CCM: Tutajidanganya Hadi Lini?

CCM: Tutajidanganya Hadi Lini?

Mkuu Mchambuzi ,Bandiko lako zuri. Linakosoa, linafundisha na kujenga.

CCM haijaacha kujifunza kutokana na changamoto za muda mrefu na zinazotokea siku baada ya siku.

CCM ina taratibu zake katika kuelimishana, kukosoana na kusahihishana. Huwezi kutaka kuisahihisha na kuikosoa CCM kupitia JF na ikakuona unachokifanya ni sawa. Kama kweli nia yako ni ya kweli kama Mwl Nyerere alivyokuwa, basi ungefuata njia na taratibu zake katika hili.

Sijakubaliana na wewe pale unapo kishutumu chama kama kimeajiri watu maalum kwa kazi za kwenye mitandao wakati hauna kidhibiti halisia kama ni kweli. Kubezwa na kukejeriwa kunatoka kutokutumia njia sahihi katika kufikisha ujumbe kwa chama. Kwa nini utumie JF wakati kuna vikao mbadala kwa maswala haya?.

Kama unavyopenda kutoa ushauri ili ufanyiwe kazi na CCM, vile lazima ukubali kama kuna kundi la watu pia wanaweza wakaona ushauri wako haufai na wakatoa angalizo lao kulingana na jinsi wanavyofikiria kama jinsi ulivyofikiria kwenye ushauri wako. Kufanya hivyo haimaanishi kuwa wametumwa na CCM.

Kumchagulia mtu kundi la kisiasa isikushangaze na wewe pale watakapo kuchagulia kundi la kisiasa. Unapowasema wametumwa na CCM, kwa nini basi unashangaa wanapokuambia pia kama umetumwa na CHADEMA.

Unfortunate, Kama hizi criticism kutoka upande wa CCM zinakupeleka kufikilia kwamba CCM inatuma watu, jaribu kubandika bandiko ambalo liko against CHADEMA ili uonje joto ya jiwe kupata uharisia ya fikra za Watanzania linapokuja swala la mapenzi kwa vyama vya siasa kupitia mitandao.

Ningependa kujadili hoja zako kuu hapo juu kama ifuatavyo:

Kwanza mimi sio kiongozi wa ngazi yoyote ndani ya chama na sina nia ya kutafuta uongozi wowote kupitia chama cha mapinduzi katika siku zijazo, lakini ninaendelea kuwa mwanachama hai wa ccm na ni katika hali hii ndio natoa dukuduku na maoni yangu kama mwanachama mwingine yoyote; Zamani kulikuwa na utaratibu wa wanachama kukaa vikao na kujadili mambo mbalimbali including changamoto za chama,lakini kwa ufahamu wangu na nadhani wako pia, utaratibu huo haupo tena katika zama hizi, sana sana wanachama mtaitwa kwenye mikutano ya hadhara kusikiliza hotuba za viongozi,siku inaisha, unless mwenzangu una taarifa ambazo mimi sina; Ni kwa mantiki hii, sioni tatizo lolote mimi kuja humu JF na kujadiliana na wanachama wenzangu kama tunavyofanya kwenye vikao vyetu vya kahawa na kashata mitaani kila tunapopata wasaa huo; Kumbuka, TANU ilizaliwa mitaani, kwahiyo katika zama hizi,hata vikao vya mitaani vinavyohusishwa wanachama mbalimbali kubadilishana mawazo KWA KUAMBIANA UKWELI,sidhani kama ni sahihi kutotambua vikao vyetu kama vikao visivyo rasmi; ulitaka viongozi wawepo kwanza ndio vikao vyetu kama wanachama vitambulike kama vikao rasmi? tupo wengi sana ambao bado tunaipenda ccm kutokana na misingi yake na ambao tuna amini kwamba bado chama kina potential kubwa ya kutatua matatizo ya wananchi kupitia viongozi bora na sio bora viongozi ingawa such potentials are getting smaller kila jua linapozama; kama viongozi wana nia ya kujua dukuduku letu wanachama, watutafute, tupo vijiweni kila siku tunaongea haya huku tukicheza bao na drafti; vinginevyo kama wanachama, hatuoni umuhimu wa kutafuta viongozi eti kuwapa dukuduku zetu huku tukijua wana mlima wa ahadi ambazo hawajazitekeleza; Watufuate kama mwalimu alivyofanya mara tu baada ya uhuru alipomwachia kawawa uongozi wa nchi na kwenda kwa wananchi kwa mwaka mzima kukaa nao, kulala wanapolala, kuamka na kunywa nao chai na kupiga nao soga; hivyo ndivyo alivyobaini changamoto za TANU na kutambua kwamba bila ya azimio la arusha,mtanzania wa kijijini hatopata maisha bora;

