mwanamakambako
JF-Expert Member
- Jan 3, 2014
- 780
- 120
Ccm kule kalenga wameangukia pua kabla ya uchaguzi, niliishatoa tahadhari mapema kabisa kuwa, wanakalenga wamemkubali mgombea wa Chadema vilivyo, cha kufanya makamanda waweke ulinzi imara dhi ya wizi wa kura, pili wanatakiwa wacheze na mbinu chafu zinazopangwa na ccm vyumbani mwao, maana kama ni kampeni tayari wameshindwa na wameuona upepo, kuwa Chadema haikamatiki, nashukuru makamanda wamefanya kazi nzuri sana, na kubaini mbinu chafu ya ccm wakishirikiana na tume, wameongeza wapiga kura kinyemera bila Chadema kuhusishwa, na tume inadai itatumia daftari la mwaka huu, wakati walikataa kuliboresha, ccm kwisha habari yake.