CCM: Tutajidanganya Hadi Lini?

CCM: Tutajidanganya Hadi Lini?

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Posts
4,850
Reaction score
9,434
Umezuka utamaduni wa baadhi ya Vijana wa Lumumba kuja JamiiForums na kuanza kutushambulia wana CCM wenye kukosoa Chama kutokana na kuzidi kukosa mwelekeo kwa zaidi ya miaka 20 sasa; Wana Lumumba hawa wana hoja kuu mbili mufilisi: Hoja yao ya Kwanza ni kwamba chanzo cha nchi kuyumba ni kutokana na Siasa za Upinzani, hasa Chadema, hasa kwamba Chadema ni chama kinacho chochea vurugu nchini; Kwa mantiki ya wana Lumumba hawa, kama Chadema isingekuwepo katika ramani ya siasa za Tanzania, basi mwamko wa watanzania katika karne hii ya ishirini na moja inayoendeshwa na Utandawazi, ungekuwa haupo;

Hoja mufilisi ya pili ya wana Lumumba hawa ni kwamba mwana ccm anayekosoa chama katika nyakati hizi anafanya hivyo kwa nia moja tu - Kutafuta umaarufu kwa Chadema, na hatimaye kwenda kugombea ubunge au udiwani kupitia Chadema; Kwa mtazamo huu, ina maana kwamba hakuna mwana ccm ambae anaweza kukosoa chama kwa kushindwa kutimiza ahadi zake za kumkomboa mwananchi (hasa wa kijijini) ambae kwa miaka zaidi ya 50 sasa amekuwa akisubiri matunda ya uhuru; Hoja zao hizi mufilisi ambazo hazijali maisha ya wanavijiji bali matumbo yao ni ushahidi tosha kwamba Wana Lumumba hawa ni Wana CCM Maslahi, kwani hawana hata muda wa kusoma na kuelewa kanuni za chama; Wanakosa ufahamu wa msingi kabisa kwamba Mwongozo wa CCM (1982) una kanuni nyingi sana ambazo kimsingi wangekuwa wanazi zingatia, wasingekisogeza chama kwenye umauti wake wa leo; Kwa mfano, moja ya Kanuni ndani ya mwongozo wa CCM (1982) inaweka wazi kwamba "KUKOSOA NA KUKOSOLEWA NDIO SILAHA YA MAPINDUZI"; Kanuni hii inahimiza juu ya viongozi na wanachama wa CCM kukubali kukosolewa bila ya kuhamaki kwani hivyo ndivyo tutaweza kujenga na kuimarisha chama;

Miaka ishirini na sita iliyopita (1987), Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alitamka maneno mazito sana ambayo pengine wana lumumba niliowajadili wangeweza kuhimiza akamatwe mara moja kwa uchochezi; Mwalimu alitoa maneno haya miaka nane kabla ya Chadema kuzaliwa; Sio tu kwamba maneno haya yanaendelea kuishi leo, lakini pia yataendelea kuishi hata kama Chadema kesho wataamua KWA RIDHAA YAO, kukifuta Chama Chao katika siasa za Tanzania; Mwalimu alitamka maneno yafuatayo (Chanzo ni Gazeti La Serikali, 1987):

["It is not that peace has come by itself. The source of peace in Tanzania is not that the Arusha Declaration has done away with poverty even a little bit. Isn't there this poverty we are still living with? This poverty is right here with us. It is not the same economy we are grappling with? The fact is not that the Arusha Declaration has banished poverty even by an iota – nor did it promise to do so. The Arusha Declaration offered hope. A promise of Justice, hopes to the many, indeed the majority of Tanzanians continue to live this hope. So long as there is this hope, you will continue to have peace. Here in Tanzania we have poverty but no ‘social cancer'. It is possible it has just begun. But otherwise we don't have a social cancer. There isn't a Volcano in the making, that one day it is bound to erupt. We have not yet reached that stage because the people still have hopes based on the stand taken by the Arusha Declaration. It did not do away with poverty but it has given you all in this hall, capitalists and socialists alike, an opportunity to build a country which holds out a future of hopes to the many.

To be sure, you few Waswahili, do you really expect to rule Tanzanians through coercion, When there is no hope, and then expect that they will sit quiet in peace? Peace is born of hope, when hope is gone, there will be social upheavals. I'd be surprised if these Tanzanians refuse to Rebel, why?