Suala la pili la kujadili linahusiana na hoja yako kwamba sina ushahidi na hoja zangu kwamba wachangiaji fulani fulani wanalipwa kuja kusema mazuri tu ya ccm na kuponda wale wote wanaokosoa chama kama mimi ninavyofanya; Sielewi kama nia yako hapa ni kunitaka nilete ushahidi au nia yako kuongezea nguvu hoja za wengine kwamba mchambuzi ni chadema;Pia unashauri nije na bandiko la kukosoa chadema nione cha moto; Kwanza, iwapo wewe ni mfuatiliaji mzuri wa jukwaa hili, nimekuja na mada nyingi tu za kuikosoa chadema, na unaweza tembelea mada hizo kupitia profile yangu humu ujionee mwenyewe; lakini kwa vile huwa najadili mapungufu ya chadema kwa hoja, mara nyingi mijadala huwa ni mizuri na ya kutuelimisha sana;

Vinginevyo naomba nikueleze tu kwamba, either way, mchambuzi ni mtu mdogo sana, lakini iwapo anasema ukweli na hafanyi fitina, baso yupo ndani ya kanuni muhimu ya chama isemayo kwamba "NITASEMA UKWELI DAIMA FITINA KWANGU MWIKO." Hata siku moja, ukweli hauwezi badilika kuwa uongo na uongo hauwezi kubadilika kuwa ukweli; Mwalimu nyerere Katika kitabu cha ‘TUJISAHIHISHE' (1962) anasema:

["Ukiondoa matatizo wayapatayo binadamu kwa sababu kama mafuriko, nzige, kiangazi, n.k, matatizo yao mengi hutokana na unafsi. Unafsi ni wa aina nyingi. Swali ambalo twalisikia mara kwa mara, "Hali yetu ya baadae itakuwaje?", ni swali ambalo sina shaka kuna wanaouliza kwa nia safi kabisa. Lakini mara nyingi linatokana na unafsi. Mtu anayeuliza anafikiri TANU iliundwa kwa faida yake binafsi. Ni kama kwamba TANU ilipoundwa ilimwahidi kwamba ikiwa atakubali kuwa mwanachama, au kiongozi, basi TANU itamfanyia yeye jambo fulani kama tunzo! Anasahau kabisa kuwa TANU inajishughulisha na haja za Jumuiya kwa ujumla. Lakini kwa mtu wa aina hiyo, hata kama TANU inatimiza madhumuni yake kwa jumuiya, ataona kuwa ni umoja ambao hauna maana kwa sababu haumtimizii haja zote za nafsi yake. Huu ni unafsi. Kama wanachama wa TANU, na hasa viongozi, hawatakihukumu chama chetu kwa mahitaji na nafsi zao wenyewe, chana hakitadumu. Wanachama wa aina hiyo ni ugonjwa katika chama.

