CCM ya sasa ni ya Kaskazini, Pwani na Unguja

CCM ya sasa ni ya Kaskazini, Pwani na Unguja

Kwa sababu ni wabinafsi!
Na kwa sababu wanaishi ki-
Cartel zaidi.
Na ni ving'ang'anizi wakishika wanafanya ya kwao milele!
Mfano ni hapo Chadema!
Mbowe ni mwenyekiti wa maisha!
Ukimbishia ana... ku-chachawangwe chap!
Lipumba ambaye ni mwenyekiti wa Cuf miaka na miaka, Cheyo, UDP, Maalim Seif, hawa walikuwa ni wa Kaskazini?
Kweli Magufuli aliondoka na akili zenu
 
Uongozi wa juu wa Sasa wa CCM umesheheni makada toka pande tajwa hapo juu.

Kanda ya Ziwa, Kati na Nyanda za Juu kusini hawaaminiwi na watu wa pwani. Waliaminiwa na mwendazake wakati huo wanaoaminiwa sasa wakiwa wametengwa.

Je, kuna CCM mbili ndani ya chama kimoja? Tusubiri tuone.
Nyanda za Juu hatutaki kabisa kutuhusisha na dhalimu Mwendazake alitutenga..

Nyanda za Juu Kwa Sasa hata kama hatuna viongozi ndani ya ccm ila tuna viongozi lundo serikalini yaani kiufupi ndio tumeshika serikali.

Spika,
Mawaziri 2 ,utumishi na Maliasili,
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wote 2,
Naibu Waziri 3,Tamisemi,Maji, biashara
Katibu Mkuu Wizara 2,Mifugo na Maji,
Wakuu wa Taasisi kama TanRoads nk

Yaani hao ni wale wenye maslahi ya Moja kwa Moja Ila wako wengi kiasi kwamba Sasa hivi ajenda za maendelea nyanda za Juu zinasonga..
 
Uongozi wa juu wa Sasa wa CCM umesheheni makada toka pande tajwa hapo juu.

Kanda ya Ziwa, Kati na Nyanda za Juu kusini hawaaminiwi na watu wa pwani. Waliaminiwa na mwendazake wakati huo wanaoaminiwa sasa wakiwa wametengwa.

Je, kuna CCM mbili ndani ya chama kimoja? Tusubiri tuone.

Huyo wa kaskazini (macha )yuko mmoja tuu hao wengine ndio wengi sijaona hoja yako ya kusema kaskazini hapo.
Hayo ndo tunayaita "mawazo muflisi"
 
Ccm kanda ya kati, ziwa na magharibi mliaminiwa mkajaA mapanga, visu, jambia na sindano za sumu kila mnapotembea.

Kaeni benchi kwanza
We chawa inaonekana kichwa chako kimejazwa kamasi badala ya akili. Mimi nazungumzia jinsi wana Mbeya tumegeuzwa machawa wa kumsifu mwenyekiti wa chama na genge lake, na picha ya mwana Mbeya mwenzetu akiwa busy kumsifu mwenyekiti wa chama anaetoka kaskazini na genge lake badala ya kusifu chama, sera za chama au mikakati ya chama afu wewe zuzu unakuja na habari zisizoeleweka.
Unachotakiwa ni kutuambia kwamba ni lini na Sisi wana Mbeya tutaaminiwa na kupewa uenyekiti wa chama taifa au umakamu mwenyekiti au ukatibu mkuu na sio tu kuwa machawa wa wajanja wachache wa kaskazini wanaokula mema ya chama bila kutushirikisha wapambanaji wao.

jibu hoja yangu ni kwanini wana Mbeya tunaaminiwa kuzidi kwenye matusi, kejeli na maandamano Lakin kweny uongozi wa juu wa chama wanaaminiwa watu wa kaskazini?
 
Uongozi wa juu wa Sasa wa CCM umesheheni makada toka pande tajwa hapo juu.

Kanda ya Ziwa, Kati na Nyanda za Juu kusini hawaaminiwi na watu wa pwani. Waliaminiwa na mwendazake wakati huo wanaoaminiwa sasa wakiwa wametengwa.

Je, kuna CCM mbili ndani ya chama kimoja? Tusubiri tuone.
Hivi SG Chongolo ni wa pwani, kaskazini au Zanzibar? NEC umeiangalia? Kamati Kuu? Lakini kubwa kabisa; kwa nini una fikra za kikaburu na za ovyo kabisa kuangalia masuala ya ukanda? #Haipendezi, acha. 🙏🙏🙏🙏
 
Na sisi chadema tunataka safari hii mwenyekiti wetu atoke Mbeya.

Sio kila siku wana Mbeya tutumiwe tu kwenye maandamano uchwara, fujo, matusi na kelele zisizokuwa na msingi dhidi ya serikali yetu hata pale inapofanya vizuri katika mkoa wetu tunafunzwa kupinga tu kama ilivyokuwa kwa wana Kigoma wakati wa Kaburu, huku zile nafasi nono za ulaji wa chama wakipeana wajanja wa chache wa kaskazini.

Hili linaumiza wengi, sema ndo hivyo viongozi wetu wa chama mkoani Mbeya wameamua kuuza utu wao na uaminifu wao kwa sababu ya matumbo yao.

