CCM Yaanza Rafu!, Yaandaa Zengwe Kuwapiga Panga Baadhi ya Wagombea! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Yaanza Rafu!, Yaandaa Zengwe Kuwapiga Panga Baadhi ya Wagombea!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Apr 12, 2012.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,561
  Likes Received: 18,294
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Nyakati za uchaguzi mjini Dodoma, ni nyakati, za harakati kubwa na pilika pilika nyingi katika mji wa Dodoma, hivyo sisi wenye interest na siasa za nyumbani, tupatapo nafasi, hupenda kupeleka pua japo kidogo mjini Dodoma japo kunusa tuu kile kinachoendelea.

  Miongoni mwa pilika pilika kubwa za kisiasa mjini Dodoma kwa sasa, ni harakati za kugombea ubunge wa Afrika Mashariki ambapo vikao vya wazi na vya siri vimekuwa vikiendelea mjini hapa, huku wagombea wakijitahidi kuandaa "the winning coalition", huku wabunge ambao ndio walengwa wakijikuta katika wakati mgumu kuchagua kambi ya mgombea gani waiunge mkono!.

  Mvutano mkubwa wa vuta nikuvute, shika nikushike ni miongoni mwa wagombea 9 wa CCM wanaogombea nafasi 3, hivyo ushindani ni mkubwa kuliko huku kila mmoja akiepuka kudondokea miangoni mwa wale 6 wataopigwa chini, hivyo pia kuna harakati za chini chini kila mmoja wao akifanya jitihada za kujinusuru.

  Ushindani mkubwa ni kati ya wale wanaowaunga mkono vijana wa kisasa ambao wana uughwaji mkubwa na wana CCM wanaotaka mageuzi ya ukweli dhidi ya wagombea wazee ambao tayari ni spent force, watakuwa hawana jipya la kuleta zaidi ya kumendea fungu la kustaafu kwa heshima!.

  Kufuatia upepo kuwavumia vizuri wagombea vijana, kuna tetesi kuwa wagombea wazee kwa kuwatumia wazee wa CCM, wamejipanga kuwaundia zengwe wagombea vijana ili kuwapiga panga la kimtindo!.

  Zengwe hili linapikwa chini kwa chini ambapo kwa kuamua kuandaa vigezo vitatu vya sifa mpya za wagombea wa CCM ambavyo wata lobby kuvipeleka kwenye caucus ya CCM over the weekend ili vipitishwe hivyo kuwapiga panga wagombea vijana wenye uugwaji mkubwa wa wabunge wengi.

  Zengwe hilo ambalo msingi wake mkubwa ni kupiga fitna ili kuwapiga chini wagombea vijana.

  Wazee hao wamekuja na viogezo vipya vitatu ambavyo sikuwahi kuvisikia kwenye sifa za uongozi za CCM hata mara moja!.

  1. Umri- eti CCM ichague wagombea wenye umri mkubwa kama uthibitisho wa long expiriance ya uzoefu wa muda
  mrefu! .
  2. Awe na shahada ya Chuo Kikuu ama ya Sheria, ama ya Uchumi kwa hoja kuwa kule kuna issues za kisheria na
  issues za kiuchumi!.
  3. Uzoefu wa kidplomasia.

  Lengo la vigezo hivi ni kuwaengua wagombea vijana!

  Baadhi ya wabunge wa EALA ambao ambao hawagombei tena, wamepiga kambi bungeni hapa wakiwa na wagombea wao kwapani, wengi wakiwa ni hawa wazee ambao ni spent force!.

  Wakati huo huo, nimehudhuria tafrija moja mahali, usiku huu hapa Dodoma, kufumba kufumbua, kumbe ni tafrija ya kampeni ya wazee fulani wawili, ambao walituamkia wote kwa shikamoo!.