Dalili nyingine ya unafsi, na ambayo ni ugonjwa mbaya sana ni fitina. Kanuni moja ya TANU inasema hivi: "Nitasema Ukweli Daima. Fitina Kwangu ni Mwiko." Lakini bado tunao wanachama ambao ni wafitini wakubwa bila kujitambua. Ni wa aina mbali mbali. Wengine humwona mwenzao anafanya kosa. Badala ya kumwambia pale pale kijamaa kwamba atendalo ni kosa, watanyamaza kimya. Lakini hawanyamazi kabisa. Watakwenda kumteta katika vikundi vya siri. Mateto haya si ya kumsaidia mwenzao, ni ya kumdhuru. Hii ni aina moja ya fitina. Wengine hugawa watu katika mafungu. "Fulani" japo kafanya kosa kubwa sana hasemwi. Lakini "Fulani" wa pili akifanya kosa japo dogo, kosa lile hukuzwa likawa kama mlima Kilimanjaro. Hawa hutafuta sababu ya kumtetea "Fulani" wa kwanza, au za kumaulumu "Fulani" wa pili, ambazo hazifanani kabisa na ukweli. Kwa watu wa aina hii, ukweli ni jambo ambalo hutegemea mtu, si kitu kinachojitegemea chenyewe bila kujali mtu. "Fulani" wa kwanza akisema katika majadiliano kuwa mbili na mbili ni tano, wao watakubali. Lakini "Fulani" wa pili akisema sivyo, mbili na mbili ni nne, watamwona ni mtu mbaya kabisa ambaye hastahili hata kusikilizwa. Hawa hawajali ukweli, hujali nafsi tu. Kwao, ukweli ni maoni yao na matakwa yao. Hatuna budi, hasa katika majadiliano na mazungumzo yanayohusu jumuiya, tujifunze kusikiliza hoja zenyewe zinazotolewa na wenzetu, na kuzijibu zile hoja kwa kuzikubali au kuzikataa, bila kujali kama anaezitoa ni rafiki au si rafiki. Pia wanaopingwa hawana budi wakubali kuwa kinachopingwa ni zile hoja zao, sio wao wenyewe. Bila mazoea haya, mazungumzo hayana maana; yanakuwa ni kupoteza wakati, maana huwa tumekwisha kuzihukumu hoja za mtu hata kabla hajazitamka; kadhalika, hoja zetu zikijibiwa kwa kupingwa halafu tunawakasirikia waliozipinga tunafanya mazungumzo yasiwe na maana, kwa sababu tunapenda hoja zetu zikubaliwe tu hata kama si hoja safi.

Ukweli una tabia moja nzuri sana. Haujali mkubwa wala mdogo; haujali adui wala rafiki. Kwake, watu wote ni sawa. Pia ukweli unayo tabia ya kujilipiza kisasi kama ukipuuzwa. Ukiniona nataka kulipiga teke jiwe kwa kuwa unafikiri kuwa ni dongo au mpira, natumaini utanionya. Lakini nikilipuuza onyo lako kwa sababu eti wewe ni mdogo au kwa sababu sikupendi, nikalipiga teke, basi litanivunja dole japo ningekuwa nani.Ukweli haupendi kupuuzwa.
Wakati mwingine, mtu tunayempinga huwa ana makosa kweli lakini hoja tunazozitoa ni za kinafsi na hazihusiani kabisa na hoja zake. Nikisema mbili na tatu ni sita, nakosa. Lakini ni bora kunionyesha kwamba pengine nafikiri tunazidisha kumbe tunajumlisha. Ni kweli mbili mara tatu ni sita; lakini mbili na tatu ni tano, siyo sit.a Lakini ukijaribu kuwashawishi wenzetu wakatae mawazo yangu na kukubali yako kwa kusema kuwa meno yangu ni machafu, au natoa kamasi daima, utakuwa unatumia hoja ambazo hazina maana. Huu ni mfano wa upuuzi; lakini mara nyingi hoja tunazotumia kuwashawishi watu wakatae mawazo ya wale tusiowapenda, au kukubali mawazo yetu, huwa hazihusiani kabisa na mambo tunayoyajadili.

