama yuko mmoja vizuri kama wako wengi tunawaasa watende haki wasimamie haki wakemee vitendo vyote vya rushwa ,wasijidhalilishe kwa kubeba chama cha magamba,waache dhambi ya tamaa kwa kupokea sh 20,000 hadhi yao ya kichungaji ni kubwa kuliko wao kujiingiza katika chaguzi
 
Waliitwa Getaway Lodge ilioko Leganga kwa juu kama unaenda Jua Kali.
Walipewa soda na elfu ishirini shirini.

Wakaambiwa wakahubiri Chagua CCM na kuwa Chadema ni mbaya na ndio maana Bendera yao ina rangi nyekundu
 
Ukiona source ni Said Kubenea ujue uongo mtupu, Si juzi tu hapa Mkuu wa Maaskofu amemshambulia Wasira pale SLAA alipogushwa kidogo tu? inawezekana kweli hata mwezi bado, kondoo wake waingie mtegoni? Kubenea jamani hata kama ni mzuri wa kupiga majungu si usome alama za nyakati kwanza? au tindikali imepunguza uwezo wa kutafakari kabla ya kuamua kutenda?
Na tuhuna zote za ufisadi zilizokuwa zikiandikwa na hili gazeti ni za uongo basi! Otherwise mna double standards!
 
Rejao
kuna watu humu Jf NI VIGEUGEU wao kama wanataka habari zilizodhibitishwa kwanini wao wasiwe waandishi ili iwe rahisi kujiridhisha kwa kila jambo walitakalo
na isitoshe Kubenea hayupo pale kumridhisha kila mtu kwani Tanzania ian watu zaidi 40 mil na wajumbe wa Jf ni katone ktk idadi hiyo,kama mjumbe wa JF haamini chanzo watanzania 40mil watakiamini tu
 
Ukiona source ni Said Kubenea ujue uongo mtupu, Si juzi tu hapa Mkuu wa Maaskofu amemshambulia Wasira pale SLAA alipogushwa kidogo tu? inawezekana kweli hata mwezi bado, kondoo wake waingie mtegoni? Kubenea jamani hata kama ni mzuri wa kupiga majungu si usome alama za nyakati kwanza? au tindikali imepunguza uwezo wa kutafakari kabla ya kuamua kutenda?

wewe ulitaka chanzo kitoke wapi?

kama vipi tafuta chanzo chako unachokiamni na usitulazimishe tuamini kile wewe uaminicho

kwani akili ni nywele kila mtu ana zake so unacho kiamini wewe si lazima tukifuate,ama ninachokiamini mimi si lazima ukifuate
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom