CCM Wapokea Kadi za Wapinzani / UKAWA kwa Malundo

CCM Wapokea Kadi za Wapinzani / UKAWA kwa Malundo

Ningekuwa mtu wa propaganda wa ccm vijamaa kama huyu ningemkataza kupost maana anaivua sana nguo ccm bila kujua, picha za arumeru enzi hizo anazipost leo, unasema kadi kwa marundo unaonesha kadi 12 mpyaa..ni kuiharibia ccm maana hata ile imani ndogo iliyobaki inaisha kwa uongo uongo hivi na magufuli anaonekana checkbob tu muongo muongo
 
Wee gamba unaleta picha za miaka nyuma sumari yupo chadema sasa hiyo picha ni uchaguzi mdogo wa arumeru kwa nasari mnaweweseka sana na bado
 
Huwezi kuamini jinsi gani ama (1) watu wako bado in denial (2) ama wanashabikia tu bila kufikiria kwa makini gharama (consequences) zitakazowatokea watanzania ikiwa kweli wanachosema kitatimia (3) ama wapo katika jamii forum kama jeshi la mashambulizi la ku-deflect kila linaoongelewa ambalo ni negative lakini la ukweli kuhusu mgombea wao. Inanifanya niwe na shaka kama hawa wanaondelea kutetea kumsimamisha mtu ambae ni fisadi kama raisi wa nchi, if they lived that moment wakati taifa likiwa gizani. Ama kweli walikuwa wamekomaa kiumri kipindi cha Richmond kuweza kuyaelewa vizuri yaliyotokea ktkkipindi hicho. Kwani kipindi kile hakuna mtu alichukiwa kama Lowassa kwa jinsi alivyowaingiza wananchi waliokuwa wakiishi katika giza zito katika matatizo makubwa, biashara zao kusimama na kipato kupotea kwa ajili ya mikataba mibovu isiyofikirika. Wengine wakipoteza maisha kwa kuungua moto ndani ya nyumba zao kutokana na majenereta kuwalipukia wakiwa majumbani mwao kwa kukosa umeme. Na kila sehemu ulikopita mjini Dar ilikuwa ni joto la kutisha na kelele za magenereta kwenye maduka, maofisi na karibu kila ulikopita. Umeme ulikuwa kwa mgawo nyakati za usiku tu, na katika hayo masaa mawili matatu ambayo wananchi walipata umeme. Vijana waligeuza usiku kuwa mchana, wakikesha kusubiri umeme ili waweze kufanya kazi za kutengeneza grill na shughuli zingine zilizohitajika kufanyika tu kwa umeme. Na wakati wakiwa katika mateso yote hayo, Lowassa akiwa waziri mkuu na chini ya usimamizi wake akaiingiza nchi kwenye mkenge kwa kuingiza watanzania ktk mkataba na kampuni la printing ambalo haliusiani kwa namna yoyote na kuzalisha umeme. We lived it!!! We can never forget that moment.. Leo hii hao wanaosema wanataka mabadiliko kwa kumchagua huyu aliyewasaliti watanzania kipindi kile kuwa rais, kwa mawazo yangu hawaitakii mema Tanzania na watanzania. Tujifunze kwa wenzetu walioharakisha harakati mabadiliko, yalivyowatokea puani baadae. Angalia Arab spring.. ni nchi moja tu iliyotoka salama Tunisia, nyingine zote ni matatizo juu ya matatizo. Angalia wimbi la wakimbizi duniani wanaokimbia nchi zao, kupoteza maisha kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe, na wakiwa njiani kutafuta safe haven. Tanzania tusifike huko. Tutumie busara na sio ushabiki. Nakubaliana mabadiliko ni muhimu, lakini sio kwa kumweka fisadi kama kiongozi wa mabadiliko, na kwa maana hiyo sasa sio given huyo fisadi aliyesimamishwa, huu sio wakati wake.
Hivi wanaweake mna nini na ccm.?
1.huu umaskini unavyotesa wenzenu mpaka wanafikia kujiuza hamuuoni
2.sasa hivi hakuna mgao wa umeme..? bado ni lowasa anasababisha..!?
3.watoto waliofeli form four wanaangaika mitaani huwaoni..?
4.wakina mama wanaojifungulia chini huwaoni..!?
5. Wakina mama wanaolala wawiwili wawili wodi za watoto muhimbili temeke mwananyamala hamuwaoni.?!
6.wenzenu wanaotembea kilometa kibao kufuata maji hamuwaoni..?
7.maisha yalivyojuu huon
Mmekazana richmond richmond, nchi ina matatizo kibao mnataka kutuaminisha mtu mmoja ndo kasababisha, litakuwa ni taifa la wajinga kama mtu mmoja ndo kasababisha na tumemshidwa mpaka anagombea urais..hivi hamuooni aibu ..!?
 
