CCM walimfanyia unyama Baba yangu mzazi

CCM walimfanyia unyama Baba yangu mzazi

Deogratius Kisandu ninavyojua mimi watakutreat kama walivyomtreat mzee wako bila kujali wewe ni msomi au la .hiyo ndio siasa huwezi kufanya kinyume chake kauli ya kuwa umesoma nakushauri upitie dirishani uwe upande wa pili utakuwa na ahueni ,ukiwa bado upo ndani taswira ya baba yako itakutesa hadi utajuta soma hapo juu Mchambuzi
 
nimecheka sana hapo kwenye aya ya tano duh!
hahahahaahahahahahahaha
 
JINSI CCM WALIVYO MTENDA MABAYA BABA YANGU.

Baada ya marehemu Mbunge Khanga wa jimbo la Kahama kuingia kwenye kesi ya kuibiwa gari la SERIKALI na skendo zingine, alivuliwa ubunge. Mzee wangu Nalimi Kisandu alichukua Fomu ya kugombea Ubunge kipindi hicho jimbo la Kahama.

Mzee walimuwekea vikwazo sana na upinzani sana, walifanya kila mbinu na kumuahidi kumtafutia nafasi nyingine ndani ya CCM akiwemo aliyekuwa mbunge jimbo la Msalala Ndg. Manyambonde. Walimshawishi sana.

Nakumbuka siku anatuambia alikuwa akilaumu sana "CCM wananionea kwa kuwa Mimi sija soma, ngoja nitengeneze kiboko yao hata wakiniua Mungu atakuja kujizihirisha kwa wanangu"

Walichokifanya Viongozi wa CCM mkoa wa Shinyanga ni kumshawishi aoe mwanamke ambaye ni kiongozi ndani ya CCM, mzee aliwakatalia sana, wakamwambia lah sivyo hutapata Ubunge. Ndipo rafiki yake MWL. Said Mselemu alipomshauri aoe tu.

Basi Mzee akapewa Mke ambaye ni Katibu wa CCM wilaya ya Kahama, Ndg Rose Mwesiga akawa mke na mama yetu wa kufikia. Na hapo ndio ukawa mwisho wa safari yake ya harakati za kisiasa. "Wewe Kisandu tumekupa mke Ubunge wa nini tena?" Kauli hiyo ilimkera mzee, ilikuwa ikitolewa na wapambe wa CCM.

Na hata alipotaka kuhamia Chama cha NCCR-Mageuzi kuwafata kina Ndg. Makongoro walimpiga mkwara kisa wamempa mke. Kitendo cha Mzee kuishia Darasa la sita kilimfanya aone manyanyaso sana ndani ya CCM. Nakuamua kuachana na Udj wa kuwasaidia CCM kwenye Kampeni zao.

Nakumbuka ilifikia hatua alikuwa anasema bora ninge baki Arusha labda wasingefanya hizi fitina.

Hayo ni ya Mzazi wangu, Leo Mimi mtoto wake Deogratius wanania adhiri vilevile, huku wakisema Deo mpaka akizile chama au ajinyonge, lakini Mimi nimesoma, nitawakomesha hasa.

R.I.P Nalimi Kisandu.

Deogratius .N. Kisandu
6 Januari 2017
Kisandu hamia CHADEMA ndugu kuna waungwana na wasomi wenzako. kwa akili na usomi wako utsaidiana na makamanda kina sumaye na Lowasa kuleta mabadiliko
 
CCM siyo ya ki-sport sport, kumbe unaweza ukapewa mpaka mke, lumumba street moja, faster.
Unasikiliza porojo za huyu mleta mada!!!
Kisandu pole na ulaghai wa marehemu baba yako.Zamani tukiwa wadogo tulikuwa tunalaghaiwa mama akizaa ukiuliza mtoto katoka wapi wanasema kameokotwa!!!

Baba yako akataka kujiolea dogo dogo kuwazuga wewe na mama yako akaona awalaghai kuwa CCM ndio inamlazimisha kuoa ;HA HA HA HA
Yaani wewe na mama yako mkaamini hayo maneno!!! Na usomi wako unaosema unao bado waweza amini story kama hizo? Hiyo ilikuwa gia tu ya mzee kuvuta kasichana kadogo ndani kuwazugeni tu
 
Msaliti dawa yake ni usaliti!!!
Kwa hiyo baba yako alimsaliti mama yako (mke wa ujana wake) akaoa mke mwingine kwa sababu alitaka ubunge kupitia CCM?
CCM nayo ilifanya vema kumsaliti kwa kumnyima hiyo nafasi ya ubunge.
 
Pole Deo ila kuna kazi nyingi za kufanya sio siasa tu, kwa ubunge ni ufalme. Kabla hujavua nguo hadharani tafadhali muone

Psychiatric aliye karibu akusadie.
 