When the majority doesn't have any hope you are building a volcano. It is bound to erupt one day. Unless these people are fools. Many in these countries are fools, to accept being ruled just like that. To be oppressed just like that when they have the force in numbers, they are fools. So Tanzanians would be fools, ******, if they continued to accept to be oppressed by minority in their own country. Why?

Therefore we cannot say that we have now reached a stage when we can forget the Arusha Declaration. Don't fool yourselves. This would be like that fool who uses a ladder to climb and when he is up there kicks it away. Alright, you are up there, you have kicked away the ladder, right, so stay there because we will cut the branch. You are up there, we are down here and you have kicked away the ladder. This branch is high up, we will cut it. Your fall will be no ordinary fall either.

Let me say no more. It is sufficient to say we should accept our principles, we should continue with our principles of building peace and peace itself. Tanzanians should continue to have faith in the party, in the government and in you in positions. Tanzanians should see you as part of them not their enemies. They should trust the party, the government and you who have opportunities for there is no country where everyone is equal. These fingers of mine are not equal, and in that sense there is no such equality anywhere."]

Source: Gazeti La Serikali, 1987;

Maneno ya Mwalimu yanatoa tafsiri nyingi lakini tafsiri yangu kuu ni kwamba - hakuna mjadala kwamba mjenzi wa Amani, Utulivu na Umoja wa taifa letu ilikuwa ni TANU (CCM); Natumia neno "ilikuwa" kwa maana moja moja tu na ni kwamba KUJENGA Amani, Utulivu na Umoja wa Taifa ni kazi moja, lakini KUDUMISHA Amani, Utulivu na Umoja, hii ni kazi nyingine na kubwa zaidi; Ni katika hili la Kudumisha Amani, Utulivu na Umoja ndio CCM imekuwa inakabiliwa na changamoto kubwa, hasa katika mazingira ya mageuzi ya kisiasa (Demokrasia ya Uliberali) yanayoendelea nchini hivi sasa;

Je – Ni Kwanini Nchi inaanza kupoteza Amani, Utulivu na Umoja?

Mwalimu Nyerere ameshajadili mengi hapo juu lakini kwa kuongezea tu – haya ni matokeo ya Usimamizi Mbovu wa CCM katika suala zima la MAGEUZI YA KISIASA (Demokrasia Ya Uliberali). Mbali na mapungufu haya ya CCM kwa upande wa SIASA, CCM pia inakabiliwa na jinamizi jingine, nalo ni Usimamizi mbovu wa MAGEUZI YA KIUCHUMI (Uliberali Mamboleo) kwa manufaa ya watanzania walio wengi; CCM tunajisahau kwamba siri pekee ya kufanikisha azma yetu ya kuwapatia watanzania maisha bora ni kwa kusimamia vizuri michakato ya mageuzi ya kisiasa na kiuchumi nchini;

Pamoja na CCM kushindwa kusimamia kikamilifu Mageuzi ya Kiuchumi kwa Faida ya watanzania wengi, kwa kipindi kirefu tulifanikiwa kuepuka kukataliwa na umma kwa sababu tulifanikiwa ‘kutongoza umma' wa porojo za kisiasa kwamba ‘free market' & ‘capitalism' ndio njia pekee ya kuwakomboa kiuchumi. Wananchi wengi walikubali hoja hizi, hasa pale zilipoambatana na hoja kwamba mbadala wa soko huria na uberapi ni Azimio la Arusha, hasa kwa kuambiwa mapungufu ya Azimio hili, huku yale mazuri yakifichwa; Lakini kwa vile mbadala wa azimio la Arusha nao ulikuwa umejaa maovu (Azimio la Zanzibar 1992), details za azimio la Zanzibar nazo hazikuwekwa wazi kwani hata Mwalimu Nyerere kuna wakati alitamka jinsi gani hakushirikishwa katika maamuzi hayo; Lakini miaka 20 baadae, tunazidi gundua kwanini Azimio la Zanzibar lilikuja kwa hila: Lilihalalisha ufisadi, lakini muhimu zaidi, liligeuza Haki Ya Mungu Kwa Watanzania (Rasilimali Za Nchi) Kuwa Haki ya Mzungu, kupitia mfumo wa Soko Holela;

