CCM yafanya umafia kumzima Dr Slaa Mbeya

CCM yafanya umafia kumzima Dr Slaa Mbeya

Katika hali isiyotarajiwa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani hapa juzi, ilibuni mbinu za kuzuia kutangazwa kwa mkutano wa Dk. Slaa baada ya kuitisha kikao na waandishi wa habari wa vyombo vyote katika muda ambao katibu huyo wa CHADEMA alikuwa akihutubia.
Habari za uhakika kutoka ndani ya CCM, zilisema kuwa ingawa ilidaiwa kuwa mkutano huo na waandishi wa habari ulikuwa na lengo la kumtambulisha katibu mpya wa chama hicho wilaya ya Mbeya mjini ambaye amefika baada ya yule wa awali kuhamishwa, lakini nia kubwa ilikuwa kuukwamisha mkutano wa Dk. Slaa.
Habari zinadai kuwa CCM iliwaambia waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo kuwa walitaka pia kuzungumzia masuala yahusuyo mchakato wa uundwaji wa Katiba mpya ambapo wamelenga kutuma makada wa chama hicho kuelimisha umma juu ya jambo hilo.
Katibu mpya wa CCM wilaya, Raimond Mwangwale, alisema uelimishaji huo utafanyika siku tatu mfululizo kuanzia Januari 12, katika kata 36 za jimbo la Mbeya mjini.
Mmoja wa makada maarufu wa CCM alilithibitishia Tanzania Daima ukweli wa mkutano huo na waandishi, ingawa alikiri kuwa mbinu yao haikufanikiwa sana. Alikiri kuwa hotuba za Dk. Slaa zimekuwa na madhara makubwa kwa CCM na imekuwa ni vigumu zaidi kuzifuta katika akili za wananchi ambao wameonyesha kuamini kila akisemacho

SOURCE:TANZANIA DAIMA

Chadema malalamiko mengine yanaonekana wazi hayajaenda shule.

Hata mzee wa miaka 100 tena anayetoka sweken kabisa kule Kipili au kilando au hata lyamba lya mfipa huwezi mwambia uwongo kama huu.

Je waandishi hao wamezuiliwa kivipi? Je hilo si jukumu la mwandishi kuamua anakwenda wapi na kupima umuhimu wa habari kwa jamii.

Naona sasa mmefilisika na kuanza kulalama kila jambo.

Uongozi wa chadema mbeya umesambaratika,kutokana na mambo mbalimbali ya kijamii na kiuchumi yanayojitokeza kila kukicha.viongozi hao wameiona chadema kuwa ni chama kisicho na mwelekeo zaidi ya kuhamasisha vurugu na maandamano yasiyo na tija.

Sio kosa lako NI WIVU TU UMEKUGANDA... Futa ndoto hizoo. Mtu makini yuko ktk jamii ya walio makini..Tunajua mko wengi MNAIKUBALI (CDM)KIMYAKIMYA.
 
Chadema malalamiko mengine yanaonekana wazi hayajaenda shule.

Hata mzee wa miaka 100 tena anayetoka sweken kabisa kule Kipili au kilando au hata lyamba lya mfipa huwezi mwambia uwongo kama huu.

Je waandishi hao wamezuiliwa kivipi? Je hilo si jukumu la mwandishi kuamua anakwenda wapi na kupima umuhimu wa habari kwa jamii.

Naona sasa mmefilisika na kuanza kulalama kila jambo.

Mara moja moja uwe unachanganya na zako, sio kila kitu utatafuniwa.

Bahasha shehe, unadhani ccm inaweza kuwaita waandishi wa habari hivi hivi bila kuto bahasha!?
 
Uongozi wa chadema mbeya umesambaratika,kutokana na mambo mbalimbali ya kijamii na kiuchumi yanayojitokeza kila kukicha.viongozi hao wameiona chadema kuwa ni chama kisicho na mwelekeo zaidi ya kuhamasisha vurugu na maandamano yasiyo na tija.

