Izato
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 5,387
- 11,564
Karamu ya kafara ya wachawi ni ibada tosha kwa Ibilisi, kwa kuwa ndiye mungu wa machukizo na maovu yao. Lakini kwa Mungu aliye hai na mwenye mamlaka na madaraka juu ya wote na vyote, kwa vyote vya haki na vitakatifu ndiyo vyenye kumpendezesha.Wapinzani wameweka mpira kwapani,wameogopa kishindo cha CCM sasa ni rasmi kila mtaa kwa sasa ni mali ya CCM,wasimamizi wengi nchi nzima wamewatangaza wana CCM kupita bila kupingwa baada ya tamko la pili la waziri Jafo.
Wapeni mihuri wateule waanze kazi ya kuwatumikia watanzania hadi 2024.
Tumeokoa mabilioni kwa kuepuka uchaguzi ,sasa mabilioni ya uchaguzi yaelekezwe kwenye maendeleo.
Mendeleo hayana chama.
Kwa dhuluma hii, CCM imepata laana, imevaa roho ya joka ya Farao na kuimeza ile haki na kuwagawia kwa hila wale wasiostahili. Laana ipi juu ya vichwa vyao wenyewe, na miongoni mwao Mungu atawatwalia Musa, ili kupitia kwake vifungo vya dhuluma vikapate kusitishwa. Roho ya mauti imeiukumba sasa CCM, na kwa hakika ndiyo inaelekea ktk shimo la kuzimu.
Tunakwenda kuliona neno hili la kiunabii likitimia juu yake; "MENE, MENE, TEKELI & PERESI"