kukomya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2011
- 344
- 144
Wana JF, nilikuwa Kasulu kwa juma zima kishughuli na leo nimeshuhudia CCM wakiumbuka kweupeee! Toka siku kama tatu hivi zilizopita magari yalikuwa yakirandaranda mitaani kuwaalika watu kuhudhuria mkutano wa CCM katikati ya mji wa Kasulu kwenye stendi ya taxi ambapo kwa mujibu wa matangazo ulikuwa uhutubiwe na viongozi waandamizi akiwemo yule jangili wa meno yaliyokamatwa kule Hongkong Kinana . Magari yale yalikwenda hadi vijiji jirani ambako inasemekana walipeleka 'takrima' ya kuwashawishi watu waache shughuli zao leo, wakubali kusombwa hadi mjini ili kufanikisha dhana ya CCM bado 'inapendwa' Kasulu.
Leo walikutana na Kisanga ambapo waliopewa 'takrima' vijijini waliingia mitini na mkutano wao kudorora na kiasi cha kuonekana kama mkusanyiko wa kikundi cha watu wanaomshangaa mcheza sarakasi!
Watu wengi walionekana wakiendelea na shughuli zao za kila siku huku wakisema maneno ya kuwaponda CCM, niliowakuta sokoni waliibeza CCM ambayo walikuwa wakisema wazi wazi kwamba wao (CCM) ndiyo chanzo chaa ugandamizwaji wa maendeleo ya mkoa huu wakitolea mifano ya kwamba iliwabidi kusubiri miaka 51 tokea kupata Uhuru kwa serikali ya CCM kuwapelekea majenereta ya umeme na hadi leo hii maji wanayokunywa ya bombani ni tope tupu baada ya Halmashauri kushindwa hata kununua shabu ya kusafishia maji.
Kwa upande mwingine waliwalaumu wapinzani na haswa CHADEMA kwa viongozi wakuu kushindwa kuja kufanya mikutano hapa na Kibondo - wilaya zoilizompa kura nyingi Dr. Slaa kuliko Kikwete. Walisema idadi kubwa ya wakazi wa wilaya hizi mbili ni wapenzi wa CHADEMA na hata zile kura walizowapa wapinzani kupitia NCCR walikipa chama hicho baada ya CHADEMA kushindwa kusimamisha wagombea wanaokubalika.
My Take: CHADEMA iitumie fursa hii ya kukataliwa CCM kuhamasisha wananchi na wasingojee hadi uchaguzi ujao.
Nashauri viongozi waandamizi wa chama akiwemo Mh. Mbowe, Dr. Slaa, Zitto na wengine kuja kuwashukuru wananchi wa eneo hili kwa kuonyesha ari ya kuziunga mkono juhudi za ukombozi zinazoongozwa na CHADEMA.