Elewa kuwa kura zitapigwa name watz na sio tu waukawa kwa hiyo kadi sio shida wengi hatuna kadi ila tunataka mabadiliko nje ya kijani!
 
CCM WAPOKEA KADI ZA WAPINZANI KWA MALUNDO



SUREZZ.jpg


58.jpg


4. Mwingulu akionyesh kadi za Chadema na TLP.jpg


14.jpg


Wapinzani wa Vyama Vyote Warudisha Kadi kwa Malundo
Hiyo ndiyo kazi anayoiweza Magufuli na team yake,Lowassa atakapo kuwa rais Magufuli atapewa uwakala wa kukusanya taka katika miji yote ya Tanzania maana yake ndio kazi anayoweza kuifanya kwa ufanisi.
 
Hizo kadi na tshirt za Chadema zinazonunuliwa na Masaburi kwaajili ya maigizo?
 
nakumbuka nyimbo moja hivi....wataondoka, wataondoka,,,,,, mashabiki wanaitikia " wataondoka mmoja mmoja..... hatari coastal union hiyoooooo.hiki ndicho chama cha mapinduzi, CHAMA TAWALA...mziki mnene
 
1. Umaskini unamfanya mtu ajiuze? Wale wanaojiuza kwenye western world kwani ni kwa ajili ya umaskini kwani.. Na unajiaminisha kuwa kesho Lowassa akiwa Raisi ndio wataacha kujiuza? pole sana ndugu yangu kama unafikiri hivyo.

2. Mgawo uliopo sasa haufikii hata asilimia 10 ya ule uliokuwepo wakati ule wa Richmond. . From what you write it seems you never lived that moment. Uliza waliokuwepo nchini na Dar wakati ule wakuelezee. Fungua macho ndugu.

3. Watoto kufeli hakutaacha kutokea hata akija Lowassa. Na wewe mwenyewe unasema "kufeli"; maana ya kufeli ni kushindwa kupata maksi zinazokubalika kuonyesha kama umekomaa vya kutosha kuweza kupanda hatua nyingine ya juu ya kimasomo. Kufeli ni factor ya vitu vingi tu, hata nchi tajiri kuna wanaofeli wengi tu. Jitihada binafsi inachangia kwa kiasi kikubwa kinachomwezesha mtu kufaulu. Wengi wa waliofaulu na kuwa na maisha mazuri leo na haijalishi ni watanzania ama la hawakuwa wamezaliwa matajiri kwa taarifa yako..Kufaulu=kuweka bidii binafsi, vitu vingine ni cosmestiques tu.

4,5,6. Wanawake kujifungulia chini ni tatizo lakini huwezi kusema linaongezeka kuliko ilivyokuwa kabla. Angali takwimu ndugu yangu usijisemee tu. Nenda angalia Demographic Health Surveys (DHS) pale utapata data za kutosha kuonyesha trend inavyoendelea Tanzania. Vifo vya va wanawake kwa uzazi, takwimu zinaonyesha zimepungua kuliko kabla. Hiyo pekee tu inaonyesha kuwa something was done and continues to seriously being done. Sijui hizo takwimu zako ndugu zinatoka wapi. Ama ni just hearsay..Unavyoongea ni kama vile Lowassa akiingia madarakani we shall stop seeing these things. Usijidanganye ndugu, nia yake ni moja tu, kuendeleza ufisadi akiwa na mamlaka ya mwisho na hakutakuwa na wa kumstopisha.

7. Maisha yako juu kila mahali, na yatakuwa juu zaidi akija madarakani huyo fisadi..

You are being brainwashed, stop and think for a moment.. nina hakika maybe you are just too young to fully comprehend unachoongea.
 
Back
Top Bottom