mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,286
- 6,727
Kuna tofauti kati ya Nchi, Serikali na Chama cha Siasa. Nikurejeshe wewe na wenye mawazo kama yako kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT), 1977 na Sheria husika.Sijui kisheria hili limekaaje, lakini nanusa conflict of interest. Ingawaje ccm ipo pande mbili, kitakiba, Zanzibar na Tanganyika ni nchi mbili tofauti..inawakuwaje Raisi wa Tanganyika (ingawaje pia ni wa muungano) kusimamia mambo ya Nchi ya zanzibar ili hali Raisi wa Zanzibar amejikalia tu kama kibogoyo... mambo gani haya? Tanganyika ni kweli wanathamini muungano, lakini hili la kusimamia uchaguzi wa ccm ya zanzibar, nchi ya zanzibar, serikali ya wazanzibar na uraisi wa zanzibar, tafadhari waacheni wapumue kwa kweli.. mumewakalia sana kooni sana..
Ibara1: Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano.
Ibara ya 3(1) Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa.
Ibara ya 4(1) Shughuli zote za Mamlaka ya Nchi katika Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kudhibitiwa na vyombo viwili vyenye mamlaka ya utendaji, ...
(2) Vyombo vyenye mamlaka ya utendaji vitakuwa ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ...
Ibara ya 33(1) Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano
Ibara ya 39(1) Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa
Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama:
(c) ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;
Ibara ya 103(1) Kutakuwa na Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambaye ndiye atakuwa Rais wa Zanzibar na Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na vile vile Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar.
Sheria Ya Uchaguzi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (Na 4, 2018), Ibara ya 43 Kwa kuzingatia masharti ya Katiba, mtu atakuwa na sifa ya kuteuliwa kuwa Mgombea wa Urais iwapo:
(d) ni mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa ambacho kimesajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa.