CCM vipande NEC Dodoma; Makamba kung'atuka? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM vipande NEC Dodoma; Makamba kung'atuka?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 7, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 7, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [​IMG][​IMG]

  Aprili 6, 2011

  [​IMG]Makamba kung'atuka rasmi
  [​IMG]Makundi yakamiana
  [​IMG]Wataka nuksi kwa chama watoswe

  KIKAO cha Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinachotarajiwa kufanyika mjini Dodoma wiki hii kitakuwa na ajenda nzito zitakazoamua kukigawa ama kukipa uhai mpya chama hicho kikongwe nchini, huku Katibu Mkuu wake, Yussuf Makamba akielezwa ya kuwa atang'atuka rasmi.

  Taarifa za ndani ya chama hicho zinaeleza kwamba, miongoni mwa ajenda zinazotarajiwa kuibua mjadala mzito na huenda kuwagawa wajumbe katika makundi ni ile ya 'kujivua gamba,' hoja ambayo ni sehemu ya ahadi ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, aliyoitoa katika maadhimisho ya miaka 34 ya kuzaliwa kwa CCM, Februari mwaka huu.


  Imeelezwa kwamba ajenda hiyo itawagawa wajumbe katika makundi mawili makubwa, lile linalojipambua kupiga vita ufisadi ambalo Kikwete sasa anaelezwa kuliunga mkono na lile linalokejeli vita hiyo ama kutajwa kuhusika na ufisadi.


  Taarifa zinabainisha kuwa ajenda hiyo ina nguvu kubwa ndani ya CCM kwa sasa baada ya kubainika wazi kwamba ilikiponza chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana (2010) na chama hicho kuporomoka na kutoa mwanya kwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuimarika kwa kuongeza idadi ya wabunge hasa katika majimbo ya miji mikuu.


  CHADEMA kilishinda ubunge katika majimbo ya Nyamagana na Ilemela mjini Mwanza, Musoma Mjini, Mbeya Mjini, Moshi mjini, Arusha mjini, Iringa mjini na sehemu ya kigoma mjini. Inadaiwa kuliibuka mpasuko mkubwa ndani ya CCM unaodaiwa msingi wake ni nguvu ya fedha kutumika kuteua wagombea ubunge kwa tiketi ya CCM, badala ya nguvu ya kisiasa.


  Imefahamka kwamba wajumbe kutoka ukanda mmoja wa Jamhuri ya Muungano wamejipanga ‘kulitolea uvivu' suala hilo kwa kutamka bayana kwamba wanaohusika, hata kama ni kutajwa tu, katika ufisadi watoswe.


  "Wale jamaa wamepania kutaja hata majina ya watu ambao wanaona ni mzigo kwa CCM. Huko moto utakua mkali maana na wao wahusika wamejipanga kuwashughulikia wabaya wao na ikibidi hata Mwenyekiti Rais Kikwete ili kupoza joto," anasema mjumbe mmoja wa NEC.


  Imeelezwa tayari nukuu mbalimbali za nyaraka za CCM ikiwamo Katiba, Mwongozo na vitabu vya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere zimeanza kukusanywa ili kushadidia hoja zitakazowasilishwa katika kukosoana na hatimaye kujisahihisha ndani ya CCM.


  Ajenda nyingine inaelezwa kuwa ni malumbano yanayoendelea kati ya UVCCM na viongozi waandamizi wa zamani serikalini, jambo ambalo linatajwa kuibua mjadala hasa baada ya wazee kuamini kwamba vijana wametumwa kabla ya Rais Kikwete kugusia suala hilo hivi karibuni.


  Pamoja na kulitolea tamko, bado wazee hao wameelezwa kwamba wanataka kusikia kauli ya Kikwete ndani ya NEC kutokana na kauli hiyo kutolewa na UVCCM Mkoa wa Pwani anakotokea, huku mwanawe, Ridhiwani Kikwete, akiwa mjumbe mwenye nguvu za kisiasa katika UVCCM mkoani humo.


  "Wazee watataka Rais atoe tamko ndani ya NEC kuwakemea vijana hao, lakini kuna wazee wengine wanawaunga mkono vijana na wataweka wazi kwamba ni lazima viongozi wa zamani wamsaidie Rais wa CCM amalize kipindi chake salama kama na wao wanataka kuwania urais na washinde," anasema mjumbe huyo.