Makosa yetu mengine hutokana na woga; woga unaotuzuia kumlaumu mkubwa japo tunajua kuwa kakosa, au unaotuzuia kumtetea mdogo anayelaumiwa na wakubwa japo tunajua hana makosa. Na msingi wa woga ni unafsi. Pengine huwa tunaogopa sisi wenyewe kulaumiwa au kupata hasara fulani. Pengine twaweza kuwa hatuna cheo chochote ambacho tunaogopa kupoteza; pengine huwa hatuna tamaa yoyote ya kupata cheo fulani. Lakini woga unaweza kutokana na tamaa ya kila binadamu kupendwa na binadamu wenzake. Sisi sote tunayo tama hii, au sivyo tusingekuwa binadamu. Woga huu huweza kumfanya mtu kuvumilia maovu, hasa kama maovu yale yanatendwa na walio wengi kwa walio wachache, au yanatendwa na wakubwa kwa wadogo. Kwa kuogopa kuwaudhi wengi tunawaacha watende makosa bila kuwasahihisha, wasije wakatuchukia. Huu ni unafsi mbaya sana Ni kweli kwamba demokrasi haiwezi kudumu ikiwa wachache watakubali matakwa ya wengi. Lakini matakwa ya wengi hujulikana katika majadiliano au mazungumzo wa wazi.

Kadhalika, matakwa ya wachache hujulikana katika majadiliano na mazungumzo. Bila wachache kusema wazi wazi matakwa yao, majadiliano hayana maana. Wakati mwingine, hata baada ya majadiliano, wachache – japo wamekubali kutii uamuzi wa wengi wanaweza kuendelea kuamini kwamba mawazo yao ni sawa, na ya walio wengi yamepotoka. Demokrasi inawapa haki, na ukweli unawapa wajibu wa kuendeleza mawazo yao mpaka wengi waone kuwa ni ya kweli. Bila hivyo Maendeleo katika mawazo hayawezekani, kwani mara nyingi wazo zuri hutokana na mtu mmoja tu. Mwanzo laweza likapingwa, pengine kwa nguvu kabisa, na walio wengi, lakini hatimaye wengi hulikubali. Huu ndio msingi wa Maendeleo katika mawazo ya binadamu.

Makosa ni makosa na dhuluma ni dhuluma, japo watendao makosa hayo au dhuluma ile ni wakubwa au ni wengi. Chama kinachopenda ukweli na haki hakina budi kiwape wanachama wake uhuru na nafasi ya kusahihisha makosa na kuondoa dhuluma. Wanachama hawana budi waone kuwa ni wajibu wao kuutumia uhuru huo, na nafasi hiyo. Wanachama wasiotumia uhuru huo na nafasi hiyo, kwa sababu ya kuogopa kuchukiwa au kupoteza nafasi zao, wanafanya kosa kubwa la unafsi, ambalo ni adui wa haki na ukweli.

Kosa jingine linalotokana na unafsi tunalifanya wakati wa kuchagua viongozi. Wakati mwingine hufanywa na wanachama; wakati mwingine hufanywa na viongozi wenyewe, au wale wanaotaka uongozi. Nimesema mahali pengine kwamba viongozi wetu hawana budi watokane naWATU. Viongozi wa TANU hawana budi watokane na wanachama wa TANU wenyewe, bila hila, vitisho, rushwa, au ujanja wa aina yoyote.Lakini mara nyingi wanachama huchagua viongozi bila kufikiri kwa makini kama viongozi hao wanaiweza, au hawaiwezi, kazi wanayochaguliwa kufanya. Wanachama wetu watafanya makosa makuwa sana ikiwa watachagua viongozi wa ovyo tu. Hii ni jambo la hatari kwa demokrasi na chama chetu, na maadui wa TANU wanaweza kusema kwamba demokrasi haina maana kwa sababu haizai viongozi wanaoweza kazi zao. Hii ni kweli, maana wote twajua kwamba demokrasi inaweza kuchagua viongozi wazuri. Lakini ni wajibu wetu katika kuhifadhi demokrasi kuona inachagua viongozi ambao wanaziweza kazi zao. Kazi za kuchagua viongozi ni kazi ya wanachama wetu; lakini viongozi wetu wanaweza kusaidia kwa kuelezea wanachama wetu kwamba jambo la kuchagua viongozi ni kubwa sana. Haifai kuchagua kiongozi kwa sababu ni mjomba, au binamu au ana sauti au sura nzuri. Wala haifai kuacha kumchagua mtu kuwa kiongozi kwa sababu kama hizo. Jambo kubwa ni kuchagua kiongozi mwenye tabia nzuri na anayeiweza kazi. Hatuna budi tutii kanuni hii katika kuajiri wafanya kazi katika TANU au Serikalini. Hawa pia hawana budi wachaguliwe kwa sababu wanaiweza kazi wanayoajiriwa kufanya, na ni watu wenye tabia nzuri.

