CCM wajipanga kuchakachua katiba mpya

CCM wajipanga kuchakachua katiba mpya

Hata wakichakachua 2014 tunaanza na serikali za mitaa na 2015 tunamalizia na serikali mpya kwa nguvu ya umma.
 
Mwali leo umefika huku?

Lakini hofu ya kuchakachuliwa katiba mpya ipo na ni kweli hawa watu wanaweza na wamejipanga kufanya hivyo, kwa sababu wao katika maisha yao yote hawakuwahi kuwa na wazo la kuleta katiba mpya, hasa yenye kubeba mahitaji ya wananchi, hawa jamaa kweli wamejipanga kuchakachua, na mchakato ulikwa WRONG since from the beginning, KUMRUHUSU RAIS KUUNDA TUME YA KURATIBU MAONI YA WANANCHI, lilikuwa KOSA KUBWA SANA!!!!
Mi hua naingia kujadili hoja. Ila tatizo la hili jukwaa linajadili watu zaidi, na sometimes hata kujadili members. Inakatisha tamaa.
BTT: Kuchakachua maana yake nini? Kuna kipengele gani ambacho mnahisi kilitakiwa kusema A lakini mnaona wataishia kusema B? Huwezi kusema kua katiba itachakachuliwa just because UNAHISI kua INTENTION ya counterpart ni mbaya. Hii katiba haijatolewa hata draft. Hayo maoni ya wananchi hata hatujayajua. Just be patient, mseme hayo at least when we have the draft in hand.
 
Jamani draft haijatoka nyinyi mlishaanza kuiponda project ya Katiba
Watu wengine mnapenda ugonvi, mazingira ya amani ni tabu sana kwenu.

Rasimu ya Katiba dada tayari imetoka, Warioba tayari ameweka maoni yake binafsi na kutupilia mbali maoni ya Watanzania wenyewe, kwanfano asilimia 66% kule Zanzibar wametaka Mkataba. Kwa mujibu wa Rasimu ya Katiba Warioba aliyoitowa tayari suala la Mkataba amelitupilia mbali amelazimisha mabaraza ya katiba watu wajadili mfumo wa serikali 2 au 3 jambo ambalo katika Maoni halikutajwa., halikuwa na priority hasa kwa upande wa Zanzibar. Kwa mtazamo wako hapo CCM imekusudia nini? Kwa Zanzibar lazima kitaeleweka wazanzibari hawakubali.,
 
Mbana hili jambo liko wazi ................... Fuatilia habari ya "Zanzibar kujiunga na OIC 2014" ambapo Makamu wa CCM ZNZ amedai wamekuabliana ndani ya CCM kuwa ZNZ wapewe baadhi ya mamlaka na kuwa swala la mafuta na gas halitakuwa la muungano.

Yaani CCM wanajitengenezea katiba yao wenyewe na si ya Watanzania wote. Sasa hawa waganga njaa wa serikali za mitaa ndiyo watatumiwa bila kujielewa ................... kweli nimeamini 'Mtaji wa CCM ni ujinga wa Mtanzania!!"
 
Mimi nilishastukia hii siku ya uchaguzi, utaratibu ulikuwa wa siri, siku ilipangwa ni siku ya kazi, kulikuwa na muda maalumu wa kufika ambao ulikuwa siri, baadaye mkifika manafungiwa, tuliuliza tukaambiwa na maelekezo ya kutoka juu. Kila mtaa ulitakiwa kuchagua watu nane ambao watapigiwa kura na kamati ya utendaji ya kata, ambayo imejaa CCM.

UKWELI NA WALAUMU VIONGOZI WA CHADEMA kwani hawakuwa smart kubaini mbinu hivi. Tunaenendekeza mikutano na maandamano wakati wenzetu wanashinda kwa mbinu ya kisayansi.

Kwenye mkutano sikuwaona vijana hasa wale tunaosalimiana kila siku Peoples!!!, nilipowauliza wanasema walikuwa hawana habari kuwa chaguzi ulikuwa na Timing na deadline, kwani walikwenda kuripoti makazini, lakini pia wa vijiweni hawakuwepo. Inaonyesha hatufanyi maandalizi mapema, bila good and visionaly leader ship licha ya kutumia nguvu hatuwezi kuleta mabadiliko ya kweli.

Napendekeza tuanze kufanya uratibu wa ushindi mapema, ikiwamo kuwaratibu wapiga kura, na vijana wengi wanapenda mabadiliko lakini hawakotayari kujitolea, wengi hawaja jiandikisha, wanaishi kwa kuzania tuu kuwa wengine watafanya kwa niaba yao.

Chama cha Mapinduzi hakina dhamira ya kwel ktk kuhakikisha watanzania tunapata katiba mpya na iliyotungwa kulingana na mahtaji ya watanzania wenyewe.Kimejipanga kuchakachua maoni ya wapenda mabadiliko kwa hofu ya kupoteza madaraka 2015.

Hayo yamebainika wakati wa mchakato huu wa kuwachagua wajumbe wa mabaraza ya katiba katka kata mbali mbali.Wenyeviti wa mitaa na vitongoji/vijiji wamepewa maelekezo toka CCM kuhakikisha wote wanaopitishwa ni wanaCCM waaminifu pekee,wasiruhusu mtu wa CHADEMA kupita.

Wanafanya kwa maagzo toka juu lengo likiwa kupata uhuru wa kupitsha mambo wanayoyataka pia kupindisha wasioyataka.Haya yamedhitishwa na mwenyekiti wa UVCCM kutoka ktk wilaya moja Nyanda za Juu.Vikao vimekuwa vikifanyika.
 
Hivi kulikuwa na mwongozo maalum juu ya uchaguzi huo? Mathalan, kuna utaratibu wa kukata rufaa kama mgombea hataridhika na uamuzi au uchaguzi?

Kama wajumbe wa WDC wanalingana na wagombea kuna uwezekano wa kutopatikana mshindi kwani kila mwenyekiti wa mtaa anaweza kumchagua mjumbe wa mtaa wake tu, na hivyo kutopatikana mshindi. Nini kitafuata?

Yawezekana mshindi akapatikana kwa kupata kura 2 tu miongoni mwa wagombea 10? Hiyo ni simple majority?

Kwa nini mahali pengine kuliwa na wajumbe kujieleza wakati mahali pengine kura zimepigwa bila wagombea kuwepo?

Kama makundi ya uwakilishi ni matatu-watu wazima, wanawake na vijana, kwa nini wamechaguliwa wajumbe wanne wanne?
 
Back
Top Bottom