CCM: Tutajidanganya Hadi Lini?

CCM: Tutajidanganya Hadi Lini?

Dah we jamaa una akili aisee!
Kama unatendaga kama unavyofikiri bado Taifa lina think tanks nyingi
Mungu akupe uhai Mchambuzi

Hilo gazeti naweza pata scanned copy?
Sina uhakika kama ameshachapisha kwenye gazeti, maana nafikiri ndiyo tunamshauri tu achapishe. Akifanya hivyo itasaidia sana kupeleka hii elimu kwa watanzania wengi ambao hawaingii JF.
 
Ndugu yangu Mchambuzi kutoka Mtaa wa Ufipa Kinondoni Zipo aina tatu za Propaganda
1.Yellow
2.Black
3.White
Wewe upo namba 2,ni propaganda ya adui kujivika sura ya kirafiki na akakushauri!
Binafsi nimekugundua unatoka Mtaa wa Ufipa kwenye nyumba ya kupanga Kinondoni,washauri viongozi wako wa Chadema ambao naamini baadhi ni vichaa kama Godbless Lema,Dr Slaa ambae juzi alitaka kumzoea Profesa Baregu akampiga stop!
Wewe unataka propaganda rangi gani!
 
Sina uhakika kama ameshachapisha kwenye gazeti, maana nafikiri ndiyo tunamshauri tu achapishe. Akifanya hivyo itasaidia sana kupeleka hii elimu kwa watanzania wengi ambao hawaingii JF.

Mi sipendagi siasa ila sijui kwa nini imenivutia hata nimeitengeneza katika PDF kwa wanaopenda Invisible unaweza iweka katika post ya kwanza baada ya Mchambuzi kuridhika na "mabadiliko" niyoyoifanyia.
Nimeweka paragraph vizuri na baadhi ya sehemu nimeweka nukta badala ya semi colon na Quotation katika italic!
 

Attachments

Last edited by a moderator:
Wapi Chris Lukosi, Ritz na Chama!?

Atachangia tu thread zenye paragraph moja??
 
ZeMarcopolo naona unagonga likes kwa great thinkers wa CCM kama stroke.

Nilitegemea busara zako japo kwa mistari miwili juu ya maudhui ya bandiko hili
 
Last edited by a moderator:
Ndugu yangu Mchambuzi kutoka Mtaa wa Ufipa Kinondoni Zipo aina tatu za Propaganda
1.Yellow
2.Black
3.White
Wewe upo namba 2,ni propaganda ya adui kujivika sura ya kirafiki na akakushauri!
Binafsi nimekugundua unatoka Mtaa wa Ufipa kwenye nyumba ya kupanga Kinondoni,washauri viongozi wako wa Chadema ambao naamini baadhi ni vichaa kama Godbless Lema,Dr Slaa ambae juzi alitaka kumzoea Profesa Baregu akampiga stop!
Ninapenda kuwa against na wewe.
Ninapenda kuamini kwamba Mchambuzi yupo katika sura anayotaka kutuonyesha yeye,kwamba yeye ni Mwana CCM anayekerwa na njia za CCM,na anajitahidi kuonyesha madhaifu yooote ya CCM mbele ya Kadamnasi,kwa lengo la kuisaidia CCM ijirekebishe.
Ningemuomba jambo moja,kwamba kwa sababu nchi hii sio ya CCM,bali ni Wananchi wote,na ni ya Vyama vyote vya Siasa....ambavyo vinaweza kuja kushika dola,na pia ambavyo Siasa zao ni ACTIVE na zina influence kubwa katika maisha yetu hata LEO,basi aweze kuja na Uchambuzi mwingine murua ili kuvisaidia hivyo vyama pia kuweza kujirekebisha na kufanya mambo yaliyo vema kabisa(ama ni kwamba anasema vyama vingine havimhusu?ama ni kwamba hajui details za vyama vingine?----sidhani kama anaweza ku discuss kwa ubora hivyo kuhusu madhara ya siasa za CCM,huku akiwa sio insider wa CCM,ati atashindwa kudiscuss kwa ubora kuhusu siasa za vyama vingine,wakati sio insider)
Chambua chambua Mchambuzi...lakini usiwe mchoyo kuchambua ya "Chama chako tu"...chambua na ya vyama vingine ili tuwe na Siasa bora
 
