KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Katibu wa uchumi na fedha Mwigulu Nchemba wameongoza maandamano leo kutoka ofisi ya CCM wilaya ya Mpanda kwenda kwenye Uwanja wa Shaulili ambapo wamefanya mkutano mkubwa wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu ya watu. Hakika wana Mpanda wameikubali sana CCM.