CCM Yaanza Rafu!, Yaandaa Zengwe Kuwapiga Panga Baadhi ya Wagombea!

Pasco, Ulivyoileta thread yako inaonyesha wazi uko upande gani, vijana hawatatusaidia chochote kama hawana vigezo vinavyohitajika, na uzuri wake umevitaja. Lile bunge si bunge la kisiasa kama bunge letu la ndani la NDIYOO na kupiga meza, linahitaji mtu mwenye uwezo wa kuchambua sheria na mchumi.

Elewa kule hatuendi kushindana kisiasa vinashindana vifungu vya sheria, tunakwenda kuwaambia Kenya kuwa sheria zetu kwenye ardhi zinasema hivi, kwenye immigration zinasema hivi kama hamkubaliani navyo basi. Kwa hiyo tunahitaji mtu wenye uwezo wa kutetea hayo si kutetea tu mwenye uelewa mzuri. At least awe na ujuzi wowote wa sheria au uchumi, kama huna hivyo unakwenda kufanya nini. Tusifanye masihara kwenye hili wenzetu Kenya na Rwanda wako serious when comes to defend their countries, they mean business.

Kumbuka Nile Delta Agreement Misri walivyotupiga bao kuuvunja ni kazi, tusirudie makosa ya aina hiyo kwa kupeleka incompetent people tutastukia nchi na ardhi inauzwa.
 

Mkuu Ndachuwa nashukuru kwa hii maneno umeweka hapa;

1. Pasco; Kwa nini uliamua kutumia maneno kama "Yaanza rafu" na "Yaandaa zengwe" badala ya "Yaweka mazingatio na vigezo vipya kwa wagombea"

Hii ingekuweka wewe (ukiwa mtoa mada not as Pasco) huru na topic hii ila kwa jinsi ilivyo ni kama umekerwa na huafiki hatua hii ambayo mimi naiona ni chanya sana na ina manufaa kwa Taifa hili kwani inatupa sasa nafasi ya kuhoji vigezo vya mwanzo vilivyotufikisha hapa na kuwa na wagombea hawa as yawezekana walioachwa ndo khaswaa tunaowahitaji

KEYS; UMRI, SHAHADA YA UCHUMI NA AU SHERIA, UZOEFU WA KIDIPLOMASIA

Kama kweli tunaipenda nchi yetu na tunataka mabadiliko then ni lazima kuangalia kila jambo with high degree of neutrality so as to obtain and maintain objectivity

UMRI; Sijaona popote walipoweka limitation ila ni zingatio kwamba tuchague watu ambao ni age relevant na kazi tunayotaka kuwapa.....cha maana ni sisi vijana kuwabana wazee kwa hoja kwamba ni vipi tofauti ya umri inaweza kuwa kigezo kama wote ni watu wazima kwa mujibu wa sheria na vigezo vingine muhimu wanavyo.........hapo hachaguliwi baba wa ubatizo jamani....ni Mbunge

SHAHADA; Wao wamependekeza hizo mbili.....kama tunaona hazifai tuweke mbadala na justification ya kila ongezeko au punguzo........sasa kama mtu specialization yake haieleweki tumpe tu kwa sababu ya ujana au uzee wake?????
Mfano; Kuna watu wamesoma political science with/ and economics hawa pia wana mawanda mapana sana kwenye issues revolving arround the stake of the union na kama ni sheria mwanasheria wa wizara ata-complement kwenye mahitaji ya kufanya hivyo......au hata mwanasheria mkuu.....chief justice etc etc...team work approach

UZOEFU WA KIDIPLOMASIA; Yaweza kuwa hoja yenye mashiko lakini ina maswali mengi pia kabla ya kupitishwa.....si tunao mabalozi kwenye nchi hizo husika???? Ofisi za kibalozi zina tija gani kwa union hii??? Attachee(s), Liaisons......is not this a high time for these people to recogn the importance of having round table chambers in their routines?????

Mystand;
1. The so called wazee nao pia ni watu na watapenda kuwa hapo walipo hata kama ni machweo ndo hulka ya wanaadamu walio/ tulio wengi ila kwa sababu mawasiliano yanawezesha kuwa na malumbano ya hoja kama hivi then tuendelee kuboresha hoja zetu kama vijana.
2. Unless we have good, sustainable and persistent pressure being echoed with clearly defined pre-requisites on the so called liberation via youths tutakuwa tunaonekana kama walalamishi na waroho wa madaraka kwa sababu hoja za hao wanaotaka kutuwakilisha (vijana) ni sooo light yaani kama ni mtihani kwa kweli watafeli wanashindwa kutuwekea plans, mission, vission za wao kama vijana as compared to Wazee wetu.....sasa hapo ujana utatusaidia nini???? Labda kama kuna kukimbia huko bungeni sawa

Hii sio rafu wala zengwe ni changamoto tu na kama kweli sisi vijana tumeazimia kuleta mabadiliko na tuanze kuwa na tabia ya kuchukulia mambo kama fursa na si kama vikwazo......na ndio moja kati ya tofauti baina ya THE CONSCIOUS REVOLUTIONARIST as compared to A MERE POLITICAL ASPIRANT
 

Hii ni hoja muhimu sana kuliko kupeleka baharia...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…