  Hivi karibuni visiwani Zanzibar, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi, alitamka hadharani kuunga mkono kauli ya vijana kuhusu viongozi wa zamani wanaotoa matamko hadharani na alikemea vijana wanaotumika kufanikisha malengo ya baadhi ya viongozi wa kisiasa.


  Imeelezwa katika kikao hicho, Katibu Mkuu, Yusuf Makamba anaweza kutangazwa kuwa anastaafu, ikiwa ni baada ya kipindi kirefu cha mashinikizo ya kumtaka ang'atuke kutoka kwa vijana, na sasa hata wazee wenzake ambao baadhi wamemuandikia hadi barua na yeye akawakejeli.


  Taarifa zaidi za kiuchunguzi zinabainisha kuwa kati ya wazee waliomwandikia barua Makamba kumtaka aachie ngazi ni pamoja na aliyekuwa Mbunge wa Kwela, Dk. Chrisant Mzindakaya.


  Mzindakaya ambaye naye alistaafu kuwania ubunge mwaka jana, anatajwa kumuandikia Makamba barua ya kutaka aachie ngazi na kuainisha sababu kadhaa, ikiwamo ya kutomudu changamoto za sasa za kisiasa.


  Inaelezwa kuwa Mzindakaya, mbali na kumwandikia Makamba barua hiyo, nakala amezisambaza kwa baadhi ya viongozi wengine wakuu wa CCM Makao Makuu.


  "Mzee Makamba atatangazwa kustaafu kwa heshima na anatarajiwa kufanyiwa sherehe ya kumuaga rasmi," anaeleza mtoa habari wetu.


  Mkutano wa sasa wa NEC unafanyika katika wakati ambao tayari UVCCM wameonyesha kuingia katika mvutano wa wenyewe kwa wenyewe, na pia mvutano kati ya baadhi ya viongozi wa umoja huo na viongozi wastaafu serikalini ambao pia kwa sasa baadhi ni wajumbe wa NEC-Taifa.


  Mbali na kadhia hiyo, CCM imekuwa katika mvutano wa makundi kwa muda mrefu kiasi cha kulazimika kuundwa kwa Kamati Maalumu ya kufuta mpasuko huo, hasa uliotajwa kuwagusa zaidi wabunge wa Bunge la tisa kutoka CCM.


  Kamati hiyo maalumu iliyoongozwa na Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, akisaidiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa na kada mwenzao, Abdulrahman Kinana, imeelezwa kama kamati iliyoshindwa kufanya kazi yake, na haikuwahi kutoa ripoti yake hadharani na dalili za kuendelezwa kwa makundi hayo zimekuwa zikijitokeza wazi wazi.


  Hayo yakiendelea, baadhi ya wajumbe wa NEC waliozungumza na Raia Mwema hawana matumaini ya kuwapo maamuzi yoyote ya maana yatakayoweza kukisaidia chama hicho.


  Kukata tamaa kwa baadhi ya wajumbe kunaelezwa kuchangiwa zaidi na hulka ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, ambaye wanamwelezea kuwa ni kiongozi asiyeeleweka, hivyo kuwawia vigumu hata kumsaidia pale inapolazimu.


  "Hakuna jipya, kwa Bwana Mkubwa wetu hatutarajii jipya lolote," anasema Mjumbe mmoja wa NEC alipohojiwa na Raia Mwema kupata undani wa kikao hicho.


  Taarifa za ndani kutoka kwa baadhi ya wajumbe hao wa NEC zinabainisha kuwapo kwa makundi mawili makuu, moja likisimamia maslahi ya taifa na jingine likisimamia maslahi binafsi, na ni kundi hili lenye kusimamia maslahi ya taifa linaloonekana kukatishwa tamaa na hulka ya Mwenyekiti wao ya kutoweka msimamo wake wazi kuhusu kundi la pili linaloundwa na marafiki zake wa karibu.


  "Si rahisi kuwa na maamuzi mazito; tatizo la bwana mkubwa haeleweki. Tunashindwa kumsaidia. Tazama kama suala la Dowans, utadhani hakuna serikali, Waziri mzima (Ngeleja) anaitisha press conference anasema walipwe, Mwanasheria Mkuu wa Serikali naye anasema walipwe, Rais kakaa kimya, Kamati Kuu nayo inakaa inasema ni suala la kisheria, halikwepeki, walipwe, badala ya kufanya siasa nao wanashabikia Dowans kulipwa, sasa unajiuliza bwana mkubwa kasimamia wapi katika suala hili, huwezi kumuelewa," anasema mjumbe mwingine.
   
