Uchaguzi 2020 CCM wakirudisha majina haya nitaamini kweli Chama hakina Vyombo vya Uchunguzi

Kadoda nguku

JF-Expert Member
Apr 22, 2019
332
475
Katika harakati za upatikanaji wa wabunge na madiwani wapo wagombea walio cheza rafu za wazi kabisa, yaani huhitaji hata VAR ili kujiridhisha na rafu za baadhi ya wagombea.

Wapo wagombea wengi walioshika namba 1 hadi 5 wanahitaji umakini zaidi katika kuwateua, hao ndio walipiga wenzao buti za kufa mtu

Kama vyombo vya uchunguzi vitafanya kazi zao kwa weledi hakika chaguzi zijazo za ndani ya chama hakutakuwa na punje ya Rushwa, lakini vyombo hivyo vya uchunguzi kama havikufanya kazi yake kwa umakini rushwa ndani ya CCM haiwezi kwisha

Njia pekee ni kuimarisha Vyombo vya Uchunguzi ndani ya chama, hii itasaidia kuondoa rushwa ndani ya chama.
Wako wagombea ambao waliwanunua viongozi wa chama wilaya na Mkoa, TAKUKURU na wafanyakazi wa ofisi ya usalama wilaya ili wawabebe.

Vitendo kama hivyo vimewafanya wanachama kusubiri maamuzi ya vikao vya juu ili kuona kama kweli yanayosemwa na viongozi wa juu wa chama yatatekelezwa.

Siwezi weka hapa majina hayo ya walioshinda na wasioshinda ambao walifanya madudu, ila kama members watataka nitaweka na madudu yao. Au kama wapo members wengine wanaofahamu madudu yaliyofanyika unaweza weka mgombea na madudu yake, kwa sababu JF ni jukwaa la wazi. Na hii itasaidia hata chama katika kufanya maamuzi.
 
Wapo wagombea wengi walioshika namba 1hadi 5 wanahitaji umakini zaidi katika kuwateua, hao ndio walipiga wenzao buti za kufa mtu
Rushwa ndani ya CCM ni kama damu ndani ya mwili wa binadamu
 
Katika harakati za upatikanaji wa wabunge na madiwani wapo wagombea walio cheza rafu za wazi kabisa, yaani huhitaji hata VAR ili kujiridhisha na rafu za baadhi ya wagombea.

Wapo wagombea wengi walioshika namba 1hadi 5 wanahitaji umakini zaidi katika kuwateua, hao ndio walipiga wenzao buti za kufa mtu
Ww utakuwa unawapigia chapuo akina Steve nyerere , Lijualikali , mashinji , Joshua Nasary , Tumbiri , na meya wa arusha
 
Wapeni watu mtu waliyemtaka. Unaweza toa rushwa na usichaguliwe. Unaweza toa rushwa na tayari watu wanakuamini so kutoa rushwa hakuna uhusiano na ushindi wako as watu walikukubali tangu mwanzo.

Azan katika uchaguzi wa 2015 jimbo la Kinondoni hakua anakubalika ndani ya CCM ya Kinondoni ila alipita kwa kuletwa na KK. Kilichofuata ni bwana Mtulia kujitwalia jimbo kizembe as wapiga kura walimuopt waliyemtaka (regardless katoa rushwa ama la) kisha KK ikaona hapana aje huyu huku.

Na siasa ni nini? Intro to Politics inasema siasa ni nani amepata mamlaka kivipi na kwa njia gani. Deep down katika siasa unatarajiwa kushawishi hata kwa rushwa. Ugiriki ya kale wagombea wa majimbo walikua wakiwalipia viingilio wapiga kura kuangalia mapambano ya gladiators.

Na hiyo ndiyo ilikua rushwa common.
 
Kuwarudisha wagombea kama akina Mrisho Gambo, Manyanya, Ngonyani ,Mapunda, Kapinga, Mwanjelwa, Masele, n.k ambao makatibu wao walishakamatwa na kukutwa na fedha za kuhonga wapiga kura ,unahitaji uthibitisho gani hapo, haiihitaji hata Huyo mchunguzi afike form four ili aweze kubaini
Shida yako nini hapo-Uchaguzi Mkuu upo na hapo ni siasa na sera.
Hayo ya Rushwa Sijui nini hayana maana kwa sb uchaguzi Mkuu huwezi honga wapiga kura wote!!!
 
Jimbo la Kawe Saa mbili asubuhi linaenda kwa Mdee!! Mpwa Mtoto wa dada hakuna anayemjua hata kura hajaomba , Mandingo Mcheza Porno mtaji wake wa waamini sio wapiga kura ukija kwa yule mama anamjua mdee vizuri 2010 alikula za uso saa mbili tu asubuhi kwahiyo hana jipya.
 
Kuwarudisha wagombea kama akina Mrisho Gambo, Manyanya, Ngonyani ,Mapunda, Kapinga, Mwanjelwa, Masele, n.k ambao makatibu wao walishakamatwa na kukutwa na fedha za kuhonga wapiga kura ,unahitaji uthibitisho gani hapo, haiihitaji hata Huyo mchunguzi afike form four ili aweze kubaini

Hivi ni nani msafi Ccm atae mnyooshea mwenzake kidole? Kuanzia kwa mwenye kiti wao hadi mjumbe? Polepole huyu anae piga kelele leo, yeye nafasi aliyopo kahongwa, kumbuka akiwa mwana harakati aliwahi kutamka kwa kinywa chake kwamba, kama uchaguzi ukiwa huru na wa haki Ccm haipo. Leo atuambie Ccm imepata wapi usafi wa kuongoza nchi?

Mwenyekiti wao kawagawa Watanzania, kuna wakubeba mgongoni na kuwa wa kuvuta mikokoteni.. Bado Ccm wana sema wanawajali Watanzania. Leo watajisifu kupeleka maendeleo kwa Watanzania. Kumbukeni maneno ya Mh. Kikwete, hivi vitu viliandaliwa na watangulizi wake. Yeye hajafanya chochote.. Amkeni
 
Jimbo la Kawe Saa mbili asubuhi linaenda kwa Mdee!! Mpwa Mtoto wa dada hakuna anayemjua hata kura hajaomba , Mandingo Mcheza Porno mtaji wake wa waamini sio wapiga kura ukija kwa yule mama anamjua mdee vizuri 2010 alikula za uso saa mbili tu asubuhi kwahiyo hana jipya.
Kwa ushindi wa masika mpwa mtoto wa dada haoni ndani. Lakini kwa ushindi wa NEC atakua Waziri
 
Kuwarudisha wagombea kama akina Mrisho Gambo, Manyanya, Ngonyani ,Mapunda, Kapinga, Mwanjelwa, Masele, n.k ambao makatibu wao walishakamatwa na kukutwa na fedha za kuhonga wapiga kura ,unahitaji uthibitisho gani hapo, haiihitaji hata Huyo mchunguzi afike form four ili aweze kubaini
umemwacha Silinde nasikia alishirikiana na dc kusambaza love usiku!
 
Ni mtoto wa dada kule Chato na tulimlea wenyewe Oyster Bay tukiwa Mawaziri wa Mkapa.
Eeeeeeeh kumbe ndio maana kaonyesha na dharau hata kuomba kura hamna?
Sasa kama kuna connection kubwa hii mbona watu wanaanza kusema atakatwa sijui apewe nani coz katoa rushwa. Hao watakaomkata wanaanzia wapi sasa. Wana guts hizo?!
 
Wapeni watu mtu waliyemtaka. Unaweza toa rushwa na usichaguliwe. Unaweza toa rushwa na tayari watu wanakuamini so kutoa rushwa hakuna uhusiano na ushindi wako as watu walikukubali tangu mwanzo.

Azan katika uchaguzi wa 2015 jimbo la Kinondoni hakua anakubalika ndani ya CCM ya Kinondoni ila alipita kwa kuletwa na KK. Kilichofuata ni bwana Mtulia kujitwalia jimbo kizembe as wapiga kura walimuopt waliyemtaka (regardless katoa rushwa ama la) kisha KK ikaona hapana aje huyu huku.

Na siasa ni nini? Intro to Politics inasema siasa ni nani amepata mamlaka kivipi na kwa njia gani. Deep down katika siasa unatarajiwa kushawishi hata kwa rushwa. Ugiriki ya kale wagombea wa majimbo walikua wakiwalipia viingilio wapiga kura kuangalia mapambano ya gladiators.

Na hiyo ndiyo ilikua rushwa common.
Na azan huyuhuy katupwa tena uchaguzi huu kwenye kura za maoni amepita tarimba wampitishe azan kuwa mgombea waone jimbo linarudi tena upinzani
 
Kinondoni bado ni ya upinzani hata wamlete huyo Tarimba hawawezi ambulia kitu
 
Katika harakati za upatikanaji wa wabunge na madiwani wapo wagombea walio cheza rafu za wazi kabisa, yaani huhitaji hata VAR ili kujiridhisha na rafu za baadhi ya wagombea.

Wapo wagombea wengi walioshika namba 1 hadi 5 wanahitaji umakini zaidi katika kuwateua, hao ndio walipiga wenzao buti za kufa mtu

Kama vyombo vya uchunguzi vitafanya kazi zao kwa weledi hakika chaguzi zijazo za ndani ya chama hakutakuwa na punje ya Rushwa, lakini vyombo hivyo vya uchunguzi kama havikufanya kazi yake kwa umakini rushwa ndani ya CCM haiwezi kwisha

Njia pekee ni kuimarisha Vyombo vya Uchunguzi ndani ya chama, hii itasaidia kuondoa rushwa ndani ya chama.
Wako wagombea ambao waliwanunua viongozi wa chama wilaya na Mkoa, TAKUKURU na wafanyakazi wa ofisi ya usalama wilaya ili wawabebe.

Vitendo kama hivyo vimewafanya wanachama kusubiri maamuzi ya vikao vya juu ili kuona kama kweli yanayosemwa na viongozi wa juu wa chama yatatekelezwa.

Siwezi weka hapa majina hayo ya walioshinda na wasioshinda ambao walifanya madudu, ila kama members watataka nitaweka na madudu yao. Au kama wapo members wengine wanaofahamu madudu yaliyofanyika unaweza weka mgombea na madudu yake, kwa sababu JF ni jukwaa la wazi. Na hii itasaidia hata chama katika kufanya maamuzi.
Nafikiri muhimu sana ni kwa CCM kurudisha majina yanayokubalika kwa wananchi....
 
Back
Top Bottom