Mkuu kama umesoma nakushauri uachane na siasa kwani utakuja kujuta.
Elimu yako unaweza kuitumia kwa namna nyingine katika kuisaidia jamii na siyo lazimam iwe ni siasa.

Ni ushauri tu unaweza kuuchukua au kuachana nao.

Soma mistari yake ya sentesi! Labda aendeleze udj wa Baba yake R>I>P mzee wake. Lakini mambo ya eti anaelimu na maandishi/andishi leneywe kama hilo na yale mengineyo tuliyoyasoma ni heri akajiongezea jitihadaa kuwa DJ wa kukodiwa kwenye majukwaa ya siasa kwakuanzisha Bendi maalumu ya kusubiri Kampeni za Uchaguzi.
 
JINSI CCM WALIVYO MTENDA MABAYA BABA YANGU.

Baada ya marehemu Mbunge Khanga wa jimbo la Kahama kuingia kwenye kesi ya kuibiwa gari la SERIKALI na skendo zingine, alivuliwa ubunge. Mzee wangu Nalimi Kisandu alichukua Fomu ya kugombea Ubunge kipindi hicho jimbo la Kahama.

Mzee walimuwekea vikwazo sana na upinzani sana, walifanya kila mbinu na kumuahidi kumtafutia nafasi nyingine ndani ya CCM akiwemo aliyekuwa mbunge jimbo la Msalala Ndg. Manyambonde. Walimshawishi sana.

Nakumbuka siku anatuambia alikuwa akilaumu sana "CCM wananionea kwa kuwa Mimi sija soma, ngoja nitengeneze kiboko yao hata wakiniua Mungu atakuja kujizihirisha kwa wanangu"

Walichokifanya Viongozi wa CCM mkoa wa Shinyanga ni kumshawishi aoe mwanamke ambaye ni kiongozi ndani ya CCM, mzee aliwakatalia sana, wakamwambia lah sivyo hutapata Ubunge. Ndipo rafiki yake MWL. Said Mselemu alipomshauri aoe tu.

Basi Mzee akapewa Mke ambaye ni Katibu wa CCM wilaya ya Kahama, Ndg Rose Mwesiga akawa mke na mama yetu wa kufikia. Na hapo ndio ukawa mwisho wa safari yake ya harakati za kisiasa. "Wewe Kisandu tumekupa mke Ubunge wa nini tena?" Kauli hiyo ilimkera mzee, ilikuwa ikitolewa na wapambe wa CCM.

Na hata alipotaka kuhamia Chama cha NCCR-Mageuzi kuwafata kina Ndg. Makongoro walimpiga mkwara kisa wamempa mke. Kitendo cha Mzee kuishia Darasa la sita kilimfanya aone manyanyaso sana ndani ya CCM. Nakuamua kuachana na Udj wa kuwasaidia CCM kwenye Kampeni zao.

Nakumbuka ilifikia hatua alikuwa anasema bora ninge baki Arusha labda wasingefanya hizi fitina.

Hayo ni ya Mzazi wangu, Leo Mimi mtoto wake Deogratius wanania adhiri vilevile, huku wakisema Deo mpaka akizile chama au ajinyonge, lakini Mimi nimesoma, nitawakomesha hasa.

R.I.P Nalimi Kisandu.

Deogratius .N. Kisandu
6 Januari 2017
Mambo binafsi unatuletea huku unataka sisi tuvunje ndoa au,mtu alipewa mke badala ya kushukuru wewe unalaumu na mbona hukulaumu wakti wote huo ,unachokifanya ni kuwadharirisha wazazi wako,unapoongea uwe na akiba ya maneno usiwe kama mwehu.
 
The moment aimeingia kwenye siasa alipaswa afahamu kuwa hilo jukwaa ni "man eat man society! Kwenye siasa, kuna unyama zaidi ya kurubuniwa...mzee alirubuniwa,
 
Unasikiliza porojo za huyu mleta mada!!!
Kisandu pole na ulaghai wa marehemu baba yako.Zamani tukiwa wadogo tulikuwa tunalaghaiwa mama akizaa ukiuliza mtoto katoka wapi wanasema kameokotwa!!!

Baba yako akataka kujiolea dogo dogo kuwazuga wewe na mama yako akaona awalaghai kuwa CCM ndio inamlazimisha kuoa ;HA HA HA HA
Yaani wewe na mama yako mkaamini hayo maneno!!! Na usomi wako unaosema unao bado waweza amini story kama hizo? Hiyo ilikuwa gia tu ya mzee kuvuta kasichana kadogo ndani kuwazugeni tu

I was there, I knew the truth.
 
Back
Top Bottom