CCM wamhusisha Karume na Uamsho

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Na Julius Magodi na Habel Chidawali, Dodoma | Mwananchi | Novemba 15 2012


RAIS Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Aman Karume juzi usiku alizomewa na baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku wakimwita kwamba ni mmoja wa wanakundi la Uamsho.

Uamsho ni kundi ambalo katika siku za hivi karibuni limekuwa likihusishwa na vurugu ambazo zimekuwa zikitokea Tanzania Visiwani, ambazo zimesababisha watu kadhaa kukamatwa na kufikishwa mahakamani.

Rais Karume alikutana na zahama hiyo wakati akitoa hotuba ya kuwaaga wanaCCM baada ya kumaliza ngwe yake ya utumishi ndani ya chama hicho akiwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar.

Dalili za Rais Karume kuzomewa zilianza baada ya baadhi ya wajumbe kutoka Mkoa wa Mjini Magharibi kuanza kutaja neno ‘Uamsho' kila alipokuwa akizungumzia matatizo yaliyopo Zanzibar.

Hali ilikuwa mbaya zaidi pale alipokuwa akizungumzia vurugu za kidini ambazo ziliikumba Zanzibar hivi karibuni zikiongozwa na kikundi cha Uamsho.

Karume alisema kuwa kikundi cha Uamsho kina haki ya kutoa maoni yake kuhusu muungano, lakini hakipaswi kufanya vurugu kama ambavyo kimekuwa kikifanya.

Wakati akiendelea kuzungumzia suala hilo, kelele nyingi zilienea katoka kwa wajumbe wa mikoa ya Zanzibar ambao walikuwa wakipaza sauti, " Uamsho huyo….Uamsho huyo… Uamsho huyo…."

Hali hiyo ilimfanya wakati mwingine kukatiza hotuba yake na kulazimisha kuwatuliza watu hao kwa kusema "CCM oyeee….CCM…..oyeee…Mapinduziii…."

Hata hivyo, baada ya kelele hizo kuendelea Karume alionekana kuhamaki na kuwaambia wajumbe hao kwamba amechoka kusikia akiitwa jina hilo la Uamsho.

"Nimechoka kusikia naitwa jina hilo ati," alisema Karume na kuongeza:

"Hivi wengine wana vichwa vya samaki kwa nini mnapiga kelele wakati mimi ninapozungumza, si mniache nizungumze mambo ambayo ni muhimu zaidi kwa masilahi ya chama chetu."

Hata hivyo, licha ya kutafuta namna ya kuwatuliza wanachama hao kwa maneno mengi na historia ya maisha yake tangu alipojiunga na Chama cha ASP mwaka 1970, bado hakukuwa na utulivu na safari hii kelele zilianza kwa pande zote za wajumbe.

Kwa upande wa wajumbe wa Bara, baadhi yao walikuwa wakipiga kelele za kumtaka kumaliza hotuba yake ambayo walisema ilishachukua muda mrefu huku wakisema hakuna cha ajabu alichokuwa akizungumza.

Mara baada ya kumaliza hotuba yake, Karume alihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Redio Deutche Welle ya Ujerumani, na alisisitiza kuwa Uamsho wana haki ya kutoa maoni yao kuhusu muungano, lakini hawaruhusiwi kuvunja sheria.

Aliwataka wanachama wa kikundi hicho kujenga hoja, kwani alisema wengine wana hoja za msingi, lakini wasitumie vitisho.

Karume alistaafu uongozi wa CCM katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti (Tanzania Visiwani) na nafasi yake ilichukuliwa na Rais wa sasa wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein.

Tofauti na utamaduni ambao CCM kimeujenga kwa viongozi wake wakuu, Karume aliendelea kuwa makamu mwenyekiti hata baada ya kustaafu urais wa Zanzibar, hivyo kumlazimisha Dk Shein kusubiri hadi juzi kuchukua nafasi hiyo.

Kwa kawaida, viongozi wa ngazi ya Rais wa Muungano na Zanzibar, baada ya kuondoka katika nafasi zao za uongozi wa nchi, pia huachia madaraka ndani ya chama na kumwachia Rais mpya.

 
Duh, kwakuwa ni ya ndani ya CCM, watamalizana wenyewe, ingekuwa njee, ungesikia CDM hao
 
Masikini KARUME; labda ni UTAMU wa MADARAKA unajua alipaswa kuwa Msaidizi wa KIKWETE lakini BILAL sababu ya kuwa na NGUVU kwenye NEC ya Zanzibar --- Akawachanganya kichwa...
 
even his skin color tells it all..they remind me of Ku Klux Klan(KKK)burning down crosses,karume and his fellow thugs burn down churches
 
Masikini KARUME; labda ni UTAMU wa MADARAKA unajua alipaswa kuwa Msaidizi wa KIKWETE lakini BILAL sababu ya kuwa na NGUVU kwenye NEC ya Zanzibar --- Akawachanganya kichwa...
Nkuu nngu007, hakuna wa kumhurumia Karume.
Kalikoroga mwenyewe, kajiunga na uamsho bila kuwashirikisha viongozi wenzake Zanzibar na Bara.
Hata makubaliano yake na Sharrif Hamad ni kazi binafsi ya kwake.

