Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,848
- 50,564
Wanasaikolojia husema binadamu (siyo mtu) dhaifu hujaribu kuficha udhaifu wake kwa kufanya mambo yake kwa kutegemea mitulinga.
CCM imekuwa inaongoza nchi hii Kwa zaidi ya miaka 33 sasa tangu mfumo wa vyama vingi urejeshwe hapa nchini.
Lakini Katika jambo ambalo CCM wameshindwa kabisa kulitafutia ufumbuzi ni suala la ajira (siyo kazi) na ujira Bora Kwa watanzania.
Miaka nenda miaka rudi kwa zaidi ya miongo mitatu sasa CCM haijui ifanye nini kuongeza ajira na kuweka uhakika wa ajira kwa watanzania huku ujira kwa watanzania ukiwa mzuri na wa uhakika.
Hali hii inatokana na CCM kuwaza kuwa ajira ni kazi na kuwa kila kazi ni ajira. Upotofu huu umefanya ajira kisiwe kipaumbele cha CCM.
Viongozi kadhaa utawasikia wakisema kuwa "kama maisha ya mjini yamekushinda rudi kijijini ukalime". Yaani zama hizi kweli kulima kwa jembe la mkono inakuwaje ni chanzo cha ajira!?
Ukisikiliza jinsi CCM inavyowaona wamachinga, bodaboda au wapiga debe kuwa ni ajira rasmi, ndipo unapojua kuwa CCM inaona ajira ni kazi za kutoka jasho pekee!
CCM wekezeni kwenye matumizi ya akili ili kuongeza ajira kwa watanzania.