pixel
JF-Expert Member
- Jun 22, 2012
- 1,630
- 406
Nitashangaa sana iwapo Rais atakuja kumjibu hoja za Warioba badala ya kufungua bunge lenye hoja mbili zenye tofauti kimtazamo.Rais ni Rais wa wote waliotoa maoni ya katiba,ni rais wa waliotaka serikali 2 na ni Rais wa waliotaka serikali 3.pale haendi kwa tiketi ya Mwenyekiti wa CCM,anaenda kama Rais wa nchi.kama wanataka kumjibu warioba walipaswa kuita press conference iwe live ili chama kitoe hoja za serikali 2.Hiyo ndio busara na hekima ya uongozi ktk mfumo wa nchi kama yetu ambayo Rais ni m/kiti wa chama tawala.wenzie watamzomea tu hapo,mambo ambayo hatutaki yaendelee.