Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,103
- 43,348
Kama pamoja na nguvu kubwa inayotumika kuwatisha wananchi bado wananchi wanatoka kila kukicha maana yake ni kuwa risasi hazijawavunja mioyo.
Nakumbuka maneno ya mwandamanaji mmoja miaka ile kule Morogoro..
"Polisi wanajifunza kuua na sisi tunajifunza kufa". Watanzania sasa wamehitimu.
Hawawezi kutawaliwa tena kibabe...hawawezi kufanyiwa kibabe...kuendelea kuchelewa ni kuendelea kuongeza gharama ya ujenzi mpya wa Taifa. Kwa kadiri siku zinavyoenda ndivyo mamilioni ya Watanzania wanazidi kuungana na watoto wao.
Wito wangu naurudia. POLISI wekeni silaha chini, Tume ya Uchaguzi isilazimishe kumrudisha Samia (atawatawala maiti sasa na atawatazamaje tena Watanzania) na Jeshi lisipuuzie sauti za hiki kizazi.
Historia inaandikwa na viongozi wote wajue na kuchagua wanataka waandikwe upande upi wa historia.