Well unbiased analysis mchambuzi. Una muono na IQ ya juu sana ya uchambuzi. Nadhani wengi tunajifunza mengi sana kupitia makala zako ingawa wahenga wanasema 'Many people are being advised but only few become benefited from such advisory'
 
Niko busy lakini nilipoanza kuusoma huu uzi nimelazimika kumaliza. This is the kind of analysis that informs and educates. Mkuu umeelezea vyema, na ni ushauri mzuri sana kwa CCM na wanalumumba. Big up brother!! and thanks for the very useful thread
 
People like Mchambuzi ni wachache sana Tanzania... na bahati mbaya sana huwa hawakubaliki na watawala na hawaeleweki na wapiganaji!!!

but, when the dust is settled, we will go back to these analyses, pretend as if they were never there and say WOW!!!

I wish JF is archiving these kinds of publications and release them as special editions 10-20 years down the road
 
Mkuu Mchambuzi ,Bandiko lako zuri. Linakosoa, linafundisha na kujenga.

CCM haijaacha kujifunza kutokana na changamoto za muda mrefu na zinazotokea siku baada ya siku.

CCM ina taratibu zake katika kuelimishana, kukosoana na kusahihishana. Huwezi kutaka kuisahihisha na kuikosoa CCM kupitia JF na ikakuona unachokifanya ni sawa. Kama kweli nia yako ni ya kweli kama Mwl Nyerere alivyokuwa, basi ungefuata njia na taratibu zake katika hili.

Sijakubaliana na wewe pale unapo kishutumu chama kama kimeajiri watu maalum kwa kazi za kwenye mitandao wakati hauna kidhibiti halisia kama ni kweli. Kubezwa na kukejeriwa kunatoka kutokutumia njia sahihi katika kufikisha ujumbe kwa chama. Kwa nini utumie JF wakati kuna vikao mbadala kwa maswala haya?.

Kama unavyopenda kutoa ushauri ili ufanyiwe kazi na CCM, vile lazima ukubali kama kuna kundi la watu pia wanaweza wakaona ushauri wako haufai na wakatoa angalizo lao kulingana na jinsi wanavyofikiria kama jinsi ulivyofikiria kwenye ushauri wako. Kufanya hivyo haimaanishi kuwa wametumwa na CCM.

Kumchagulia mtu kundi la kisiasa isikushangaze na wewe pale watakapo kuchagulia kundi la kisiasa. Unapowasema wametumwa na CCM, kwa nini basi unashangaa wanapokuambia pia kama umetumwa na CHADEMA.

Unfortunate, Kama hizi criticism kutoka upande wa CCM zinakupeleka kufikilia kwamba CCM inatuma watu, jaribu kubandika bandiko ambalo liko against CHADEMA ili uonje joto ya jiwe kupata uharisia ya fikra za Watanzania linapokuja swala la mapenzi kwa vyama vya siasa kupitia mitandao.
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi ee, hebu nisikilize mdogo wangu; ngoja leo niongee nawe kama kaka anavyoongea na mdogo wake. sikio la kufa huwaga halisikii dawa. hama! achana na hawa watu.

Wewe utakuwa mwanaCCM bora kuliko sisi? tuliokuwa tunapewa mafunzo miezi kibao? achana nao. sijui nikutajie tu namba yangu ya kadi? mimi nilikuwa mwanachama wa ccm kata ya ndugumbi sasa nikwambie. achana nao, sikio la kufa halisikii dawa!!!
 
Ngurumo unaweza kuzungumza na Mchambuzi hii makala itundikwe Tanzania Daima?
Ningefurahi kuiona na Raia Mwema
 
Last edited by a moderator:
Kuishauri ccm ni kupoteza muda wako.
Kama wanamtetea Kinana we hushangai.
 
Hii makala/uchambuzi ni kwa walio timamu wanaopenda mijadla raisi na ya kipuuzi huwezi kuwaona hapa!!!!!!!!!! Lakini ukweli ukisemwa unatabia ya kujidhirisha ngoja tuendelee kusubiri!!!!!!!!!!
 
