CCM wadhamiria kulinyakua jimbo la Moshi Mjini!

Nadhani maoni ya Mleta mada yaheshimiwe, na yawe kama darasa! Ni busara sn kukubali mapungufu pale yanapokuwepo.
Namheshimu sn member @T2015CDM na kwa uzoefu wake na cdm naamini ana substance!
Kama ana ukaribu na vikao vya ndani vya chama km ambavyo mnadai basi aliseme huko pia.

Mkuu PakaJimmy angalia vizuri hiyo ID sidhan kama ni Original. Ni mtu amerecreate a almost similar akijua kabisa atawateka wengi kwa kutumia Iman mliyo nayo kwa T2015CDM lakin huyu ni T.2015.CDM
 
Kama walivyosema wadau ushauri wako ni mzuri,lakini umeonesha makengeza kwa kuuleta hapa.Kwa jinsi inavyoonekana ni kama tayari mna makundi ya mnyukano kuwania kumrithi Ndesa na ww upo kwenye kundi mojawapo.Kama ndivyo basi humu sio uwanja sahihi wala si wakati muafaka.Laa kama nimepotoka uniwie radhi.
 
Kama huyo ulie mtaja ameonekana kuwa ni mbovu na kama ndie anaeandaliwa kukiwakilisha chama kulitetea jimbo.haina maana kuwa yeye ni bora kuliko wana chama wenzake.cdm ina wanachama wengi wazuri na makini.akiboronga atawekwa pembeni na mwanachama mwingine atachukuwa nafasi hiyo.halafufu si kweli kwamba hapo ndiyo tayari ameshapata tiketiketi ya kukiwakirisha chama nafasi hiyo itashindanishwa na wanachama wenzake atakaeshinda ndie atakae peperusha bendera ya chama.makosa yaliofanywa na wanachama wa cdm waliopewa dhamana na wachi ili wawaongoze hawatapewa ccm eti ndio wayasahihishe.yatasahihishwa na wanacdm wenyewe.
 
Kw swala la kutokukubali ushaur ni uzushi pia Japhar ni m2 anayekubalika sana na wakaz wa manispaa ya moshi kuliko mgombea yoyote ama kutoka ndan au nje ya CHADEMA ikiwemo CCM.Swala la uongoz wa mkoa CHADEMA pamoja na jumuiya zake kwkweli ni kama hamna uongoz kwan hata ofisi hamna wengi ni wa2 wa blaa blaa kuanzia mtendaj mkuu BAZIL LEMA PAMOJA NA WAENEZ WOTE WA MKOA PAMOJA NA WILAYA ZAKE HASA MMOJA ANAYEJULIKANA KWA JINA LA MAKELELE WAMESHINDWA KABISA KUENDESHA NA KUIMARISHA CHADEMA NDAN YA MKOA WA KILIMANJARO KUNA HAJA YA KUFANYA MABADILIKO MAKUBWA YA UONGOZ WA CHADEMA MKOA WA KILIMANJARO ULIOPO HAUFAI DR. SLAA NAJUA MNAPITA HUMU LIFANYIE KAZI
 
Mkuu PakaJimmy angalia vizuri hiyo ID sidhan kama ni Original. Ni mtu amerecreate a almost similar akijua kabisa atawateka wengi kwa kutumia Iman mliyo nayo kwa T2015CDM lakin huyu ni T.2015.CDM
Aisee wewe mkari, unafaa sana kukaa kitengo cha Anti fraud.
 
hilo lijnawezekanika kwa kila jambo na ni kweli mkakati huo upo na hujaanza leo wadau kikubwa ni kukaza na kuondokana na ufisadi wa hao magammba.ila ni kweli napo chama kinatakiwa kuwa makini mana mh jafary naye ni mgumu sna kuelewa mambo hvyo kikubwa ni kuwa makinii
 
kikubwa ni kukazana mana unapokose marqa moja hutakiwi kukosea tena.jimo hilo ni kweli wana lilia sna wadau wa magamba ila kikubwa tunalifanyia kazi asante kwa taarifa
 
Kumhonga mchaga mpaka abadilike kutoka cdm kwenda ccm! Ni ngumu sana maana wengi hawana njaa za ovyo!
 
Kama meya ana tatizo ni vema chama kikalishughulikia mapema vinginevyo watu watapoteza imani kubwa ambayo wameshaionesha kwa CHADEMA.
 
Ukweli ni kwamba hata CCM wafanye lolote katu Moshi mjini ni CHADEMA daima. Hili hata makada wote wa Ccm wanalijua kuanzia Nape mpaka JK, ndio maana ni rahisi sana kwa CCM kuihusisha Chadema na propaganda za kikabila kwani CCM inachukiwa sana Moshi mjini kuliko hata choo kichafu kibovu.

Mikakati yote ya CCM kulichukua jimbo hili iliishia 2010 chini ya secretarieti ya Yusuph Makamba, baada ya CCM kushindwa vibaya kwa kura na kupoteza viti vingi vya udiwani ilivyokuwa inavishikiria hapo kabla pamoja na jitihada kubwa ya kutaka kuvitetea.

Kama kuna raia wanaojua machungu ya CCM na hasira ya kutaka kuona CCM inaondoka madarakani basi fika Moshi mjini.

Nina uhakika hakuna raia wa Moshi mjini anayeweza kuhongwa kwa kitu chochote halafu iipigie Ccm kura.

Watu wa kwanza kuichukia CCM hapo Moshi mjini ni wakinamama na wazee.

Uchaguzi wa 2015 nina uhakika CCM haitapata hata kiti kimoja cha udiwani Jimbo la Moshi Mjini achilia mbali ubunge.
Ni kweli mkuu kwa kuwa mtaji wa CCM yaani ujinga, umaskini, na maradhi si SERA ya CDM kama wao CCM aka CHARITY for MABWEPANDE killers!!
 
Mpango mzima hapa ni kuongeza majimbo na wala si kupunguza. Naamini cdm watajua cha kufanya hasa ukizingatia utumishi makini wa mzee ndesa pale motown. Lengo ni kushika Dola na majimbo mengi iwezekanavyo
 
Wanabodi,

Jimbo la Moshi mjini limekuwa ngome ya upinzani toka mwaka 1995 pale lilipochukuliwa na NCCR Mageuzi na baadae mwaka 2000 lilichukuliwa na Chadema hadi sasa wanalishikilia.

Kwa sasa hivi kinachoendelea katika manispaa ya Moshi kinatia mashaka makubwa kama kweli Chadema wana dhamira ya dhati kuleta maendeleo ya kweli. Madiwani wa Chadema pamoja na Mbunge wa sasa Philemon Ndensamburo, wate wakati wa kampeni walijinadi kwa mambo sita ya msingi wakati wa kampeni.

Kutatua tatizo la wafanyabiashara ndogondogo walitoa ahadi wakichaguliwa watajenga Machinga Compelex, wote waliguswa na ahadi hiyo leo mwaka 2015 hawajaona jengo wala kiwanja, la pili suala la utoaji wa huduma ya elimu bure. Kwamba halmashauri ilikuwa na mapato mengi ambayo yangewezesha kutoa elimu bure leo hii hakuna kitu.

Waliahidi pia kujenga Hospitali ya Manispaa ya Moshi ya Wilaya, lakini kama ilivyokuwa kwa Machinga Complex, hakuna jengo wala kiwanja, walihaidi wangefufua viwanda vilivyokufa, hakuna kiwanda chochote kilichofufuliwa. Walihadi wakichukuwa halmashauri kazi ya kwanza kudhibiti matumizi ya fedha.

Lakini hivi karibuni tumeona mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Gama, akifanya uamuzi mgumu kuzuia safari ya madiwani na watendaji 57 kwenda Kigali Rwanda, kwa siku sita, ilikuwa igharimu zaidi ya Sh200 milioni za walipa kodi maskini wa mji wa Moshi...hawa ndio Chadema.
 
Mkuu Ritz,hujambo?pole kwa kaz ngumu uliyonayo ndani ya ccm!!!mchana huu umekula?mbona upo hivyo?tafuta chakula tafadhali!!!
 
Na vp kuhusu majimbo ya CCM, mambo yakoje?? Unavyofanya uchambuzi, inabidi uangalie pande zote manake CDM wanaweza wakapoteza Moshi mjini lakini wakapata mengine yote yaliyobaki Tanzania na hivyo kukawa hakuna ubaya kisiasa. Kwa upande wa pili, unaweza ukaonesha hivyo kumbe jitihada zimefanywa ila zimezuiwa na serikali kuu chini ya Mkuu wa mkoa na watu wengine wizarani.
 
Nawashauri waachane na Moshi kwanza, wajipange jinsi ya kutukana, kuhonga, kuiba kura na wake za watu kule Sumbawanga!.
 
Wanabodi,

Jimbo la Moshi mjini limekuwa ngome ya upinzani toka mwaka 1995 pale lilipochukuliwa na NCCR Mageuzi na baadae mwaka 2000 lilichukuliwa na Chadema hadi sasa wanalishikilia.

Kwa sasa hivi kinachoendelea katika manispaa ya Moshi kinatia mashaka makubwa kama kweli Chadema wana dhamira ya dhati kuleta maendeleo ya kweli. Madiwani wa Chadema pamoja na Mbunge wa sasa Philemon Ndensamburo, wate wakati wa kampeni walijinadi kwa mambo sita ya msingi wakati wa kampeni.

Kutatua tatizo la wafanyabiashara ndogondogo walitoa ahadi wakichaguliwa watajenga Machinga Compelex, wote waliguswa na ahadi hiyo leo mwaka 2015 hawajaona jengo wala kiwanja, la pili suala la utoaji wa huduma ya elimu bure. Kwamba halmashauri ilikuwa na mapato mengi ambayo yangewezesha kutoa elimu bure leo hii hakuna kitu.

Waliahidi pia kujenga Hospitali ya Manispaa ya Moshi ya Wilaya, lakini kama ilivyokuwa kwa Machinga Complex, hakuna jengo wala kiwanja, walihaidi wangefufua viwanda vilivyokufa, hakuna kiwanda chochote kilichofufuliwa. Walihadi wakichukuwa halmashauri kazi ya kwanza kudhibiti matumizi ya fedha.

Lakini hivi karibuni tumeona mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Gama, akifanya uamuzi mgumu kuzuia safari ya madiwani na watendaji 57 kwenda Kigali Rwanda, kwa siku sita, ilikuwa igharimu zaidi ya Sh200 milioni za walipa kodi maskini wa mji wa Moshi...hawa ndio Chadema.

Uongo mtakatifu/noble lie
 
Back
Top Bottom