Makanisa yakwepa siasa za Arumeru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makanisa yakwepa siasa za Arumeru

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by MziziMkavu, Mar 27, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  MAKANISA yenye idadi kubwa ya waumini katika Jimbo la Arumeru Mashariki, yanaonekana kukwepa kujiingiza kwenye mtego wa kushabikia vyama vya siasa katika kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo unaoendelea.

  Katika ibada za jana Jumapili, viongozi wengi wa madhehebu ya kikristo walisikika wakihubiri amani lakini wakaepuka kushawishi waumini wao kushabikia chama chochote cha siasa.

  Badala yake wengi wao waliwahimiza waumini wao kushiriki kampeni za vyama na kuwasikiliza wagombea wa vyama vyote, kisha Jumapili ijayo wajitokeze kwa wingi kumpigia kura mgombea wanayemtaka.

  Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mlima Meru, Paul Akyoo aliliambia gazeti hili kuwa: “Sisi tunawahimiza waumini wetu kushiriki kampeni kwa amani na kwa kuheshimiana, hatuungi mkono chama chochote wala mgombea yeyote kwasababu kanisa halina itikadi ya kisiasa, ila waumini wake wanaweza kuwa wanasiasa”.

  Askofu Akyoo aliongeza: “Kanisa haliingilii kampeni, nafasi yetu inaishia tu kuwaasa wana Arumeru wote kufanya kazi hii ya uchaguzi kwa amani na utulivu, ili hatimaye wapate kiongozi, mbunge wanayemtaka.”

  Mapema katika Ibada ya Jumapili iliyofanyika Kanisa Kuu la Kilutheri la Usa River, Askofu Akyoo aligusia kuwapo kwa taarifa kwamba baadhi ya vyama vya siasa vingeleta fujo kwenye uchaguzi, lakini alisita kuendelea na taarifa hiyo baada ya waumini wa kanisa hilo kuguna.

  Katika Kanisa Katoliki la Usa River, paroko aliyekuwa akiongoza misa jana ambaye hata hivyo jina lake halikufahamika mara moja, aliwaambia waumini wake kuwa: “Msisahau kwamba Jumapili ni siku ya kupiga kura kumchagua mbunge wetu, kwa hiyo hakikisha kwamba unakwenda kupiga kura na ukimaliza rudi utulie nyumbani au endelea na shughuli zako zingine”.

  Jumapili ijayo Aprili mosi, ndiyo siku iliyopangwa kufanyika uchaguzi huo na kwa mujibu wa kalenda ya kanisa ni siku ya matawi ya mitende ambapo wakristo wanakumbuka jinsi Yesu Kristo alivyoingia Yerusalemu kwa shangwe kabla ya kukamatwa, kuteshwa na kuuwawa.

  Katika makanisa ya Kipentekoste na yale ya Kanisa la International Evangalism (IEC) linaloongozwa na Askofu Mkuu, Eliud Isangya, viongozi wa ibada pia walikwepa kuzungumzia uchaguzi kwa maana ya kuegemea upande wowote, badala yake walihimiza amani na utulivu wakati wa kampeni na upigaji kura.

  Dini na siasa
  Wakati madhehebu ya dini yakionekana kukwepa kuingia moja kwa moja kwenye mtego wa siasa, kumekuwapo na taarifa kwamba baadhi ya vyama vya siasa vimekuwa vikisaka kuungwa mkono na taasisi hizo za kidini.

  Miongoni mwa taarifa hizo ni ile inayomuhusu mmoja wa makada wakongwe wa CCM (jina tunalihifadhi kwa sasa) ambaye juzi kati ya saa 3.30 na 4.15 asubuhi alikuwa ofisini kwa Askofu Akyoo akiomba kanisa hilo kumuunga mkono.

  Habari zinasema katika kikao hicho cha dakika kama 45 hivi, Askofu huyo aliweka bayana kwamba kanisa hilo haliwezi kuingia moja kwa moja kwenye siasa kwani waumini wake ni wanachama wa vyama tofauti.

  Hata hivyo Askofu Akyoo alipoulizwa jana kuhusu ugeni wake huo, hakukubali wala kukanusha, badala yake alisema: “Jamani hapa kanisani watu wengi wanafika kwa masuala hasa ya kiroho, hivyo ni vigumu wakati mwingine kujua nani anakuja kwa ajili ya kazi gani”.