Kosa jingine ni kutojielimisha. Kanuni yetu moja inasema: "Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu wote na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote". Wengi wetu hufikiri kuwa kujielimisha ni kwenda Kivukoni, au kupata nafasi kwenda kusoma katika nchi za nje. Wengine hufikiri kuwa kujielimisha ni kujua kusoma na kuandika. Hilo ni kosa, lakini sio kubwa kama la pili. Wengi wetu, hasa baadhi ya viongozi, hufikiri kuwa tunajua kila kitu na hatuna haja ya kujifunza jambo lolote zaidi. Mtaalamu mmoja wa zamani alisema kuwa "mwanzo wa elimu ni kutambua kuwa haujui kitu."]


Mwalimu Nyerere, Tujisahihishe, kurasa 1- 4, May 1962.
 
Mchambuzi,

Umeshasema mara nyingi kwamba CCM imara itategemea na uimara wa Chadema.

Kama hilo gari ambalo na wewe umepanda linasuasua kiasi hicho kwanini usishuke ukasukuma?

Inakuwaje na wewe unajaribu kusukuma hilo gari bovu ilihali na wewe umekaa humo humo ndani? Kwa nini usitoke humo ili ulisaidie liwake?
 
Vinginevyo naomba nikueleze tu kwamba, either way, mchambuzi ni mtu mdogo sana, lakini iwapo anasema ukweli na hafanyi fitina, baso yupo ndani ya kanuni muhimu ya chama isemayo kwamba "NITASEMA UKWELI DAIMA FITINA KWANGU MWIKO." Hata siku moja, ukweli hauwezi badilika kuwa uongo na uongo hauwezi kubadilika kuwa ukweli; Mwalimu nyerere Katika kitabu cha ‘TUJISAHIHISHE' (1962)
Mkuu Mchambuzi ,
Ninashukuru kwa kujibu bandiko langu na pia ninashukuru kwa maelezo yako pamoja na kwamba bado kuna sehemu tunashindwa kukubaliana.

Kama unavyobainisha kuwa muundo wa CCM ni mzuri ila utekelezaji wake unasuasua. Lakini pia kumbuka uongozi wa CCM unaanzia kwenye kaya ambapo huko ndiko mikutano ya chama inapoanzia. Kama unaweza kukaa kwenye kahawa na kujadiliana mstakabali wa CCM, kitu gani tena kinashindikana kukaa katika kikao cha nyumba kumi na kuongelea matatizo yanayokikabili chama. Nyerere aliamua kwenda kwa wananchi kusikiliza matatizo yao kwa bile kipindi hicho chama hakikuwa na safu ya viongozi, ofisi, watendaji na uelewa kama chama kilivyo kwa sasa.

Siwezi kukubaliana na wewe kama kutoa ushauri kuhusu CCM imebaki ni kwenye vijiwe na kwenye mitandao kwa vile utaratibu uliokuwapo haupo tena!. siwezi kuamini kama JF ni last lesort kwako otherwise, kuna tatizo lingine.

