CCM Wapokea Kadi za Wapinzani / UKAWA kwa Malundo

CCM Wapokea Kadi za Wapinzani / UKAWA kwa Malundo

Ccm wanachapisha kadi za chadema halafu wanadai wao wamevuna.....kweli wamechoka!
 
CCM WAPOKEA KADI ZA WAPINZANI KWA MALUNDO



SUREZZ.jpg


58.jpg


4.+Mwingulu+akionyesh+kadi+za+Chadema+na+TLP.jpg


14.jpg


Wapinzani wa Vyama Vyote Warudisha Kadi kwa Malundo

Kwa mshangao mkubwa kadi nyingi zinazorudishwa ni mpya. Najiuliza wenye kadi hizo kweli walikuwa wana UKAWA /chadema?
My take : hiyo ni janja ya popo kupandisha mjuu guu na kuachia mzigo kupitia paji la Uso.
 
haahaaa.....wewe mleta uzi unajua vema....
masaburi kajaribu ila kashindwa naona bado mnaendeleza sanaa zenu feki na mtakoma.
lowasa anawatesa mno
 
Ugomvi wa wanaume ni Mtamu sana. walijua kukata ni jambo rahisi sana sasa jamaa akamua kushika pu...bu wanalia kila kuona na jamaa kakomaaa, mmmmh!!!!!!
 
ili kuwaamin ccm ni lazima ujitoe ufaham hawa jamaa wanaongoza kwa siasa za propaganda wakiongozwa na masaburi na sasa ivi anakusanya kadi za watu na kuchukua namba ya kitambulisho huyu jamaa sijui anapata wapi nguvu yakufanya hayaa mamboo na bado anadhururaa mtaani
 
Huwezi kuamini jinsi gani ama (1) watu wako bado in denial (2) ama wanashabikia tu bila kufikiria kwa makini gharama (consequences) zitakazowatokea watanzania ikiwa kweli wanachosema kitatimia (3) ama wapo katika jamii forum kama jeshi la mashambulizi la ku-deflect kila linaoongelewa ambalo ni negative lakini la ukweli kuhusu mgombea wao. Inanifanya niwe na shaka kama hawa wanaondelea kutetea kumsimamisha mtu ambae ni fisadi kama raisi wa nchi, if they lived that moment wakati taifa likiwa gizani. Ama kweli walikuwa wamekomaa kiumri kipindi cha Richmond kuweza kuyaelewa vizuri yaliyotokea ktkkipindi hicho. Kwani kipindi kile hakuna mtu alichukiwa kama Lowassa kwa jinsi alivyowaingiza wananchi waliokuwa wakiishi katika giza zito katika matatizo makubwa, biashara zao kusimama na kipato kupotea kwa ajili ya mikataba mibovu isiyofikirika. Wengine wakipoteza maisha kwa kuungua moto ndani ya nyumba zao kutokana na majenereta kuwalipukia wakiwa majumbani mwao kwa kukosa umeme. Na kila sehemu ulikopita mjini Dar ilikuwa ni joto la kutisha na kelele za magenereta kwenye maduka, maofisi na karibu kila ulikopita. Umeme ulikuwa kwa mgawo nyakati za usiku tu, na katika hayo masaa mawili matatu ambayo wananchi walipata umeme. Vijana waligeuza usiku kuwa mchana, wakikesha kusubiri umeme ili waweze kufanya kazi za kutengeneza grill na shughuli zingine zilizohitajika kufanyika tu kwa umeme. Na wakati wakiwa katika mateso yote hayo, Lowassa akiwa waziri mkuu na chini ya usimamizi wake akaiingiza nchi kwenye mkenge kwa kuingiza watanzania ktk mkataba na kampuni la printing ambalo haliusiani kwa namna yoyote na kuzalisha umeme. We lived it!!! We can never forget that moment.. Leo hii hao wanaosema wanataka mabadiliko kwa kumchagua huyu aliyewasaliti watanzania kipindi kile kuwa rais, kwa mawazo yangu hawaitakii mema Tanzania na watanzania. Tujifunze kwa wenzetu walioharakisha harakati mabadiliko, yalivyowatokea puani baadae. Angalia Arab spring.. ni nchi moja tu iliyotoka salama Tunisia, nyingine zote ni matatizo juu ya matatizo. Angalia wimbi la wakimbizi duniani wanaokimbia nchi zao, kupoteza maisha kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe, na wakiwa njiani kutafuta safe haven. Tanzania tusifike huko. Tutumie busara na sio ushabiki. Nakubaliana mabadiliko ni muhimu, lakini sio kwa kumweka fisadi kama kiongozi wa mabadiliko, na kwa maana hiyo sasa sio given huyo fisadi aliyesimamishwa, huu sio wakati wake.
 
Wana waleteeni hizo kadi wakijua kwamba mnazinunua kwa bei kubwa kisha siku ya uchaguzi wanakuja kuwamalizeni na kitambulisho cha mpiga kura. Leteni mchezo na wana UKAWA nyie.
 
Walizo nunua wao
 

Attachments

  • 1441501495715.jpg
    1441501495715.jpg
    67.2 KB · Views: 114
Back
Top Bottom