fikirini
Senior Member
- May 24, 2011
- 114
- 22
Mbunge wa CCM ameibuka na kuwajibu wapinzani wakati akichangia mjadala wa bajeti leo. Alimjibu Mbunge wa Mbozi kwa tiketi ya Chadema David silinde aliyesema kuwa ni miaka 50 sasa tangu uhuru na Tz haina maendeleo. Zungu amesema Tz inamaendeleo na mafanikio makubwa na isingekuwa hivyo basi hata yeye(Silinde) asingeweza fika bungeni angebakia huko huko na degree yake(mmmh, hapa kuna uhusiano kweli?) mimi nilivyomuelewa silinde au kwa mtazamo wangu ni kuwa maendeleo tuliyonayo Tz si kiwango stahiki, hatustahili kuwa hapa tulipo ukilinganisha na rasilimali kibao ambazo nyingi wanazichezea wachache walioko madarakani na zingine wageni wanagawiwa.
Jamani upinzani haupo kwa ajili ya kupinga tu, wanauchungu pia na nchi yao.
Jamani upinzani haupo kwa ajili ya kupinga tu, wanauchungu pia na nchi yao.