CCM haikuundwa au haifanyi kazi pale tu viongozi wa juu wanapotembelea eneo lako. Chama kina wajumbe wa nyumba kumi wanaobeba matatizo ya "watu wadogo" kama wewe na kuyapeleka kwenye vikao vinavyohusika. Nitaikubali statement yako, ukisema muundo wa CCM haupo tena achilia mbali utekelezaji wa shughuri zake za kila siku.

Mkuu, hivi umeshaangalia mazingira ya kisiasa nchini, kwa maana ya siasa zinazoendeshwa katika vyama na upeo wa wananchi kisiasa na ukajiuliza kwa nini watu wanakukejeri na kukurushia matusi pale unapotaka kukisahihisha chama kupitia majukwaa ya wazi kama JF, halafu pia ukajiuliza, kwa nini watu wanaonipongeza na kunishangilia hapa JF kila ninapoikosoa na kuitaka CCM ijisahihishe wengi wao ni wapinzani wa CCM?.
 
Last edited by a moderator:
mkuu umetumia mwezi mzima kuandika hii makala , amabayo imenichukua dakika mbili, kuona ni ya kijinga...

Amewataja nyie kwenye uchambuzi. Najua inauma sana. Lakini huyo ndio CCM wa ukweli. Nyie ni CCM-Maslahi period!!!!
 
Mkuu Mchambuzi ,
Ninashukuru kwa kujibu bandiko langu na pia ninashukuru kwa maelezo yako pamoja na kwamba bado kuna sehemu tunashindwa kukubaliana.

Kama unavyobainisha kuwa muundo wa CCM ni mzuri ila utekelezaji wake unasuasua. Lakini pia kumbuka uongozi wa CCM unaanzia kwenye kaya ambapo huko ndiko mikutano ya chama inapoanzia. Kama unaweza kukaa kwenye kahawa na kujadiliana mstakabali wa CCM, kitu gani tena kinashindikana kukaa katika kikao cha nyumba kumi na kuongelea matatizo yanayokikabili chama. Nyerere aliamua kwenda kwa wananchi kusikiliza matatizo yao kwa bile kipindi hicho chama hakikuwa na safu ya viongozi, ofisi, watendaji na uelewa kama chama kilivyo kwa sasa.

Siwezi kukubaliana na wewe kama kutoa ushauri kuhusu CCM imebaki ni kwenye vijiwe na kwenye mitandao kwa vile utaratibu uliokuwapo haupo tena!. siwezi kuamini kama JF ni last lesort kwako otherwise, kuna tatizo lingine.

CCM haikuundwa au haifanyi kazi pale tu viongozi wa juu wanapotembelea eneo lako. Chama kina wajumbe wa nyumba kumi wanaobeba matatizo ya "watu wadogo" kama wewe na kuyapeleka kwenye vikao vinavyohusika. Nitaikubali statement yako, ukisema muundo wa CCM haupo tena achilia mbali utekelezaji wa shughuri zake za kila siku.

Mkuu, hivi umeshaangalia mazingira ya kisiasa nchini, kwa maana ya siasa zinazoendeshwa katika vyama na upeo wa wananchi kisiasa na ukajiuliza kwa nini watu wanakukejeri na kukurushia matusi pale unapotaka kukisahihisha chama kupitia majukwaa ya wazi kama JF, halafu pia ukajiuliza, kwa nini watu wanaonipongeza na kunishangilia hapa JF kila ninapoikosoa na kuitaka CCM ijisahihishe wengi wao ni wapinzani wa CCM?.