Maono yako na hao baadhi ya unaowaita viongozi ni sawa!ila kwa mtazamo chanya hao hawakua na nia ya dhati kutumikia chama,ndio maana imekua rahisi wao kurubuniwa na vijisenti!ni nzuri kuwajua mamluki kama hao mapema
 
Kwa sababu nyinyi wanawake mnamuita handsome lazima utafanya hivyo tu
Mimi ni mara kumi kuangalia katuni ya tom and jerry kwenye tv yangu lakini si huyu mtu wenu jk

Watake radhi wanawake mkuu,sio wote wenye mtazamo huo,ni baadhi tu tena wenye low iq
 
Kama kuna channel 2 kwenye TV,moja Dr Kikwete na moja Dr Slaa. Ntamwangalia Dr Slaa!

Umeenda mbali sana...kama kuna channel 'A" inaonyesha hotuba ya jamaa jk na nyingine "B" inaonyesha maigizo ya kina kanumba nitatune channel B ni burudike kuliko kuangaliz mtu anachekacheka tu wakati nchi iko ICU
 
Ni mteule wa MUNGU, Tanzania-Africa, kusini mwa jangwa sahara. tupme kura za ndio

ACHENI KUCHAKACHUA NENO CHAGUO LA MUNGU!
2005 MLITUAMBIA JK NI CHAGUO LA MUNGU, 2010 MKABADILISHA NA KUDAI SLAA NDIO CHAGUO LA MBINGUNI LAKINI AKAKATALIWA ARDHINI!
2011! MKAJA NA DAI LA BABU WA LOLIONDO NAE NI CHAGUO LA MUNGU! WATU WAMEPOTEZA MAISHA KWA MAMIA BAADA YA KUNYWA KIKOMBE CHENYE MAONO YA MBINGUNI!

SASA MNAANZA TENA NA KAULI ZENU ZA CHAGUO LA MUNGU KWA SASA NI SLAA! JAMANI TUMECHOKA NA UCHAKACHUAJI WA NENO CHAGUO LA MUNGU!

TUACHENI WANANCHI TUCHAGUE VIONGOZI HAPA ARDHINI HAO WA KUCHAGULIWA TOKA MBINGUNI WAKATI WAO UMEPITA! WAO WALIKUWA AKINA MUSA, DAUDI, YESU NA MUHAMAD! SASA WANANCHI NDIO WATACHAGUA KIONGOZI LAKINI SIO WAKUCHAGULIWA NA MAASKOFU, MAKASISI, WACHUNGAJI AU MASHEHE NA MAIMAMU!!!

:lol:
 
Chadema malalamiko mengine yanaonekana wazi hayajaenda shule.

Hata mzee wa miaka 100 tena anayetoka sweken kabisa kule Kipili au kilando au hata lyamba lya mfipa huwezi mwambia uwongo kama huu.

Je waandishi hao wamezuiliwa kivipi? Je hilo si jukumu la mwandishi kuamua anakwenda wapi na kupima umuhimu wa habari kwa jamii.

Naona sasa mmefilisika na kuanza kulalama kila jambo.

unalipwa bei gani na hao waliokutuma?
 
Mimi sijaona umafia wowote hapo ccm kivyao na chadema kivyao.Haya magazeti nayo.
 
Uongozi wa chadema mbeya umesambaratika,kutokana na mambo mbalimbali ya kijamii na kiuchumi yanayojitokeza kila kukicha.viongozi hao wameiona chadema kuwa ni chama kisicho na mwelekeo zaidi ya kuhamasisha vurugu na maandamano yasiyo na tija.

Nadhan wewe ni mmoja kati ya wana ccm wewe furahia ccm wakkat ndugu zako wanaanza kuumia subiri uone huo umeme kama utaweza kuulipa ukiambia hali ya maisha ni ngumu unalalamika nini wakat serikal yako inashindwa kumage hali ya uchum?
 
kwani waandishi wote ni wa serikali? Kwani ni kazima waende waandishi wote?
 
Back
Top Bottom