  My Take.
  CCM kama chama, kimekaa mkao wa kifo, watu pekee wanaoweza kukinusuru CCM na kifo cha aibu, ni hawa wagombea vijana wa kileo ambao sasa wanataka kupigwa zengwe. Kama kweli itatokea CCM ikawapiga zengwe hawa vijana, hiyo ndio itakuwa uthibitisho wa CCM ni chama mfu, hakiwahitaji vijana wa kisasa, wito wangu kwa vijana hawa ni kuwa baada ya kupingwa panga, hameni CCM, achaneni na CCM ili mjiokoe nafsi zenu kwa 2015, jiungeni na vyama vinavyo kubali nguvu ya vijana, vinginevyo down the drain, mtakwenda chini na CCM yenu!.

  Asante.

  Pasco.
   
 2. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,087
  Trophy Points: 280
  Mkuu hata hao wazee wakishindwa basi watoto wao watang'ara..kwahiyo kitu ni kile kile.
  ebu tusubiri kama William atapona.
  halafu hiyo heading inashtua
   
 3. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  mtoto wa nyoka ni nyoka
   
 4. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,674
  Likes Received: 17,731
  Trophy Points: 280
  Pasco umeniumizia kichwa bure kusoma, kumbe ni mambo ya Mitumba ya CCM bana, we gat a brand new and talk in town called CHADEMA. They begin with god, and will finish with god
   
 5. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hii uchanguzi havutii maana CCM INAKUFA
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Baada ya performance ya Lucinde huko Meru, sina hakika na hoja ya vijana wa CCM! Wamelelewa vibaya, na afadhali wawapige chini wasipeleke aibu kwa majirani zetu.
   
 7. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  ILA MKUU PASCO WA JF

  Punguza BAHASHA maana wewe huitaji nchi ikombolewe
   
 8. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #8
  Apr 12, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,788
  Likes Received: 36,786
  Trophy Points: 280
  acha wafu wawazike wafu wao. :rip:
   
 9. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #9
  Apr 12, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  pasco mbona hugombei??nimemuliza william, kwenye ile thread yake ya kumsifu nasari lakini hakujibu'nataka kujua next step kama akishindwa hizo mbio zake''atarudi new york au tumtafutie kazi hapa hapa??
   
 10. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #10
  Apr 12, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  unamaana vijana wa cccm wamelelewa kama lulu
   
 11. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #11
  Apr 12, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,674
  Likes Received: 17,731
  Trophy Points: 280
  Na yule Kijana wa zamani wa CCM Benjameni William Mkapa tunaenda kumzomea kesho UDSM, unless otherwise atueleze na tuelewe privatization imetusaidia nini, na je ndivyo alivyotumwa kufanya ikulu na Mwl.Nyerere
   
 12. M

  Mkekuu JF-Expert Member

  #12
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Upo saaaaawa.
   
 13. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #13
  Apr 12, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Williama yuko wapi?
   
 14. Jembe Ulaya

  Jembe Ulaya JF-Expert Member

  #14
  Apr 12, 2012
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 456
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  They smile in your face, dirty bastards back stabbers, ndio CCM hao. Cha kushangaza ni nini? Hu ni mchezo wao wa kila siku.
   
 15. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #15
  Apr 12, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ulichokosea ni hapo uliposhindwa kuwataja majina!
   
 16. 2015ready

  2015ready JF-Expert Member

  #16
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mbona ni vigezo vyenye maana sana tuu? Mimi sioni kama kuna tatizo kwenye hilo. Wawakilishi wetu EAC ni lazima wawe wenye uzoefu, na wamesoma. Lakini hii haimaanishi kuwa hata wao wazee wataupata huo ubunge.
   
 17. K

  Keil JF-Expert Member

  #17
  Apr 12, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Pasco,

  Title na contents haviendani ... mimi nilidhani ni Uongozi wa CCM, kumbe ni rafu za wagombea wao kwa wao? Hilo ni kawaida sana ndani ya CCM.

  Hoja ya elimu inaweza kuwa na mashiko, ingawa mwakilishi yeyote wa CCM huwa ninamchukulia kwamba anawakilisha maslahi ya chama chake kwanza. Kwa hiyo kwangu mimi sioni tofauti whether ni kijana au mzee, wote ni wale wale tu, "opportunists".