Sawa mkuu, mimi na wenzangu wa vijiwe vya kahawa tutaanza kuwatafuta hao viongozi wa kaya unaopendekeza, viongozi ambao umuhimu wao kwa viongozi wa juu huwa ni nyakati za kura za maoni kutafuta wagombea ubunge na udiwani kuelekea chaguzi kuu; Na hii ni kwasababu wanachama wa ccm hawapo ngazi ya taifa, mkoa au wilaya bali kwenye kata huku wajumbe wa nyumba kumi kumi ndio wakiwa ni nguzo kuu ya kura zao; Pia ujue kwamba katika vikao vyetu vya kahawa kujadili chama, wapo wajumbe wa nyumba kumi kumi wengi tu wanaoeleza jinsi gani uongozi wa chama hauwathamini nje ya vipindi vya uchaguzi;

All that said and done, kufuata ushauri wako haina maana kwamba nitaacha kujadiliana na wanachama wenzangu na wananchi kwa ujumla juu ya changamoto za chama humu JF, hasa iwapo umuhimu wa tekinolojia kama hii ni kufanikisha ufanisi wa masuala kama haya on an any time, any location basis;

Vinginevyo tumeona viongozi wengi wa ccm wakija humu an kwenda facebook kujenga hoja zao nje ya utaratibu wa kutumia vikao, sasa kwanini na sisi wanachama tusitumie tekinolojia hii kufikishiana ujumbe tunaokusudia?

Tafakari...

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
People like Mchambuzi ni wachache sana Tanzania... na bahati mbaya sana huwa hawakubaliki na watawala na hawaeleweki na wapiganaji!!!

but, when the dust is settled, we will go back to these analyses, pretend as if they were never there and say WOW!!!

I wish JF is archiving these kinds of publications and release them as special editions 10-20 years down the road
Actually, JF Mods inabidi waaanze sasa kufikiria kuanzisha Special publications kutoka kwenye hii michango ya members. Na mfano mmojawapo wa Journal ni hili bandiko, I tell you someone may graduate with this thread if at all he/she can add some staff.
 
Ndugu yangu Mchambuzi kutoka Mtaa wa Ufipa Kinondoni Zipo aina tatu za Propaganda
1.Yellow
2.Black
3.White
Wewe upo namba 2,ni propaganda ya adui kujivika sura ya kirafiki na akakushauri!
Binafsi nimekugundua unatoka Mtaa wa Ufipa kwenye nyumba ya kupanga Kinondoni,washauri viongozi wako wa Chadema ambao naamini baadhi ni vichaa kama Godbless Lema,Dr Slaa ambae juzi alitaka kumzoea Profesa Baregu akampiga stop!
avatar32492_5.gif
 
Ndugu yangu Mchambuzi kutoka Mtaa wa Ufipa Kinondoni Zipo aina tatu za Propaganda
1.Yellow
2.Black
3.White
Wewe upo namba 2,ni propaganda ya adui kujivika sura ya kirafiki na akakushauri!
Binafsi nimekugundua unatoka Mtaa wa Ufipa kwenye nyumba ya kupanga Kinondoni,washauri viongozi wako wa Chadema ambao naamini baadhi ni vichaa kama Godbless Lema,Dr Slaa ambae juzi alitaka kumzoea Profesa Baregu akampiga stop!

Mkuu, inamaana zile allowance za Lumumba hazitoshi Kukufanya uache kutumia Kuberi Asubuhi kama Breakfast???
 
Asante sana Mchambuzi kwa makala nzuri sana yenye tathmini ya hali ya juu kuhusu nchi yetu na mahali tulipofikia kutokana na uongozi mbovu wa ccm. Ninapenda kuiita ccm (ya jk) nikiitofautisha na CCM (ya Mwalimu).

Ni ukweli uisopingika ya kuwa ccm imegeuka saratani, inajimaliza yenyewe na pia inamaliza na chembechembe za uhai zingine zilizo karibu na chama hicho. Kama ilivyo saratani, bila ya kufanya maamuzi magumu ya kukata kabisa kiungo chenye saratani na kuitibu kwa dawa kali na mionzi, maisha hupotea. Inafurahisha sana kuona ya kwamba katika vuguvugu hili la ukombozi wa mtanzania bado kuna watu kama wewe ambao wako tayari kusimama na kueleza ukweli bila woga. Ninaamini kabisa ya kuwa wapo wengine ndani ya cccm ambao wanayaona haya, lakini kutokana na woga hawako tayari kutamka hadharani. Wamekubali kuendelea kupiga makofi, kuvaa mashati ya kijani na kuwaziba midomo wote wanaotaka kusema ukweli kwa kuwa maslahi yao binafsi wameyaweka mbele kuliko maslahi ya Taifa.