Leo Nyerere angeitwa mchochezi! Haya maneno hapa chini ni mazito saaaaaana hasa kipindi kama hiki!

"Unless these people are fools. Many in these countries are fools, to accept being ruled just like that. To be oppressed just like that when they have the force in numbers, they are fools. So Tanzanians would be fools, ******, if they continued to accept to be oppressed by minority in their own country"

Cc Mzee Mwanakijiji , Wilbroad Slaa , Zitto , John Mnyika , Kitila Mkumbo , Mwigulu Nchemba


 
Mchambuzi, nimeisoma makala yako kwa umakini mkubwa, na nakiri kuwa kuna mambo nimejifunza, ingawa hayakuwa mageni sana lakini yameniongezea maarifa.

Ndani ya chama chetu CCM, kwanza kabisa hatujabadili mfumo wa siasa, hii ina maana siasa zetu ni zile za chama kimoja kikiwa mamba na vyama vingine vikiwa dagaa.

Lakini kumbe ukweli ni kuwa, siasa ya hapa nchini imebadilika, inataka kuona ahadi zikitekelezwa na sio ahadi zikibadilishwa tarehe, kwa mfumo huu wa siasa ni changamoto kwa viongozi wanaounda serikali.

Kikubwa ninacho kiona kuhusu viongozi wanaounda serikali ni udhati wa kutumikia taifa, hapa nakiri kuwa viongozi wengi wa CCM wanaounda serikali hii ya Kikwete wengi ni weupe, nikimaanisha ni wachovu kiutendaji. Kama tungekuwa na baraza la mawaziri lililo sheheni watu kama dr. Mwakyembe, dr. Kagasheki and the like, hali ingekuwa si haba katika kutekeleza ilani ya chama.

Katika kasi ambayo CHADEMA wanalipeleka taifa, katika hali ya kuwaaminisha wananchi kuwa serikali ya CCM inapaswa kuwapa zaidi ya inachokitoa kwa jamii, na ukweli ni kwamba, CHADEMA wana hoja za kuthibitisha kauli zao hizi, hoja zenyewe ni kama ufisadi, misamaha ya kodi, matumizi makubwa ya fedha kwenye shughuli za kawaida n.k, basi serikali yangu kwa kipindi hiki kifupi ijitahidi kuendana na kasi ambayo CHADEMA wanaaminisha watu, jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wa serikali.

Hapa naona kabisa serikali yangu inalazimishwa kukata viuno kwenye ngoma wanayoipiga CHADEMA, kama vijana wameyapokea mapambano na kuungana na jitihada za CHADEMA katika kuleta mabadiliko, hii hiwe changamoto ndani ya serikali ili kukinusuru chama chetu kwenye uchaguzi mkuu wa 2015.


Safi sana mkuu, tangia nimekufuatilia humu ndani naona sasa unabadilika na unakubaliana na hali halisi, wenzako siwaoni humu chalii yangu wote wananusa na kukimbia tuu..

Back to topic

Waliosoma na wasome na kuelewa watakaosikia na wasikie na waelewe.
 
Mchambuzi , huwa siyapendi maelezo Marefu sana kama haya yako , ila kutokana na hali halisi ilibidi tu niyapitie hadi mwisho , umeandika Ukweli sana , lakini nani atakusikiliza ? Lumumba imelemaa kwa Posho , ahadi za U- DC na Ubunge wa Viti maalum , na sasa hivi kuna vijana wameahidiwa Majimbo hata kama hawatashinda kura za maoni ! Si ulimuona Dr Hamis , pamoja na kwamba hakushinda kura za maoni lakini leo anawakilisha Nzega !
 
iniume nini? Maneno ya kwenye kanga hayo? Msubiri kimbunga 2015. CCM daima.
Hiyo ndio shida ya chama ambacho objective yake ni KUTAWALA tu, wala si kuwaongoza wananchi katika kujitafutia maendeleo.

Watu wamechoka na ahadi, wanataka matendo.
 
Back
Top Bottom