Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 50,955
- 22,131
Kesi ya Mbunge: Shahidi 'daktari' akiri hakumaliza kidato cha nne
Na Mussa Juma,Arusha
Shahidi wa tisa Flora John Mzava(48) katika kesi inayomkabili mbunge wa jimbo la Simanjiro mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka jana alipata wakati mgumu mahakamani kuhusiana na elimu yake baada ya kukiri hajawahi kusajiliwa na Baraza la madaktari nchini.
Â
Shahidi huyo ndiye alimfanyia uchunguzi, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Arusha, James Millya mara baada ya kudaiwa kupigwa kibao na Sendeka hata hivyo alikiri aliishia darasa la saba.
Â
Katika kesi hiyo  Sendeka anatuhumiwa kwa makosa mawili ya kumpiga kibao na kumtishia na bastola , Millya, Januari 9 mjini Monduli.
Â
Mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya mkoa wa
Arusha James Karayemaha, Shahidi huyo  alisema alipokuwa akifamfanyia uchunguzi Millya, alimkuta ana uvimbe usoni na ana maumivu ya kiuno.
Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano kati ya mwanasheria wa serikali Michael Luena  na shahidi huyo.
Â
Luena: Hebu chukua kielelezo namba P1 Je,unaitambua
Shahidi: Naitambua kuwa ni PF3 kwani ina mwandiko wangu na saini yangu
Luena: Nani alimfanyia uchunguzi Millya/
Shahidi: Mimi
Akiwahojiwa na wakili wa utetezi, Mpaya Kamara ,Shahidi huyo alikiri kuwa   hajasajiliwa na Baraza la madaktari(Tangayika Medical Council) kama sheria ivyosema kwa kuwa yeye ni daktari wa vidonda.
Â
Kamala: Hebu eleza elimu yako ya msingi ulisoma wapi?
Shahidi: Nilisoma katika shule ya msingi Enduleni iliyopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha
Kamala: Ulimaliza mwaka gani?
Shahidi:Â Mwaka 1976
Kamala: Ulichaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari?
Shahidi: Ndio katika shule ya sekondari Karatu lakini niliishia kidatu cha pili mwaka 1978 kutokana na ugonjwa
Kamala: Kwa hiyo hukumaliza kidatu cha nne
Shahidi : Ndio
Kamala: Hebu angalia PF3 ilipaswa na kujazwa na nani sio medical Officer?
Shahidi: Ndio
Kamala: Wewe umesaini kama nani? Au uliandikiwa barua yoyote ya kukurusu kusaini badala ya mganga mkuu wa wilaya/
Shahidi : Sina
Kamala: Wewe ni daktari
Shahidi : hapana
Kamala Awali ulisema kuwa wewe unaweza kuhudumia magonjwa yote hata
upasuaji je ulifanya operesheni ngapi
Shahidi: siwezi ila nafunga vidonda na kupasua majipu
Kamala kama wewe sio daktari ulithibitisha vipi James Ole Millya alipata majeraha
Shahidi: Baada ya kumpokea na kumfanyia uchunguzi
Kamala :Uligundua nini?
Shahidi: Amepigwa na kitu chenye ncha kali shavu la kulia na alipata maumivu katika kiuno
Kamala:Maumivu hayo yalisababishwa na kitu gani?
Shahidi :Inawezekana ikawa mkono,mbao ama fimbo
Baada kumaliza kutoa ushahidi,mwanasheria wa serikali aliieleza mahakama kuwa amefunga ushahidi upande wa mashitaka na kuomba mwenendo wa kesi hiyo. Ombi hilo lilikubaliwa na mawakili wa utetezi na hakimu Karayemaha alisema kesi hiyo itatajwa desemba 4 mwaka huu na kueleza kuwa kama mwenendo mzima wa kesi utakuwa umekamilika siku hiyo watapatiwa