CCM yaendelea na ''Copy and Paste'' toka CHADEMA, Sasa Wachukua Sera ya Majimbo!

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,567
1,250
Katika muendelezo wa ccm kutumia sera makini za Chadema, Waziri wa nishati na madini Prof. Muhongo ameeleza kuwa serikali imeanza kutoa mafunzo maalum ya gesi na mafuta kwa vijana wa mikoa ya Lindi na Mtwara ili wananchi wa mikoa hiyo wafaidike na utajiri wa maliasili hiyo iliyopo katika mikoa hiyo.
Pia ameeleza kuwa vijana toka mikoa hiyo wamepata upendeleo maalum wa kusoma chuo cha madini Dodoma, chuo kikuu Dodoma (UDOM) na vyuo vya nje ya nchi katika kozi zinazohusika na mambo ya gesi na mafuta.
Source: BBC Dira ya dunia saa 12:30 Jioni.

MY TAKE:
Kwa mwenendo huu ni dhahiri ccm imeanza kutekeleza sera ya majimbo ya Chadema ambayo wamekuwa wakiipinga kwa muda mrefu.
 
Top Bottom