JokaKuu,Buchanan,
..huku Tanganyika chochote kile ambacho CCM wataamua ndicho kitakachokuwa.
..ila tatizo kubwa liko Zanzibar. sijui ni vipi, na ni nani, atayewashawishi wa-Znz waachane na jitihada zao za kuwa na mamlaka kamili.
..hoja kwamba hakuna anayeijua Tanganyika nadhani haina mashiko kwasababu hata hii Tanzania hakuna aliyekuwa akiijua wakati inaasisiwa mwaka 1964.
..pia Tanzania ni zao la Zanzibar na Tanganyika. wa-Zanzibari wanaelekea "kusepa" toka ktk Tanzania, sasa katika mazingira hayo sijui unataka wa-Tanganyika wafanye nini.
NB:
..umeambiwa Waziri Mkuu Pinda haendi Znz kukagua shughuli za maendeleo.
..mimi nadhani "dongo" hilo amerushiwa hata Raisi Kikwete. Lini mmemsikia akifanya ziara za kikazi Zanzibar, au hata kukagua uhai wa chama?
cc Kasheshe, Lizaboni, chama, NasDaz, Barubaru, gombesugu, Pasco, Nguruvi3
Haya maneno kwamba PM hana mamlaka ZNZ ni maneno tu ya kukuza mambo; kwa mujibu wa Katiba yetu, Ibara ya 52 (1) inasema: Waziri Mkuu atakuwa na madaraka juu ya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa siku hata siku wa kazi na shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Hii kutokwenda kwenda ZNZ kufanya shughuli za serikali ni matumizi tu ya busara ambayo mungu amemjaalia mwanadamu! Ikiwa ZNZ leo hii kuna Makamu wawili wa Rais, kuna sababu gani PM awe anaenda huko kukagua miradi wakati huko nako kuna viongozi? Hata hivyo, wala si kwamba haendi kabisa, pitia picha hii hapa chini:


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kiweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Jendelecheju- Kaebona na Koani- Jumbi mkoa wa Kusini Unguja Desemba 17, 2013.
Kuna hizi hapa:

MKE wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akivuna mpunga katika bonde la Cheju, mkoa wa Kusini Unguja.

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda na mke wake, Tunu Pinda wakivuna Mpunga katika bonde la Cheju, mkoa wa Kusini Unguja, juzi. Katikati ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira wa Zanzibar, Burhani Saadat.

Hizo picha tatu hapo juu ilikuwa kipindi cha Karume wakati hiyo ya kwanza ni kipindi cha Shein. Kwahiyo labda hoja iwe PM haendi ZNZ mara kwa mara...ingawaje wengine watajiuliza kuna umuhimu gani kwa taifa ikiwa ataenda mara kwa mara ikiwa ZNZ nayo ina viongozi wake!
Tukirudi hoja yako ya ni namna gani utafanya hadi wa-ZNZ wa-forgo mamlaka yao; nakubaliana na wewe! It's almost to IMPOSSIBLE! ZNZ, linapokuja suala la mamlaka yao, mara zote wapo pamoja katika hilo!
Last edited by a moderator: