CCM wadhamiria kulinyakua jimbo la Moshi Mjini!

CCM wadhamiria kulinyakua jimbo la Moshi Mjini!

Wanabodi,

Jimbo la Moshi mjini limekuwa ngome ya upinzani toka mwaka 1995 pale lilipochukuliwa na NCCR Mageuzi na baadae mwaka 2000 lilichukuliwa na Chadema hadi sasa wanalishikilia.

Kwa sasa hivi kinachoendelea katika manispaa ya Moshi kinatia mashaka makubwa kama kweli Chadema wana dhamira ya dhati kuleta maendeleo ya kweli. Madiwani wa Chadema pamoja na Mbunge wa sasa Philemon Ndensamburo, wate wakati wa kampeni walijinadi kwa mambo sita ya msingi wakati wa kampeni.

Kutatua tatizo la wafanyabiashara ndogondogo walitoa ahadi wakichaguliwa watajenga Machinga Compelex, wote waliguswa na ahadi hiyo leo mwaka 2015 hawajaona jengo wala kiwanja, la pili suala la utoaji wa huduma ya elimu bure. Kwamba halmashauri ilikuwa na mapato mengi ambayo yangewezesha kutoa elimu bure leo hii hakuna kitu.

Waliahidi pia kujenga Hospitali ya Manispaa ya Moshi ya Wilaya, lakini kama ilivyokuwa kwa Machinga Complex, hakuna jengo wala kiwanja, walihaidi wangefufua viwanda vilivyokufa, hakuna kiwanda chochote kilichofufuliwa. Walihadi wakichukuwa halmashauri kazi ya kwanza kudhibiti matumizi ya fedha.

Lakini hivi karibuni tumeona mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Gama, akifanya uamuzi mgumu kuzuia safari ya madiwani na watendaji 57 kwenda Kigali Rwanda, kwa siku sita, ilikuwa igharimu zaidi ya Sh200 milioni za walipa kodi maskini wa mji wa Moshi...hawa ndio Chadema.




Kwa mtu ambaye ajui kama wewe atasema hivyo, kwa mfano pesa ambayo waliotaka kuitumia madiwani ipo katika kifungu kuwawesesha madiwani kimafunzo, hata kama wasipokitumia kwenda rwanda kitatumika katika malengo yale yale. bajeti inapopangwa upangwa kwa vifungu km ni kwa ajili ya elimu kifungu fulani, maendeleo kifungu fulani na nk kwa hiyo mtu ambaye ajui haya mambo utaongea tu.
 
Nibora ungeongelea jimbo lingine,kama nimchinga complx tunaweza kujenga kwa siku mbili maana pesa sipo ila kwasasa tunaweka mipango,
 
Mods thread yangu aina uhusiano na CCM mmeiunganisha.
 
Ngoja kwanza tumalize udiwani Oct 28 ndio tutaanza kuongelea mambo ya 2015.
 
huyu dogo nepi anamlipa bei gan? Watu wa mo town si wajinga kihivyo walishasema no kwa magamba na hilo halitobadilika wameelimika endeleen kuwadanganya wajinga
 
Kumhonga mchaga mpaka abadilike kutoka cdm kwenda ccm! Ni ngumu sana maana wengi hawana njaa za ovyo!

anaweza akala ela yako na kura asikupe vilevile. CDM ipo damuni mwa watu.
 
Kuna mwandishi mmoja anaitwa daniel mjema amepewa kazi maalumu kumchafua mbunge mtarajiwa kupitia chadema 20i5 mh.meya japhary maiko
 
Nahisi kama kuna harufu ya ugomvi binafsi,ingawa inawezekana sipo sahii.Kama ni kweli basi ni vema ungetumia vikao halali vya chama kufikisha hili tatizo!
 
Ndugu zangu wana chadema kuna baadhi ya mambo inabidi tuyaseme hatakama yana uma hii ni kwa kukisaidia chama. Tusipokuwa makini tutalipoteza hili jimbo la Moshi mjini.

Kwa taarifa nilizozipata toka kwa mjumbe wa kamati kuu ya ccm ni kuwa chama hicho kimeelekeza nguvu nyingi mkoani huko haswa baada ya kugundua kuna uzaifu katika nguzo kuu za chadema jimboni hapo. Wengi wanajua kuwa huu ni mhula wa mwisho wa mzee wetu Ndesamburo na sasa anaandaliwa meya wa mji Mh. Jafari ili kupokea kijiti hicho, kwa wale ambao wanamfahamu huyu bwana au kumfatilia watakubaliana nami kuwa ameshaonyesha mapungufu kadhaa katika uongozi wake wa manispaa ya Moshi mjini ila tushukuru sana madiwani wenzake ni wavumilivu sana na wamemstahi vya kutosha la sivyo wangesha mng'oa.

Kwanza ni mbishi, jeuri, mbabe na kwasababu ameshajihisi kuwa ni mrisi wa jimbo Jafari amebadilika sana naweza kusema haambiliki anamaamzi ya kibabe na akiamuwa hashauriki, baada ya Ndesamburo kumwachia shughuli za jimbo kuzisimamia kama msaidizi Chadema Moshi mjini imeharibika taswira na kuonyesha mapengo mengi ambayo ccm wanayatumia ipasavyo kujiimarisha kwa siri kubwa na kwa kasi, katika historia ya chadema hapa Moshi mjini haijawahi tokea kukawa na mgogoro kati ya manispaa na wananchi pindi Manispaa ilikiwa chini ya chadema, ni wakati huu wa Mh.jafari naomba chama kimwangalie kwa ukaribu sana.

Nawaomba viongozi wa Chadema Taifa mliangalie hili kwa umakini mkubwa, ccm wamejipanga kikamilifu haswa baada ya kugunduwa hawawezi kilirudisha jimbo la Arusha mjini na Mtoa taarifa huyo amesema hawawezi kuyaachia majimbo yote makubwa ya kaskazini yaende upinzani sisi kama wanachama na wapemzi hatuko tayari kulipoteza jimbo hili mama lililokilea chama mpaka hapa kilipo sasa Mh. Jafari ameshindwa hata kuendesha mikutano ya kukiamsha chama?

Hi ni aibu chama kiko kama hakiko viongozi mkoa wako singizini wakati wenzao hawalali kikiimarisha chama kwa vikao na wazee wa mkoa na sasa upepo unaanza kubadilika taratibu.

Ukitaka kuyaamini haya ninayo yasema hapa fuatilieni chaguzi mbalimbali za CCM mkoa wa Kilimanjaro haswa jimbo la Moshi Mjini mtajua ni nini kinaendelea.
Nikuunge mkono CHADEMA HAINA VIONGOZI MAKINI HATA KIDOGO KATIKA MKOA WA KILIMANJARO HATA OFISI YA MKOA NI KAMA HAIPO KWAN HAMNA KITU PALE OFISINI CHAMA KIMELALA VIONGOZI WENGI NI BLAA BLAA ILA KWA UBUNGE JAPHAR ATACHUKUA HILO HALINA UBISHI ILA UONGOZ WA CHAMA TAIFA WAJUE HAPA UONGOZ KW MASLAH YA CHAMA HAMNA
 
Back
Top Bottom