  Wiki iliyopita gazeti hili lilipata taarifa kwamba kulikuwa na kikao kati ya viongozi wa CCM na wachungaji wa madhehebu ya Kipentekoste takriban 170, ulioandaliwa na chama hicho katika Hoteli ya Gateway wakiwataka wawashawishi waumini wao kumchagua mgombea wa CCM, Sioi Sumari.

  Mbunge wa Nkenge (CCM), Mchungaji Asumpta Mshama anadaiwa kwamba ameletwa kwenye kampeni kwa ajili hiyo ikizingatiwa kuwa Arumeru Mashariki kuna waumini wengi wa dini ya kikristo.

  Akizungumzia suala hilo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa alisema viongozi wa dini zote waepushe madhabahu ya makanisa yao kutumiwa kisiasa hata kama wana malengo ya kupata fedha.

  Kwa upande wao CCM, wamekuwa wakiwatuhumu Chadema kwamba ndiyo wanaoingia makanisani kuomba kura na kwamba chama hicho cha upinzani kimemteua Mbunge wake wa Karatu, Mchungaji Israel Natse kuwa Meneja Kampeni mwenza ili kufanikisha mpango huo.

  Kabla ya kuchaguliwa kuwa mbunge kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, 2010, Natse alikuwa kiongozi wa KKKT Jimbo la Karatu. Kwenye uchaguzi wa Arumeru Mashariki anaongoza kampeni za Chadema kwa kushirikiana na Mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere.

  Kishindo cha Mbowe

  Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe jana alianza kwa kishindo kampeni za kumnadi mgombea ubunge wa chama hicho jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari kwa kuwaomba wapiga kura wa jimbo hilo kumwongezea mbunge wa 49 ili kukipa Chadema nguvu ya kuhoji Serikali kuhusu matumizi na usimamizi mbaya wa rasilimali za taifa.

  Akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Samaria, Kata ya Maroroni jana, Mbowe alisema ugomvi na vita kati ya Chadema na CCM hautokani na uadui bali ni tofauti kiimani na kiitikadi katika usimamizi na matumizi ya mali na rasilimali za nchi.

  “CCM ndiyo iliyopewa ridhaa ya kuongoza na kusimamia rasilimali za taifa letu, lakini imeonyesha kushindwa kutekeleza wajibu huo ndiyo maana licha ya utajiri mkubwa tuliojaliwa na Mwenyezi Mungu, tumeendelea kuwa masikini wa kutupwa.

  Huu ndio ugomvi wetu na tunawaomba wananchi wa Arumeru mtuongezee nguvu kwa kumchagua Nassari,” alisema Mbowe.

  Alisema licha ya uchache wao bungeni, watatumia dhamana waliyopewa na wananchi kupigania mabadiliko katika katiba mpya ikiwemo uhuru wa watu kujiunga na chama chochote cha siasa bila kuhofia kusulubishwa na chama tawala kama hali ilivyo sasa ambapo wafanyabiashara wanaounga mkono upinza baadhi yao hufilisiwa kwa kutumia hila mbalimbali.

  Kuhusu ardhi, alisema rasilimali hiyo lazima inufaishe Watanzania badala ya hali ilivyo sasa ambapo ardhi yote yenye rutuba na inayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji hugawanywa kwa wageni kwa kivuli cha uwekezaji huku wananchi, wakiwemo wa Arumeru, wakikosa hata sehemu ya kuzikia ndugu zao.

  CCM wanasa waraka
  Kwa upande wake CCM wamedai kwamba wamenasa waraka wa siri kutoka Chadema ambao unaeonyesha kuwa chama hicho kimekubali kushindwa katika uchaguzi huo.

  Waraka huo wa ndani unaodaiwa kuandikwa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Slaa, umeelekezwa kwenda kwa timu ya kampeni ya chama hicho katika uchaguzi wa Arumeru Mashariki.

  Meneja Kampeni wa CCM, Mwigulu Nchemba alisema waraka huo ulionesha kuwa Chadema kinajutia vitendo vyake kwenye kampeni hivyo kinakiri kwamba kitashindwa.

