Draft la playok online: Nahisi mkulima ni jini

Balqior

JF-Expert Member
Jun 8, 2021
1,709
5,699
Huyu jamaa hajulikani ni nani haswa, ana copy/kete zisizojulikana na finishing kali sana anafunga nazo watu, Ronaldo pale manyanya alisema mkulima anatumia dalmax ya kulipia ya tshs laki 3, hiyo software inauzwa wapi Google play?Mbona nlitafta sijaiona?

Mwenye account ya mkulima nasikia anaitwa amani sanga, draft kubwa alijulia wapi? wakati hajawahi shiriki mashindano ya kitaifa ya draft?

Kwenye chat, mkulima anawajua kina dogo ally, Shabaan Katoto, etc, wengine wanasema mkulima ni mzee mmoja wa ilala alikuwa ni bingwa wa draft zamani kidogo, sasa kama ni ivyo mbona anacheza copy zisizojulikana?

Mkulima anawafunga sisco na Ronaldo ambao ni mabingwa wa kitaifa wa draft na kuwapa masharti watafute sare Kwenye michezo 24..si mtu hatari huyo

Mwenye taarifa za ziada kuhusu mkulima atujuze
 
Mm huu mchezo ulishanishinda kitambo ...kukaa kufikiria kete gani nisukume huwa siwezi ila natamani sana kama ningeujua
 
Hawa jamaa waliotengeneza hii web ya play ok kwann wasingetengeneza app ikawa rahisi zaidi kucheza
 
Hawa Akina mkulima Ronaldo sijui Dogo Ally wanapatikana wapi???

Mnawapa sifa kupitiliza naomba Kama watakuwa tayari na Mimi nijipime uwezo nao.

Dar es salaam
Nenda pale Manyanya kijiwe cha dreva wa tx utakutana na hao mafundi. Ila sidhani kama utapata nafasi ya kucheza na kina ronaldo maana utapewa tu manjuka wa level yako na watakutoa kamasi
 
Nimeona unamsifia sana mkulima. Anacheza kwenye website gani? Nahitaji kucheza naye. Na anacheza ipi? American pool rules ambayo huku mnaita French au Tanzania rules ambayo mnaita British.
 
Back
Top Bottom