 2. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #2
  Apr 7, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nilini haswa ili tuanze kufurahia mpasuko wao?
   
 3. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #3
  Apr 7, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,674
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Tutaona!!
   
 4. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #4
  Apr 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Nyerere aliasa zamani, upinzani wa kweli wa CCM utatoka ndani ya CCM. Pia alitoa mfano wa shoka na mti; pale mti unapotumika kuwa mpini wa shoka, iti itaangamia. Sisi letu jicho na vita vya panzi.....
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Apr 7, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Safari hii CCM kamwe haitoweza kuwaambia CCM Zanzibar kitu juu ya ZAMU YAO kuongoza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wala si vinginevyo.

  Hata hivyo nako bado kuna maswali mengi tu maana akina Hussein Mwinyi na Vuai Nahodha endapo watapendekezwa basi nako Zanzibar itakua haijapata mzawa wao maana wote hawa ni watoto wa Tanzania Bara (japo wamezaliwa Zenj) na vijiji vyao vikiwa vinajulikana vema tu kwamba ni kule Kisarawe na Kondoa respectively. Hivyo the search of Zanzibari for Union Presidency on CCM ticket is by itself a hot task on its own right.

  Likewise, the MUST-Be-President Edward Lowassa shall never buy anything short of getting Hon Kikwete's duly signed Presidential Promisory Note that given the amount of money he has since invested in clearing all hurdles for the incumbent, the keys to Magogoni State House MUST-JUST settle on his palm and NOTHING LEAST of all that under the sun.

  The big-eggoed politician would equally seek this position in order to find an opportunity to settle political scores with perceived and real enemies like 6 and posibly do everything posible to make them look tinier than a piriton in the eyes of the public. If not enough, the present group of Mega-Corruption faces certainly only see a future, protection and survival with Lowassa at the helm.

  Sure, things are never any easier with a tomorrow a CCM as Sitta would not just let his past most outstanding pro-citizenry parliamentary performance as the speaker of the National Assembly is such a powerful capital from which carefull political nurturing of presidential ambitions need to be pitched.

  More so, the gentleman enjoys very good rapport far beyond own CCM political party ulike the earlier contenders mentioned above.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Apr 7, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Kama nyoka anaweza kuacha kuwa nyoka kwa kujivua gamba basi CCM yaweza kuwa CCM kwa kujivua gamba lake! Hakuna mabadiliko ya maana yatafanyika katika ngazi ya NEC. Siku CCM ikiitisha Mkutano Mkuu wa kujisafisha ndipo nitaamini kuwa kweli wanataka kuanza upya kwani Chombo cha Juu katika CCM ni Mkutano Mkuu - siyo Kamati Kuu, siyo Halmashauri Kuu!.. Until then.. let the illusion begin!
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Apr 7, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,412
  Trophy Points: 280
  Wacha waparurane tu hawa mafisadi. Kuparurana kwao labda kutaleta ahueni kubwa katika nchi yetu maana matatizo yetu mengi yanasababishwa na hiki chama cha mafisadi/majambazi kuwepo madarakani.
   
 8. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #8
  Apr 7, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,467
  Likes Received: 4,126
  Trophy Points: 280
  Tusubiri tuone kama wana ujasiri huo wa kujisafisha.
   
 9. U

  UNIQUE Senior Member

  #9
  Apr 7, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 180
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu msijifariji CCM ni wasanii wa mkimataifa kwa hiyo subirini muone watakavyoyapangua matatizo hayo.
  unique
   
 10. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #10
  Apr 7, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  A monkey (CCM) can never be a human being in my lifetime. I don't mean to say that Dr Darwin was wrong, but I can prove him wrong on CCM evolution in five years before the 2015 election. CCM will remain a monkey until after 2015.
   
