CCM Wanusa harufu ya kushindwa uchaguzi

CCM Wanusa harufu ya kushindwa uchaguzi

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,756
Reaction score
2,646
Katika hali ya kubaini mambo magumu, CCM kupitia Serikali yake sasa imeanza kuvibana vyombo vya habari kuhakikisha vinaandika zaidi habari za Dr. Magufuli kuliko Lowassa. Hatua hiyo inakuja wakati tayari CCM ina vyombo vyake vinavyoipigia debe zikiwemo TV za TBC na Star TV na magazeti ya Uhuru, Daily news, Habari Leo, Jambo Leo na Raia Mwema/ Tanzania, bado inakerwa na vyombo Huru vya habari.
Hivi karibuni CCM wamemfukuza mwandishi wa habari wa Mwananvhi aliyeandika story ya Magufuli kuxomewa Mbeya na wana Chadema.
Hali hiyo inakuja baada ya kuona wanatumia fedha nyingi kwenye vyombo vya habari bila faida. Mahudhurio kwenye mikutano ya CCM ni hafifu ukilinganisha na ya mgombea wa Ukawa Edward Lowassa.
Baadhi ya wamiliki wa vyombo vya habari wanetishiwa kufungiwa wanapoonyesha au kuandika sana habari za Ukawa.
CCM wamekuwa wakisomba watu kwa malori tena wakiwalipa hela.
Kama hiyo haitoshi Vyombo vya serikali kama National statistics Bureau zinatumika kuonyesha uchumi unakua hata kama maisha ya Watanzania ni magumu. PPRA wao wameingia mkenge kutangaza ufisadi Tanroads sasa wanajisafisha.
CCM inatumia fedha na nguvu kubwa kumnadi Dr. Magufuli kiasi cha kuanza kutumia matusi na kejeli kwa Lowassa ili watu wamchukie, lakini ndio anazidi kupendwa.
Utafiti umeonyesha kada ya watu wa chini hasa mama ntilie, boda boda, wakulima na wafanyakazi wanaongoza kwa kumkubali Lowassa.
Juzi gazeti la Uhuru la CCM limedai eti Lowassa ametenga sh milioni 10 ili kuwahonga bodaboda baada ya kuona wameshindwa kuwashawishi.
 
kuna moderator humu hapendi kuona unaisema CCM! Subiri huu uzi wako utafutwa sasa hivi. Mods wacheni upendeleo kwa CCM munaposha maana halisi ya kuitwa great thinkers. wacheni wanaJF watoe maoni yao. Tumewakimbia kina Issa michuzi
 
Wasiwasi wangu ni jinsi mgombea wao anavyo zidi kuonyesha kutofahamu mambo mengi ya kawaisa kabisa! Ni jukumu letu tumkatae huyu mtu hasije akazulia machafuko mbele ya safari.
 
kuna moderator humu hapendi kuona unaisema CCM! Subiri huu uzi wako utafutwa sasa hivi. Mods wacheni upendeleo kwa CCM munaposha maana halisi ya kuitwa great thinkers. wacheni wanaJF watoe maoni yao. Tumewakimbia kina Issa michuzi
Tunavyo jua sisi Lowasa ana shinda uchaguzi na kuwa Raisi wa kwanza kutoka chama cha upinzani.dalili ziko wazi,unaweza kuziona mwenyewe.Yeye hasombi watu na wanajaa wenyewe lakini ili mkutano wa Magufuli ujae zinatumika pesa nyingi kusomba watu
 
Wameshindwa kutumia reference ya uchaguzi wa serikali za mitaa?

Walishindwa vibaya sana sema wakaficha vichwa kwenye mchanga.
 
Back
Top Bottom