Tunaishukuru JK na CCM kwa kumvumilia mpaka sasa.
Lakini sasa it was sweet revenge na hakuna aliyemuokoa katika mkutano mkuu wa CCM. Kila mtu kamruka, na sasa anaitetea uamsho kama hana akili nzuri.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Nkuu nngu007, hakuna wa kumhurumia Karume.
Kalikoroga mwenyewe, kajiunga na uamsho bila kuwashirikisha viongozi wenzake Zanzibar na Bara.
Hata makubaliano yake na Sharrif Hamad ni kazi binafsi ya kwake.

Tunaishukuru JK na CCM kwa kumvumilia mpaka sasa.
Lakini sasa it was sweet revenge na hakuna aliyemuokoa katika mkutano mkuu wa CCM. Kila mtu kamruka, na sasa anaitetea uamsho kama hana akili nzuri.

Lakini ya yeye na Sharrif Hamad ni pia MSUKUMO toka WESTERN EUROPE... CCM-Zanzibar isingifanya hivyo SERIKALI NZIMA ya TANZANIA wasinge pata MISAADA...

Kwahiyo ILIKUWA NI LAZIMA....
 
Mkuu nng007
Karume ni uamsho mtupu amemtumia sana shemeji Mansoor Himid kuleta vurugu ndania ya chama; Dr. Shein hakuwa na jinsi na alitumia madaraka yake kumuondoa Himid kwenye uwaziri; tamaa yake ya madaraka imemponza; aling`ang`ania madaraka ya umakamu kwa kuwakingia kifua uamsho; tunamuomba ajondoe kabisa kwenye ajiunge na uamsho rasmi!

Chama
Gongo la mboto DSM
 

Lakini ya yeye na Sharrif Hamad ni pia MSUKUMO toka WESTERN EUROPE... CCM-Zanzibar isingifanya hivyo SERIKALI NZIMA ya TANZANIA wasinge pata MISAADA...

Kwahiyo ILIKUWA NI LAZIMA....

Ndio maana imedhihirika kuwa ile mapatano kati yake na Sharrif ilikuwa one -man-show, na hakuwashirikisha CCM-Zanzibar wala Bara.
Hilo likawapa kichwa kina Sharrif kufikiri wanaweza kuazisha movement yao ya Uamsho yenye malengo ya kisiasa.
Leo Karume anaanikwa hadharani na kukanwa na uamsho yake, huku viongozi wa Uamsho wakisota sello kwa kufanya mambo ya kuhuni.

Uhuni uliofanywa na Uamsho unaweza kuwa traced back to Karume.
 
Let Zanzibar come to its senses, na mambo ya Zanzibar yaamuliwe na watu ambao ni sober. Karume is not sober.
 
Uamsho huyoooo.... Aibu sana kwake, familia yake, na chama chake
 
Masikini KARUME; labda ni UTAMU wa MADARAKA unajua alipaswa kuwa Msaidizi wa KIKWETE lakini BILAL sababu ya kuwa na NGUVU kwenye NEC ya Zanzibar --- Akawachanganya kichwa...

Asubiri 2015 awe mgombea Mwenza wa Lowassa iwapo bid ya Membe na Nahodha itagonga mwamba!
 
Inafaa wamwajibishe! Kwanza ana jazba sana, nilimwona mwaka juzi ktk TV yeye na binti yake wakigombea mpaka wa kiwanja na kanisa la anglican zanzibar. Hana busara
 
Haya anayofanya yatamgharimu yy na kizazi chake, hata hao Uhamsho wakifanikiwa malengo yao yy na wote wenye asili ya bara watasakamwa waondoke, hatakuwa na amani ataitwa mlowezi.
 
hata mungu hua humsamehe mtu anapojua na kurekebisha makosa yake kabla ya kufa. Big up simba mtoto, waache wazomeee, lakini bila wewe leo wangekua wanaendelea kuuliwa kama vibua.
 
Jamani mbona CCM wanavichwa vibovu? Wanalazimisha sera yao mbovu ikubalike ya serikali 2, kwa sasa watu weng wameelimika wanajua kuchambua mambo wanache fikira za Nyerere wakati wake yeye alikuwa ndo msomi miongoni wa wajinga wengi, ila sasa dunia imebadilika. Ndugu za wanaCCM hiyo sera yenu imepitwa na wakati na katu hamuwezi kubadilisha maamuzi ya wananchi. Angalizo> Msipoangalia mtasababisha vurugu kwa znz kwa ustahamilivu wenu kuwa mdogo.
 
Back
Top Bottom