  Mfano mzuri ni kwenye mswada wa Katiba sikuona hata kijana mmoja kati hao mnaowaita waleta mabadiliko ndani ya CCM aliyesimama na kutetea maslahi ya Taifa. Sana sana huwa tunawaona wako kimya, wakitoka kwenye vikao wakiwa huku kitaa ndo wanakuja na tambo za kufa mtu kwamba wao ndo wataleta mabadiliko ndani ya chama. Mabadiliko my foot!

  Piga ua galagaza, kuna vijana ambao hata wafanye nini hawatavuka kiunzi, Papaa Mkulu Mamvi hatawaachia wapenye. Wao wakomae na kura za kutoka kwa wapinzani. Lakini wanachoniboa hao vijana, wakishaingia huko ndani hawaleti mabadiliko tunayoyataka, wanaishia kuwa akina ndiyo mzee na kuanza kutumia lugha ya kejeri kwa wapinzani na huku ni wabunge hao hao wa upinzani waliowasaidia kuingia kwenye EALA.

  Naomba nikukumbushe picha ya Nape Nnauye kwenye kile kikao cha NEC ambacho Lowassa alimnyooshea kidole JK. Ile picha ya Nape akisalimiana na Lowassa na pembeni yuko Sumaye, ilikuwa na mengi sana. Yule hakuwa Nape ambaye alikuwa anatamba kwenye majukwaa, siku hiyo alikuwa mdogo kama piriton. Juzi kati hapa kwenye mgomo wa Madaktari, Kigwangalla walitaka kumtoa macho wabunge wenzake wa magamba. Baada ya hapo Kigwa hakuongelea tena swala la mgomo wa madaktari. Hawa ndio vijana wa kuleta mabadiliko kweli?

  Kijana yeyote ambaye yuko CCM akiwa na ndoto ya kuleta mabadiliko, anaota ndoto ya mchana. CCM hawataki mabadiliko na hata Katiba Mpya wamelazimishwa, hata hizi kauli za Taifa kwanza wanazitoa kwa kujilazimisha. CCM wanataka kila kitu kibaki kama kilivyo, ndo maana hata kwenye hizi kampeni za chaguzi ndogo akina Mwigulu wanatuhumiwa kumwaga hela nyingi ili washinde. Sasa vijana kama hao wana tofauti yoyote na status quo ambayo inanunua uongozi? Hapa tunadanganyana tu.

  Mimi ninawaona ni vijana "opportunists" tu ambao wanataka ulaji na ndio maana hata wakiwa Bungeni huwezi kuwasikia wakikemea uozo au uovu. Mtu anayetanguliza Taifa kwanza angewapasha wabunge wenzake wa magamba ambao walikuwa wajadili mswaada wa sheria ya kuandika katiba kwa mipasho na ushabiki.

  Hakuna mabadiliko yatakuja kutokea ndani ya CCM, mwaka mzima sasa tangu secretariat ibadilishwe, hakuna kipya nilichokiona. Walijitutumua mwanzo, sasa wamerudi kwenye status quo na hakuna ambaye anaongelea kuvua gamba wala mabadiliko.
   
 18. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #18
  Apr 12, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Pasco anapaswa asome mara tatu au nne akuelewe, si kwa ugumu wa lugha, hasha! ni kwa ukweli wa maandishi mstari kwa mstari, neno kwa neno.
  kwa kuongezea mfano, Mwigulu ambaye ni mhazina wa ccm, anajidai kumuuliza pinda kuhusu mpango wa chenji ya rada, kanakwamba hajui, usitegemee huyu kijana kuyatenda matakwa ya wananchi, atatufanyia ukanumba tu, kumbe mzinzi mkubwa.
   
 19. chitalula

  chitalula JF-Expert Member

  #19
  Apr 13, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,307
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  kaka uko sahihi kabisa
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  Apr 13, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,561
  Likes Received: 18,294
  Trophy Points: 280
  Keil kumbe ni kaka??
   
Loading...