Endelea kutuchambulia Mchambuzi, yaweke hadharani yaliyofichwa maana siku inakuja, na haiko mbali ambapo wadhalimu wote watajibu mbele ya watoto na wajukuu zetu!

Mungu Ibariki Tanzania!
 
Mzee mchambuzi bahati mbaya kubwa mtu anapokaribia kufa au akiwa katika hatua ya kukata roho hata mnapomuombea dua au maombi kwa mola wake ampe nafuu ili aweze kuamka na kuendelea na maisha au afe vizuri akiwa ametubu madhambi yake huwa haelewi hajitambui lakini hiyo isitukatishe tamaa kumuombea mgonjwa wetu huyu kwani kuna mawili yatatokea 1.aidha atapona na kijirudi au atakufa akiwa ametubu madhambi na madhila makubwa aliyowafanyia wenzake wakati wa uhai wake.
 
Chama hakiko ktk kutetea maslahi ya wananchi anymore, ni Matumbo ya wajanja wachache yanayofaidika (VINANA), vijana wengi humu JF wanalipwa peanuts..kuja kuharibu mijadala ya kitaifa. Hali inatisha CCM badala ya kuwaletea maisha bora wananchi inatumia njia chafu kujilinda na challenge inazopata kila kona. RIP CCM
 
Sawa mkuu, mimi na wenzangu wa vijiwe vya kahawa tutaanza kuwatafuta hao viongozi wa kaya unaopendekeza, viongozi ambao umuhimu wao kwa viongozi wa juu huwa ni nyakati za kura za maoni kutafuta wagombea ubunge na udiwani kuelekea chaguzi kuu; Na hii ni kwasababu wanachama wa ccm hawapo ngazi ya taifa, mkoa au wilaya bali kwenye kata huku wajumbe wa nyumba kumi kumi ndio wakiwa ni nguzo kuu ya kura zao; Pia ujue kwamba katika vikao vyetu vya kahawa kujadili chama, wapo wajumbe wa nyumba kumi kumi wengi tu wanaoeleza jinsi gani uongozi wa chama hauwathamini nje ya vipindi vya uchaguzi;

All that said and done, kufuata ushauri wako haina maana kwamba nitaacha kujadiliana na wanachama wenzangu na wananchi kwa ujumla juu ya changamoto za chama humu JF, hasa iwapo umuhimu wa tekinolojia kama hii ni kufanikisha ufanisi wa masuala kama haya on an any time, any location basis;

Vinginevyo tumeona viongozi wengi wa ccm wakija humu an kwenda facebook kujenga hoja zao nje ya utaratibu wa kutumia vikao, sasa kwanini na sisi wanachama tusitumie tekinolojia hii kufikishiana ujumbe tunaokusudia?

Tafakari...

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums


Watakusikiliza lakini? Hata kama utakuwa na nia njema kabisa katika haya unayoyasema huku nje ya vikao. Kama hu-fit katika agenda yao nakuapia utaaandika weee, yataingia sikio moja na kutokea upande wa siko la pili. Nipo hapa!
 
Mchambuzi,

Umeshasema mara nyingi kwamba CCM imara itategemea na uimara wa Chadema.

Kama hilo gari ambalo na wewe umepanda linasuasua kiasi hicho kwanini usishuke ukasukuma?

Inakuwaje na wewe unajaribu kusukuma hilo gari bovu ilihali na wewe umekaa humo humo ndani? Kwa nini usitoke humo ili ulisaidie liwake?

Mh!mkuu,hili nalo neno!
 
Back
Top Bottom