Leo wapo maskini wengi ambao bado wana amini katika porojo za maisha bora kwa kila mtanzania kupitia uliberali mamboleo, hasa wanapotishwa kwamba mbadala wake ni kurudia Azimio La Arusha; Mkakati huu unatusaidia CCM kujenga subira kwa wananchi lakini mafanikio katika hili ni ‘short lived'; Ushahidi wa hoja yangu hii ni kwa kuangalia jinsi gani kasi ya upepo wa mageuzi ya kisiasa inavyozidi kuyumbisha Chama kwani mageuzi ya Kisiasa (demokrasia ya uliberali) yanazidi kufungua macho watanzania wengi kwamba sehemu kubwa ya sababu kwanini maisha yao bado ni duni ni kutokana na kuchechemea kwa mageuzi ya kisiasa nchini (Demokrasia ya Uliberali); Na ushahidi wa hili upo wazi, hasa kwa kuangalia jinsi gani umma unazidi kuwa na mwitikio mkubwa kwa Siasa za Upinzani, hasa Chadema;

Ni katika mazingira haya CCM kuendelea kujaribu to dictate the pace of political reforms at our own pace/terms ndio tunajikuta ‘on a collision course' na nguvu ya umma kupitia Chadema; Lakini kwa sababu ambazo ni ngumu kuzielewa, CCM tunajidanganya kwamba kuzima siasa za Chadema ndio itakuwa ni mwisho wa mwamko wa Watanzania kudai haki zao ndani ya Demokrasia ya Uliberali; Tunasahau kwamba watanzania wanaishi Karne ya Ishirini na Moja inayoendeshwa na mguvu za Utandawazi, na wanaona dunia nzima, juu ya uwepo wa uhusiani mkubwa sana baina ya Demokrasia ya Uliberali (Liberal Democracy) na Maisha Bora Kwa Raia wan chi yoyote ile; Pengine ni muhimu nikafafanua kidogo dhana ya Demokrasia Ya Uliberali (Liberal Democracy) kwani, tusipokuwa makini, kibiriti kitachowasha moto wa machafuko nchini kitakuwa ni kwa CCM kuendelea to dictate the wave of democratic change at her own pace/terms, badala ya kufuatana na mahitaji ya wananchi;

Demokrasia Uliberali ina sifa kadhaa lakini zilizo muhimu ni hizi zifuatazo:


  1. Utawala WA SHERIA (Hii ni tofauti na utawala KWA SHERIA);
  2. Chaguzi huru, za uwazi na zinazofuata misingi yote ya haki;
  3. Uwepo wa Haki za Binadamu – rights that an individual enjoys because of being human – e.g. rights to life and liberty; freedom of thought and expression and equality before the law;
  4. Uwepo wa Haki za Raia – rights that an individual enjoys by virtue of citizenship – esp political, social and economic justice; na
  5. Utenganishaji wa mihimili ya dola – Legislature, Executive & Judiciary; Ukosefu wa hili huwa ni sababu kubwa kwa nini ‘State Fail';

Haina haja ya mjadala mrefu kuelezea jinsi gani Tanzania bado tunachechemea katika maeneo yote tajwa hapo juu. Vinginevyo, CCM, tuna haki ya kujipongeza kwa ujenzi wa (1) Amani, (2) Utulivu na (3) Umoja, vitu ambavyo tumevijenga kwa gharama na sacrifices nyingi sana; Lakini ni wajibu wetu pia kukubali kwamba CCM tumeshindwa kudumisha vitu hivi vitatu, hasa kutokana na kuchechemea kwa mageuzi ya kisiasa nchini (demokrasia ya uliberali); Ni muhimu kwa wana lumumba wachumia tumbo waelewe kwamba Udhaifu wetu katika haya haujaletwa na CHADEMA kwani kama tulivyokwisha ona, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alilizungumzia suala hili miaka Miaka 25 iliyopita (1987);

