CCM vs Serikali

CCM vs Serikali

Msafiri Haule

Member
Joined
Aug 6, 2018
Posts
28
Reaction score
18
Salamu kwenu, nyote wenye kulitakia heri taifa.

Yahitaji maarifa ya CUBA kuelewa kwa namna gani CCM inamudu kusimamia serikali. Hii inakuja baada ya wajumbe wakuu wa Kamati kuu kuwa ni viongozi wakuu wa serikali mfano Rais, Spika na Waziri.

Sasa, maagizo ya Kamati Kuu kuielekeza serikali ambayo ilikuwa ndiyo inaongoza hicho kikao hususani kuangalia upya hoja za wananchi juu ya Tozo, je Kuna msingi?

Ni wazi kuwa Kamati kuu haijui kama kiongozi mkuu wa serikali ndiye Mwenyekiti wao wa Chama na ndiye aliyewaongozea kikao chao?

Kwanini kamati kuu haikutoa kauli kuwakumbusha wabunge wa chama juu ya umuhimu wa kuwa wasemaji wa matatizo/kero za wananchi?

Kamati Kuu ya chama yaona sababu ya msingi kuwa na tozo hasa ikiwa ripoti ya CAG yatoa madudu namna pesa za umma zinavyoporwa? Bado kuna haja ya tozo inayoongeza ugumu wa "walalahoi?"

Msimamo:
Taifa linaombwe katika usimamizi wa rasilimali mama katika kutoa matunda chanya kwa watu wote. Ni maoni yangu kuboresha mifumo (institutions) ya kitaasisi ili itoe nafasi katika uwazi na uwajibikaji wa mali za umma. Wananchi tunapoona uhalali wa kimatumizi katika kodi/fedha tunazolipia, hatuta lalama. Ila, kutuvuruga kwa kujitekenya na kucheka wenyewe si sawa.

Kwa maana hiyo, sioni msingi wa kauli kutoka Kamati Kuu ikiwa Mwenyekiti wa Kamati Kuu ndiye aliyeidhinisha tozo, hivyo anajua undani wa maumivu katika hili.
 
Salamu kwenu, nyote wenye kulitakia heri taifa.

Yahitaji maarifa ya CUBA kuelewa kwa namna gani CCM inamudu kusimamia serikali. Hii inakuja baada ya wajumbe wakuu
Kwa mfumo wa hapa kwetu, chama hakina mamlaka juu ya serekali, ila rais ndiye mwenye mamlaka juu ya chama. Hii ni tofauti na nchi kama UK, Africa Kusini n.k ambapo chama kina mamlaka ya kumwondoa kiongozi wa serekali ktk uongozi. Kilichofanywa na CC ya CCM ni sarakasi kuonyesha chama kinajali lakini ni wale waleee!
 
Back
Top Bottom