CCM wajipanga kuchakachua katiba mpya

CCM wajipanga kuchakachua katiba mpya

janken mbisso

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
248
Reaction score
71
Chama cha Mapinduzi hakina dhamira ya kwel ktk kuhakikisha watanzania tunapata katiba mpya na iliyotungwa kulingana na mahtaji ya watanzania wenyewe.Kimejipanga kuchakachua maoni ya wapenda mabadiliko kwa hofu ya kupoteza madaraka 2015.

Hayo yamebainika wakati wa mchakato huu wa kuwachagua wajumbe wa mabaraza ya katiba katka kata mbali mbali.Wenyeviti wa mitaa na vitongoji/vijiji wamepewa maelekezo toka CCM kuhakikisha wote wanaopitishwa ni wanaCCM waaminifu pekee,wasiruhusu mtu wa CHADEMA kupita.

Wanafanya kwa maagzo toka juu lengo likiwa kupata uhuru wa kupitsha mambo wanayoyataka pia kupindisha wasioyataka.Haya yamedhitishwa na mwenyekiti wa UVCCM kutoka ktk wilaya moja Nyanda za Juu.Vikao vimekuwa vikifanyika.
 
Wewe ni mtabiri kutoka wapi? Nigeria?
 
La ajabu mpaka afisa mtendaji wa mtaa wangu wa kimara akishirikiana na mwenyekiti wananiambia kwamba wametumwa kwamba wahakikishe kuwa tuliochaguliwa awali tunapokwenda kwenye uchaguzi wa pili kesho hakuna mtu wa Chadema atakayepitishwa akidhani kuwa mimi ni ccm. Nimejikausha tu nawasanifu.
Lakini hapa kwenye katiba mpya ni kiini macho tupu!
 
Huku moro ha2kuruhucwa hata kuwepo eti wana2pigia kura wa2 hawa2jui wala ha2jajieza kwao
 
Ni kweli lazima tulijue kuwa wazo la katiba mpya ccm sio lao wamedandia kwa sababu ikipatikana katiba ya wananchi wanajua watakuwa wamekalia kuti kavu sio uwongo wanahamasishana kuvuruga huu mchakato bila kujua wanajidanganya.
 
Jamani draft haijatoka nyinyi mlishaanza kuiponda project ya Katiba
Watu wengine mnapenda ugonvi, mazingira ya amani ni tabu sana kwenu.
 
Mm kwa leo nimeamua kuikimbia WDC baada ya kukomaa na kutoruhusiwa kupiga kura kama mjumbe wa WDC
 
Jamani draft haijatoka nyinyi mlishaanza kuiponda project ya Katiba
Watu wengine mnapenda ugonvi, mazingira ya amani ni tabu sana kwenu.

Mwali leo umefika huku?

Lakini hofu ya kuchakachuliwa katiba mpya ipo na ni kweli hawa watu wanaweza na wamejipanga kufanya hivyo, kwa sababu wao katika maisha yao yote hawakuwahi kuwa na wazo la kuleta katiba mpya, hasa yenye kubeba mahitaji ya wananchi, hawa jamaa kweli wamejipanga kuchakachua, na mchakato ulikwa WRONG since from the beginning, KUMRUHUSU RAIS KUUNDA TUME YA KURATIBU MAONI YA WANANCHI, lilikuwa KOSA KUBWA SANA!!!!
 
Ni ukweli ulio dhairi kabisa kuwa ccm wamepanga kuhakikisha kuwa wanaleta katiba itakayowaweka wao madarakani milele na hilo tumeshalielewa tangu awali.
 
Mwenyekiti wa tume ya katiba Jaji Joseph Warioba analijua hili? Kama ndiyo,anachukua jukumu gani kuhakikisha unyama huu haufanyiki? Tunaomba wale wote wenye ushahidi wa kutosha juu ya jambo hili waweke wazi ili wananchi tujue na ikiwezekana tutafute namna ya kulidhibiti. HAKIKA HAWA MAGAMBA(VIRUS-CCM) NI JANGA LA TAIFA LINALOTAKIWA KUSHUGHULIKIWA NA KILA MPENDA HAKI WA NCHI HII!
 
Wakubwa hapa monduli, bado ni aibu kubwa nasikia list hadi Lowassa,aka mkuu wa wa ufisadi hadi aridhie wala mikutano ya kuu ya kijji hajfanyika kwa baadhi ya vijiji kabisa,
Ukweli ni kwamba lowassa na viongozi wa ccm monduli wanahujumu sana swala uwakilishi wa wananchi,
Leo kata baadhi hapa monduli wamegoma kabisa kutangaza matokeo ya wajumbe waliochagua na WDC, hadi Lowassa atoe kauli.
 
Hata watumie njia hizo za kijinga kama walivyozoea, watambue kuwa mwisho wa yote katiba mpya itapatikana baada ya waTz kuipigia kura rasimu ya katiba mpya. Wakiweka ujinga wao TUNAIKATAA
 
La ajabu mpaka afisa mtendaji wa mtaa wangu wa kimara akishirikiana na mwenyekiti wananiambia kwamba wametumwa kwamba wahakikishe kuwa tuliochaguliwa awali tunapokwenda kwenye uchaguzi wa pili kesho hakuna mtu wa Chadema atakayepitishwa akidhani kuwa mimi ni ccm. Nimejikausha tu nawasanifu.
Lakini hapa kwenye katiba mpya ni kiini macho tupu!

Mkuu hapo ndo visimu vyetu vya mchina inapobidi fifanye kazi barabara, ukiona hujuma za hivo zinapangwa we unakibofya na kuwarekodi, ukiweza hata kapicha chukua, kisha unarusha kwa makamanda; shahidi kama hizo ni muhimu huko mbele tuendako. Huu ni mpambano mkuu hakuna kulala.
 
baada ya kesho nitaweka wazi mengi yanayojiri hapa kwetu arusha, jina langu limepita kwa shurba sana.
kesho nitajua tu.
 
Kujua haya tu ni ishara kwamba hakuna hujuma yoyote itakayofanikiwa , Shame on them !
 
Chama cha Mapinduzi hakina dhamira ya kwel ktk kuhakikisha watanzania tunapata katiba mpya na iliyotungwa kulingana na mahtaji ya watanzania wenyewe.Kimejipanga kuchakachua maoni ya wapenda mabadiliko kwa hofu ya kupoteza madaraka 2015.

Hayo yamebainika wakati wa mchakato huu wa kuwachagua wajumbe wa mabaraza ya katiba katka kata mbali mbali.Wenyeviti wa mitaa na vitongoji/vijiji wamepewa maelekezo toka CCM kuhakikisha wote wanaopitishwa ni wanaCCM waaminifu pekee,wasiruhusu mtu wa CHADEMA kupita.

Wanafanya kwa maagzo toka juu lengo likiwa kupata uhuru wa kupitsha mambo wanayoyataka pia kupindisha wasioyataka.Haya yamedhitishwa na mwenyekiti wa UVCCM kutoka ktk wilaya moja Nyanda za Juu.Vikao vimekuwa vikifanyika.

Watanzania msitarajie kupata katiba mpya,ni maigizo tu ya WATAWALA wakishirikiana na WATAWALIWA.
 
Back
Top Bottom