CCM waondoeni hao wahuni walioteka chama chenu

ndiyo hata vyombo vya dola ni CCM au sehemu ya wahuni ndo maana hawataki kuinusuru nchi.
Katika tovuti ya www.katibampya.com kuna Rasimu ya katiba yenye muundo wa dola lenye mihimili minne ya kitaifa, Yaani.
1. Baraza la Usimamizi wa Taifa
2. Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania
3. Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania
4. Mahakama ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Muundo huu unafunga kabisa ufisadi, ubadhirifu wa mali za umma na vitendo vya kuvunjifu wa maadili ya taifa, aidha pia rasimu hiyo imeweka falsafa, mamlaka na mifumo ya sheria za kikatiba inayowezesha taifa kurudi kwenye umoja wake, mshikqmano, uwazi, ukweli na uwajibikaji wa pamoja.

Baraza la Usimamizi wa Taifa limetqmkwa katika SURA YA NNE ya katiba hiyo kuanzia ibara ya 98 mbaka ibara ya 116 na kufuatia mihimili mingineyo kama ilivyotamkwa hapo juu.

Neno langu la mwisho ni hivi shida si tu wahuni, shida mfumo wetu wa kikatiba Huna mianya mingi ya kusababisha wahuni wawepo,
#Tufunge mianya hiyo
 
wahuni hawataki katiba mpya.
 
wahuni hawataki katiba mpya.
Pigia kelele mbaka watataka tu, lakini swali linakuja je hipi unaitaka maana ni vizuri iwepo ndo useme hii naitaka na ndio maana naona pendekezo lililopo kwenye tovuti tajwa hapo juu linafaa.
 
Nani ndani ya genge la kimafia la CCM anayeweza kufanya hilo!??

Wakati Kolimba anasema CCM imepoteza dira, alikuwa na wasiwasi wa haya yanayotokea sasa.

Niliwahi muuliza Mzee P. Mangula juu ya "supremacy" mwenyekiti wa CCM kuja kuleta shida, akasema haiwezekani kwani mwenyekiti lazima atakuwa ni kada mwaminifu wa chama aliyekulia chamani hivyo hataweza kuwa "Mungu - mtu".

Leo hii, maCCM yameacha misingi ya chama na kukabidhi kila kitu (surrendered - all) kwa mwenyekiti.
Watu ni waoga kuhoji chochote kutoka kwa mwenyekiti zaidi ya kuwa washangiliaji, kisa ni kuogopa rungu (supremacy) la " mwenyekiti-rais"

Ni mCCM gani leo anaweza kuwa na guts kama za wale G55!!!??

Bila kutenganisha kofia ya uwenyekiti na urais (katiba mpya ya JMT ipige marufuku kwa rais kuwa mwenyekiti wa chama), basi maCCM yataendelea kuwa mateka na misukule ya mwenyekiti -rais as long as chama kimepora ushindi wa urais.
 
Unafikiri ni rahisi kiasi hicho! Wahuni siyo watu wa kuwaondoa kirahisi kwenye ulaji wao. Wako tayari kwa lolote ili tu kuilinda mirija yao ya wizi.
ungetoa na soluhisho sasa sio kusema sio rahisi
 
Mateka wenyewe wanafurahia kutekwa au we hujaona hilo, ni mabumbumbu hawaelewi lolote lile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…