Huku ubaguzi wa wazi ndani ya chama chetu unaofanywa dhidi yetu wakiufumbia macho.

Ni dharau, kejeli na aibu kwa wana Mbeya kila siku kutumiwa kwenye uchawa namna hii.
Acha upuzi wewe CHAWA, CHADEMA haina siasa za ukanda wala ukabila, ni UTAIFA tu.
 
Uongozi wa juu wa Sasa wa CCM umesheheni makada toka pande tajwa hapo juu.

Kanda ya Ziwa, Kati na Nyanda za Juu kusini hawaaminiwi na watu wa pwani. Waliaminiwa na mwendazake wakati huo wanaoaminiwa sasa wakiwa wametengwa.

Je, kuna CCM mbili ndani ya chama kimoja? Tusubiri tuone.
Mwl. Nyerere akiwa ndiye muasisi wa Tanganyika huru hatimaye Tanzania huru, alifanya kila jitihada kujenga taifa lisilokuwa na ukabila wala udini. Sasa badala ya kuendeleza maono yake, sasa hivi watu wenye fikra finyu wanaturudisha kule tulipotoka ambapo waasisi wa taifa letu walitaka tutoke.

Hivi mtu unaathirika kivipi kama kiongozi anatoka katika kanda ambayo wewe hutoki? Ama unapata faida ipi kwa kuwa na kiongozi ambaye ana dini na kabila moja na wewe!?

Kiongozi ambaye amepewa dhamana ya kuongoza taifa kupitia masharti ya katiba ni kiongozi wetu, haijalishi katokea upande gani wa taifa letu.
 
Nguvu ya CCM ni mwenyekiti, hakuna zaidi.. hta wanec wote wakatae mwenyekiti akishasema watafyta mkia.. kumbuka enzi za Edo alifikir akijaza wanec na CC ya chama basi amepitaaa...
Kaangalie wajumbe wa NEC ndipo utaelewa nguvu ya CCM imelalalia wapi

All in all pamoja na mapungufu yake lakn CCM imebeba taswira haswa ya nchi kwakuwa watendaji ndani ya chama mpaka wajumbe wa NEC wanatoka pande tofauti tofauti za nchi yetu

Hili pía lingehamia huku upinzani kwetu Chadema ingefuta ile dhana ya ukabila na ukanda iliyomea kwa miaka mingi ndani ya chama!!!
 
Uongozi wa juu wa Sasa wa CCM umesheheni makada toka pande tajwa hapo juu.

Kanda ya Ziwa, Kati na Nyanda za Juu kusini hawaaminiwi na watu wa pwani. Waliaminiwa na mwendazake wakati huo wanaoaminiwa sasa wakiwa wametengwa.

Je, kuna CCM mbili ndani ya chama kimoja? Tusubiri tuone.

Uko sahihi ila sio Bagamoyo ambako wanaipenda sana ccm kama akitajwa JPM na cuf kama akitajwa Maalimu Seif.

Pwani ya Chalinze, Mkuranga na Kibiti ndio wanategemea CCM lakini sio Kisarawe, Kibaha na Bagamoyo
CCM ya sasa imesheheni watu wa kaskazini mashariki Hata hivyo Tanga, Muheza, Handeni Na Pangani hawamwelewi kiongozi wa nchi kabisa kwa sasa

Wananchi wa kawaida huko Kilimanjaro hamwelewi kabisa kiongozi wa nnchi na wanalalamika vibaya mno.

Wanufaika wengine wa utawala huu ni Kigoma ambao awali walikuwa wakiyumbishwa na vuguvugu la CDM na ACT kwa sasa wana lamba asali.

Wanaomwelewa kiongozi wa nchi huko Mbeya ni wale wanaotoka Rungwe Tukuyu pekee wengine wote hawataki hata kusikia.

Iringa na Njombe hawamwelewi kabisa pamoja na kwamba kuna chawa wengi wakitokea huko lakini wananchi wa kawaida hawataki kusikiliza maneno matupu bila vitendo halisia.

Kanda ya Ziwa au kaskazini magharibi huko ndio manunda watupu ukienda wanajifanya kukuchekea lakini moyoni wana lao jambo lisilo la kwaida na ni vigumu kuwabadilisha wakiwa na uamuzi wa sirini.

Dodoma ni aibu tupu na ndio mara kwanza CCM itapasuliwa uchaguzi ujao na kukoksa baadhi ya majimbo labda waended waombe msamaha kwa akina agwe.
Singida huko wanavizia tu akitolewa mtu wao kutoka kwenye baraza la walamba asali wataamua la kufanya.

Morogoro kuna misimamo mikali isiyo yya kawaida ukiwakosea inatarajiwa watabadilisha sura za wabunge karibu wote wa mkoa huo kwenye uchaguzi ujao.
 
Uongozi wa juu wa Sasa wa CCM umesheheni makada toka pande tajwa hapo juu.

Kanda ya Ziwa, Kati na Nyanda za Juu kusini hawaaminiwi na watu wa pwani. Waliaminiwa na mwendazake wakati huo wanaoaminiwa sasa wakiwa wametengwa.

Je, kuna CCM mbili ndani ya chama kimoja? Tusubiri tuone.
Siasa za ukanda na ubaguzi wa aina yeyote sio hulka wala utamaduni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)!
 
Back
Top Bottom