  Alisema kuwa Dk Slaa katika waraka huo, anaonesha kulalamikia timu ya kampeni hizo ya chama chake kwa kitendo cha kumkashifu Rais Mstaafu, Benjamini Mkapa katika mikutano yake.

  Pia alidai kwamba vitendo vya kufanya vurugu, kuwapiga wanahabari, kuchana bendera na hata kutishia watu ambavyo vimekuwa vikifanywa na wafuasi wa Chadema vinalalamikiwa kwenye waraka huo.

  Nchemba alisema Dkt Slaa aliwaeleza viongozi walioko katika timu hiyo kwamba kufuatia vitendo hivyo, vikiwemo vya kupiga yowe kinyume na mila za Kimeru, uwezekano wa Chadema kushindwa ni mkubwa.

  "Tumenasa waraka wa ndani wa Chadema, unaonesha wanavyojutia matendo yao waliyotenda katika hizi kampeni, na Dk Slaa anahofia sana ushindi wao,"alisema Nchemba

  Aliongeza kuwa katika waraka huo, Dk Slaa aliishangaa timu ya kampeni ya chama hicho kwa kuwa katika vikao vya awali walikwishakubaliana kuwa wasifanye kampeni za vurugu kama wanazofanya sasa.

  "Kuna kipengele kimoja kimeeleza kuwa walikuwa wamekubaliana kufanya kampeni bila ya vurugu, lakini matendo yote waliyofanya yamekuwa kinyume na kwamba Dk Slaa eti anawashangaa kuwa wamekiuka makubaliano ya amani,"alisema Nchemba.

  Alisema Dk Slaa amekiri kuwa watu wa Arumeru hawawakubali tena na kwamba kwa sasa wana mpango wa kuingiza kundi la watu kutoka sehemu mbalimbali ili wafanye fujo ambazo zitaishinikiza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwatangaza washindi hata kama watakuwa wameshindwa.

  "Wanampango wakuingiza watu wao watakaofanya vurugu hapa wakati wa kutangazwa kwa matokeo, ili kuishinikiza Tume, kwasababu wanajua kabisa kuwa wanaArumeru wamekasirishwa na vitendo vyao vya kufanya vurugu"alisema Nchemba.

  Meneja mwenza wa kampeni za Chadema, Nyerere alipuuzia madai hayo na kusema kwamba wao Chadema wanajiamini watanyakua Jimbo la Arumeru Mashariki na kuwataka CCM kutoishi kwa mashaka.

  "Si kweli na tutashinda ushindi wa mapema na usio na mashaka, CCM wasubiri vipimo"alisema Nyerere

  Imeandaliwa na Neville Meena, Mussa Juma, Peter Saramba na Moses Mashalla
  Makanisa yakwepa siasa za Arumeru
   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Makanisa ni home of intellectuals sio kama vilaza wala tende.
   
 3. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2012
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CCM wameishiwa wamebaki na mabarua ya siri we Mwigulu mbunge mzima tunaekutegemea Iramba magharibi unabaki kudanganya wanaarumeru.
   
 4. T

  TORABORA Member

  #4
  Mar 27, 2012
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Idiot. Wacha matusi ya rejareja.
   
 5. CHEMPO

  CHEMPO JF-Expert Member

  #5
  Mar 27, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Shule ni msaada sana kwa viongoz wa dini,,,,,,
   
 6. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #6
  Mar 27, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hawawezi kukwepa wak majuzi mwigulu aliingia kwenye kikao alicho alikwa na lotti ambaye ni mwenyekiti wa ccm maji ya chai na ni kaimu katibu dayosisi ya meru kagawa kalenda zami za chakula hilo lipo wazi
   
 7. Kiwewe

  Kiwewe Senior Member

  #7
  Mar 27, 2012
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kama Askofu Akyoo amekataa kutumia kanisa kisiasa, basi wawafuate wale viongozi wa dini flani kule Igunga waliotumika kushawishi waumini wake wachague CCM na wasichague upinzani.
   
 8. odinyo

  odinyo JF-Expert Member

  #8
  Mar 27, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  ni gazeti.msg fupi ni nzuri
   
Loading...