 11. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #11
  Apr 7, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu wewe una matatizo ya kimsingi na inaelekea unashindwa kuona alama za nyakati.
  Wakati Zenj wakiwa busy kujiiimarisha kama a separate entity and finally a sovereign, wewe unaongelea Zenj kutawala Tanganyika?
  Kwa ridhaa ya nani haswa?
  Hilo wazo tu linatia kinyaa.
  Hata CCM ikibomoka(ambacho si kitu kibaya),Zenj waombe tu warudi kwenye Afro Shirazi Party yao ili itawale kisawasawa huko kwao.
   
 12. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #12
  Apr 7, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,345
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Ccm wamekuwa wakipasuka mara kwa mara na kufanikiwa kujiunganisha .......sasa sijui extent ya mpasuko huu ikoje ukilinganisha na mipasuko mingine iliyotangulia.......................labda kwa kuwa wanaotaka mabadiliko ni vijana basi ccm hawana chao tena!
   
 13. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #13
  Apr 7, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Gamba la ccm haliwezi kuvuliwa na vikao halali kwa sababu wajumbe wa vikao hivyo, hasa mkuu wao, ndio gamba lenyewe!

  Kuvua gamba maana yake wajumbe wakubali kwamba wameshiba kutokana na ufisadi, wakubali kustaafu ufisadi kwa hiari. Hili haliwezekani kutokea.

  Gamba la ccm litavuka tu pale mafisadi ndani ya ccm watakapofarakana na kupingana. Watakaoshindwa watajimega. Hivyo ndivyo gamba litatoka, siyo kwa maamuzi ya vikao ikiwa JK bado ni Mkiti wa ccm
   
 14. G

  Godwine JF-Expert Member

  #14
  Apr 7, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Wameua tumaini langu Daima ningependa Makamba nawe mgombea wa urais wa CCM mwaka 2015 makamba ni mtu safi aliyefanikiwa kubadili mfumo wa siasa na kufanya CCM iwe safi na wapinzani wajijenge hakuna mtu muhimu katika siasa za vyama vingi kama makamba kwani pande zote mbili zimenufaika naye Upinzani umejijenga na CCM wameonyesha hitikadi zao za kweli mafisadi wapi na wazalendo wapi...


  Daima tutakukumbuka makamba
   
 15. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #15
  Apr 7, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
   
 16. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #16
  Apr 7, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,445
  Likes Received: 5,831
  Trophy Points: 280
  Makamba wamwondoe 2016 tafadhali.Sisi bado twamtaka awe hapo CCM kati ya sasa na 2015
   
 17. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #17
  Apr 7, 2011
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu please dont insult one of the most brilliant human thinkers EVER by comparing his paradigm shifting idea to the mediocrity that is CCM.
   
 18. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #18
  Apr 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Ubaguzi utawamaliza wazanzibari! Imagine prospect ya mafuta tu katika eneo lenu, tayari mnatamani mtengane na Wadanganyika. Sasa wewe Uwezo Mnao umeingiza wazo la zamu ya urais kwa Wazanzibari wenzio lakini hapohapo umeshaanza kuwatenga Mwinyi Jr. na Nahodha. Umesahau Mkapa alipokuwa anaondoka madarakani mlikuwa na nafasi nzuri sana kwa kumwunga mkona Salim A. Salim na wadananyika wengi wangewaunga mkono pia, lakini ubaguzi wenu dhidi wa wapemba ukamnyima mzee wa watu nafasi. Siwezi kutabiri kwa kuwa sina undugu na Shekhe Yahya Hussein lakini naamini mkipata tiketi ya CCM mtakuwa na wakati mgumu kuwin mioyo ya wadanganyika kwa viongozi kama Karume, Nahodha, Hussein Mwinyi nk.
  Ushauri wangu kwa ndugu wa kizanzibari: Maadam mmeweza kuungana ktk serikali ya Umoja wa Kitaifa na kuongozwa na watu mliowaita wapemba wasiofaa kutawala huko siku za nyuma, nawashauri muondoe vijitabia vya kubaguana hovyohovyo na Mwenyezi Mungu mwenye rehema atawabariki na kubariki juhudi zenu za kutafuta urais.


   
 19. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #19
  Apr 7, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hilo gamba litavuka kweli!! Maana kama kweli hawa jamaa wanataka kuvua gamba wa-Tanzania mjue kutakuwa na uchaguzi mkuu maana mkuu wa kaya ndilo gamba kuu, kwahiyo kulivua ni kutafuta watawala wengine.:rip: CCM
   
Loading...