CCM Waanza Kutekeleza Agizo la JK Kalenga

CCM Waanza Kutekeleza Agizo la JK Kalenga

CHADEMA

Political Party
Joined
Apr 13, 2013
Posts
495
Reaction score
2,539
Baada ya M/Kiti wa CCM Taifa Kuwaagiza WanaCCM wenzake kuwa wasiwe Wanyonge kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kalenga, Hatimaye Vijana wa Chama hicho wameanza kuonyesha nguvu na ukatili wao kwa kumchoma kisu cha Mbavu Ndugu Richard ambaye ni M/Kiti wa Tawi la CHADEMA la Kijiji cha Tagamenda siku moja tu baada ya Mama Mzazi wa Kijana huyo ambaye alikuwa Mjumbe wa Serikali ya Kijiji hicho kwa tiketi ya CCM kuamua kuhamia CHADEMA kwa madai ya kuchoshwa na siasa zisizokuwa na mwelekeo za Chama hicho

Tukio hili ni muedelezo wa matukio mengine kadhaa ambayo CCM wamekuwa wakiyafanya kwenye Kampeni hizi ambapo siku mbili zilizopita walimteka Paroko wa Chuo cha mission cha Katoliki kilichopo eneo la Tosamaganga kwa madai kuwa ni MwanaCHADEMA.

HATUTAACHA HALI HII IENDELEE

Pichani ni Daktari akiwa amezamisha kidole chake kwenye jeraha la Ndugu Richard wakati alipokuwa akimsafisha kidonda baada ya tukio hilo.
 
Attachments

  • Jeraha.jpg
    Jeraha.jpg
    34.5 KB · Views: 2,525
baada ya m/kiti wa ccm taifa kuwaagiza wanaccm wenzake kuwa wasiwe wanyonge kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la kalenga, hatimaye vijana wa chama hicho wameanza kuonyesha nguvu na ukatili wao kwa kumchoma kisu cha mbavu ndugu richard ambaye ni m/kiti wa tawi la chadema la kijiji cha tagamenda siku moja tu baada ya mama mzazi wa kijana huyo ambaye alikuwa mjumbe wa serikali ya kijiji hicho kwa tiketi ya ccm kuamua kuhamia chadema kwa madai ya kuchoshwa na siasa zisizokuwa na mwelekeo za chama hicho
lakini picha inaonyesha jeraha lipo maeneo ya kifuani!! Anyaway, siasa za vurugu ccm na chaedema wote mnahusika.
 
Hivi ccm mnataka kuipeleka wapi hii nchi, kwa nini mnafanya siasa za kurazimisha, mnaelewa maana mfumo wa vyama vingi, haya polisi Iringa, kazi kwenu, nyie mnajua kumkamata mh Msigwa pasipo na makosa, ila kimtu kama kikatibu kinachotishia kuua hadharani hamuwezi, wala hamuwezi kukamata hao vijana wa ccm wanaoendesha fujo kila uchaguzi.
 
mungu nakuomba uibariki tanzania mungu nakuomba uwabariki watanzania mungu naomba uwafungue macho hawa watanzania hawa wote ni ndugu lakini kwa tamaa za kipesa madaraka ndo yanasababisha haya matatizo mungu nakuomba uweke ulinz wako katika taifa hili serikali imeshindwa kuwalinda raia wake ila imemudu kuwaangamiza raia wake ambao ndo wanasababisha viongoz hawa wawe madarakani
 
chadema wakileta vurugu wapewe kichapo tu. tumewachoka
 
Wewe kriss unadhani wote wezi kama wewe?
 
Kurugenzi ya Habari

Picha mliyotumia siyo ya ki weledi. Ingekuwa vyema kutoa picha baada ya kuwa amepewa matibabu na siyo hii!
 
Kurugenzi ya Habari

Picha mliyotumia siyo ya ki weledi. Ingekuwa vyema kutoa picha baada ya kuwa amepewa matibabu na siyo hii!

Unaficha nini?
Ingeletwa yenye kuoinyesha bandage mgebisha au hujuhi kuwa kuna watu mpaka wapapse ndio wanaamini?
 
Sababu kama hizi ndizo zinapandikiza chuki na visasi ndani ya jamii na kusababisha mauaji ya kimbari. Tusije kushangaa viongozi wanaojinadi kwa utawala bora na sheria wakapandishwa the Hague.
 
Kazi ya kuuwa ya chadema haina makosa, tuwalaani daima
 
Baada ya M/Kiti wa CCM Taifa Kuwaagiza WanaCCM wenzake kuwa wasiwe Wanyonge kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kalenga, Hatimaye Vijana wa Chama hicho wameanza kuonyesha nguvu na ukatili wao kwa kumchoma kisu cha Mbavu Ndugu Richard ambaye ni M/Kiti wa Tawi la CHADEMA la Kijiji cha Tagamenda siku moja tu baada ya Mama Mzazi wa Kijana huyo ambaye alikuwa Mjumbe wa Serikali ya Kijiji hicho kwa tiketi ya CCM kuamua kuhamia CHADEMA kwa madai ya kuchoshwa na siasa zisizokuwa na mwelekeo za Chama hicho

Tukio hili ni muedelezo wa matukio mengine kadhaa ambayo CCM wamekuwa wakiyafanya kwenye Kampeni hizi ambapo siku mbili zilizopita walimteka Paroko wa Chuo cha mission cha Katoliki kilichopo eneo la Tosamaganga kwa madai kuwa ni MwanaCHADEMA.

HATUTAACHA HALI HII IENDELEE

Pichani ni Daktari akiwa amezamisha kidole chake kwenye jeraha la Ndugu Richard wakati alipokuwa akimsafisha kidonda baada ya tukio hilo.

Mtatunga mengi na kupanga njama nyingi ovu ili ku buy sympathy ya watu hamtafanikiwa...

Ila nawaonea huruma wananchi wanaokuwa sehemu ya wahusika wa maigizo yenu maana inawagharimu sana na itawachukua muda kutambua udhalimu wenu...

Ni wakati muafaka kwa watanzania kukaa kando na siasa za CHADEMA maana mipango yao inawagharimu sana wananchi wasio na hatia..

Ipo siku unyama huu utawarudia hata kama watoto wa viongozi wa CDM wamekimbiziwa nje ya nchi..
 
Back
Top Bottom