CCM walishana yamini Dodoma

Hahahaa ameanza mazoezi ya peoples power inabidi aanze na alama hii ya V ile ya ngumi ameshaizoea.
Ni kweli ile ya ngumi imezoeleka mpaka wananchi wameanza kuitafsiri vibaya

attachment.php
 
maana ya kulishwa yamini na maelezo ulotoa no correlation ndugu.
Hili ni jukwaa la siasa sio lugha, ukitaka maswala ya lugha nenda kwenye jukwaa la lugha, hapa chukua ujumbe kama unafanyia kazi poa au kama unapotezea kivyako....!
 
Wabunge wa CCM waliomaliza kikao cha bunge hapo jana wamezuiliwa kuondoka na leo kutwa nzima wamekuwa kwenye kikao cha Wabunge wote wa CCM kuangalia jinsi gani wanavyoweza kudhibitiana kutokana na hoja iliyofikishwa kwa Spika juu ya kumwondoa madarakani Waziri Mkuu kwa kura ya kutokuwa na imani nae hasa ingizingatiwa kwamba kura yenyewe itakuwa ni ya Siri.
Tusubiri tuone kitakachojiri Ngoma bado nzito na Inogile.

Wasiwasi wangu ni kuwa, Mama mlinzi wa kanuni asijegeuza kanuni akasema inatakiwa iwe kura ya wazi. maana kila mara anapindua kanuni halafu CDM wakisusa MAGAMBA na mke wake KAFU wanabaki kuendelea kupiga kura na azimio linapita kimagumashi hivyo hivyo.
 
watakulaje amini na kitu ambacho hawajui
tambiko lake, wanajidanganya tu hao.
 
Mhh, kwani wako kwenye mechi ya Yanga na Simba ambako usaliti ni lazima ulishwe yamini?
 
Kama alivyo mwanadamu yeyote, ukifika wakati wa kufa hata ukikimbilia wapi kufa utakufa tu. CCM nayo imefikia katika wakati kama huo, wawafukuze mawaziri au wasiwafukuze kufa ni lazima watakufa tu, wapige kura ya kutokuwa na imani na serikali au wasipige kufa watakufa tu,watumie mahakama au vyombo vya dola kufa watakufa tu. Hapa tulikofika ni kutamu kupita maelezo, kwani hawatoki kwa namna yeyote. Kubwa ni kila mtz mzalendo wa kweli ku-play part kwenye M4C, kwa namna yeyote mf.michango ya fedha, kuzungunza na mtu mmoja mmoja juu ya umuhimu wa mabadiliko sasa,mitandao ya jamii kuelimisha umma n.k.
 
usiogope hata wakilishana na kuchanjiana damu. Muda wa M4C umefikia na sauti ya wanyonge imeshafika masikioni mwa Mungu. Lazima wang'oke iwe leo au kesho
 
nadhani suala ni serikali kuzuia ujio wa hiyo kura kwa kuwawajibisha waliotuhumiwa na kuchukua hatua za kisheri zaidi dhidi yao. hapo watakuwa wamepata kura za wabunge wa ccm dhidi ya hoja. lkn kama hali itabaki kuwa kama ilivyo, kisha wabunge walazimishwe kuuiunga mkono serikali, ni uzandiki wa hali ya juu
 
Namshukuru sana mungu kwa haya yanayoendelea kujiri kwani mkanganyiko unaendelea na kauli zinazidi kudhihirisha ule msemo wa chukua chako mapema, na kwa wanaopingana na kura yenyewe ya kwamba wanaendelea kusubiri zamu yao ya kuchota ifike na itafikaje bila kuonesha ya kuwa unaitetea serikali ya chama chetu!?
kweli mwisho unaelekea kutimia i had a dream.Thanks Lord.
 
maana ya kulishwa yamini na maelezo ulotoa no correlation ndugu.

Mnafiki ni mnafiki tu, kwa wabunge wa CCM haina haja hata ya kula Yamini, yanaburuzwa kama ng'ombe. Hivi nyie wabunge CCM hamuwezi kusimamia ujasiri wenu? aibu tpuuuuuuuuuu! bora ya John Cheyo alietamka "nikikosa mimi basi chagueni CCM"
 
Hapo sawa,ila mpaka cdm waingie raslimali za Taifa itakuwa vipi. Maana tunashudia kwa macho yetu.Faru waliokuwa wengi Tanzania wakaunzwa Kwa Kaburu Sasa tunanunua kwao kwa bei kubwa sana.
 
Bila shaka msimamizi wa zoezi hilo ni yule mganga wao Maji Marefu. CCM kwa uwanga na uchawi bana.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom