Watu wamekuwa wanajiuliza kwa nini namba ya wapiga kura huwa inapungua tofauti na idadi ya watu walioandikishwa?!Je ni kweli huwa watu hawajitokezi kupiga kura?
Majibu ni haya.
1. CCM hukusanya vitambulisho vya wapiga kura kwa njia za hila na kuanza kuvipitia kwa jina moja moja/majina kupitia mabalozi wao wa nyumba 10 na kubaini watu wa vyama vya upinzani au wasio unga mkono CCM. Wakibaini watu hao kwa njia ya pembejeo kama case study ya Kalenga au Mgawo wa mahindi kama walivyo fanya Igunga vitambulisho vya watu hao hutengwa pembeni na kuzuiwa mpaka uchaguzi utakapo kwisha, wakati mwingine vitisho hutumika kwa watu kuambiwa labda vitambulisho vyao viko kwa mkuu wa wilaya kwa ukaguzi, au viko kwa mkuu wa kituo cha Polisi kwa uhakiki wa maina.
2. Kununua viparata vya kupigia kura kwa watu ambao wana tamaa ya fedha au kuwapa fedha na zawadi mbalimbali ili wakaipigie kura CCM, Kuna baadhi ya maeneo kuna watu wamepewa mpaka rushwa za chumvi, magodoro na hata vyarahani vya kushonea (Mama Men.. alisha wahi kugawa vyarahani kwa kina mama wa Moshi mjini). Njia hizi huchangia kwa namna moja au nyingine kupunguza idadi ya wapiga kura. Na ndio zimekuwa zinatumia na CCm kupata ushindi bila wao kujali kuwa wana najisi misingi ya kidemokrasia na haki ya kuchagua na kuchaguliwa.