Kwa wana CCM wenye mapenzi ya dhati na nchi yetu Tanzania, huu ni wakati muafaka wa kuanzisha "Mapinduzi Ya Kifikra" ndani ya Chama; CCM tunahitaji kuzinduka kutoka kwenye usingizi mnono wa ‘party- state politics' na kukabiliana na ukweli kwamba "Chama Cha Mapinduzi is no longer the Only Political Expression of the STATE"; Kuna uwezekano kwamba CCM is still the only political expression of the GOVERNMENT kutegemeana na jinsi gani mtu anajenga hoja, lakini CCM being the Only Political Expression of the STATE ni suala ambalo halipo tena na halitatokea tena hata kama Chadema itaamua kujifuta kama chama cha Siasa kwa ridhaa yao; Katika zama hizi mpya za Demokrasia ya Uliberali, mfumo ambao baadhi ya sifa zake tumezijadili hapo juu, The Political Expression of the State MUST BE EQUALLY SHARED na Vyama vingine vya Siasa nchini kama Chadema, CUF, n.k; Vile vile kuna umuhimu kwa CCM kuamka kutoka kwenye usingizi mnono wa ‘party-state politics' na kutambua kwamba Chadema, CUF n.k, all are ‘EQUAL CONTENDERS FOR THE VERY SAME STATE' iliyopo chini ya CCM hivi sasa, kupitia Sanduku la Kura;

Ni vigumu kuelewa kwanini CCM hatukubali kuishi ndani ya mazingira haya mapya ya 'genuine liberal democracy', kwani in the long run, itaokoa hata CCM yenyewe; CCM tunaishi kama vile ipo siku nchi itarudia mfumo wa chama kimoja kwa ridhaa ya wananchi; Pengine viongozi wenye mtazamo huu ndani ya CCM bado wanaishi katika mawazo ya miaka 20 iliyopita ambapo 80% ya watanzania kupitia tume ya nyalali walipendekeza nchi iendelee kuwa chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa; Tukumbuke tu kwamba hata rafiki zetu China ambao wana nguvu kubwa sana za kijeshi na kiuchumi, mfumo wao wa chama kimoja hautadumu milele;

CCM, tumepoteza fursa ya kuingia katika ushindani wa kisiasa huku tukiwa bado tunapendwa na sehemu kubwa ya umma; Mwalimu alitujengea mazingira mazuri sana ya kuingia katika siasa za ushindani tukiwa imara, lakini tukashindwa kutumia fursa hiyo kwa sababu ya viongozi wachache tu wasio na mapenzi na chama bali matumbo yao; CCM tunajiona kwamba we have the TIME lakini tunasahau kwamba Chadema has the CLOCK; Tukubali tu matokeo na tuendeshe siasa za hoja kama ilivyo katika nchi za wenzetu ambapo vyama vikuu vya siasa hupokezana vijiti ndani ya mazingira ya amani, utulivu na umoja wa kitaifa kwani kushindwa kwa chama kimoja katika uchaguzi ndio fursa ya chama hicho kujipanga na kuja kushinda uchaguzi unaofuata; Lakini siasa za CCM hivi sasa ni kama vile kushindwa kwa chama ndio itakuwa mwisho wa CCM; Kuna uwezekano wa hili kutokea lakini pia tukubali kwamba haikutakiwa tufike huko, ni sisi wenyewe ndio tumejijengea mazingira haya, hasa kwa kudharau dhana nzima ya demokrasia ya uliberali ambayo ni sisi wenyewe tuliikubali mwaka 1992 kupitia mapendekezo ya tume ya nyalali kwa kuchukua maoni ya watanzania wachache na kukataa maoni ya wengi walio pendelea mfumo wa chama kimoja uendelee; CCM, Tatizo letu sio Chadema, Tatizo letu ni kuendelea kukaidi demokrasia ya uliberali ndani ya uchumi wa kiliberali ambao tumeshindwa kuusimamia kwa maslahi ya wananchi walio wengi;

Ningependa kumalizia Kwa kujadili matukio makubwa mawili yaliyotokea hivi karibuni ambayo ni muendelezo wa CCM kutoheshimu dhana ya Demokrasia Ya Uliberali; Matukio haya ni lile la Naibu Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai kuwatimua wabunge watano wa Chadema bungeni na pia tukio la kukamatwa kwa mbunge wa Arusha Mjini, Mh. Godbless Lema; Nikianza na hili la Ndugai, kuna umuhimu wetu kurejea kidogo katika historia ya dunia, hasa kubaini kwanini wenzetu Uingereza hatimaye walikuja na mfumo wao wa Westminster; Katika karne ya kumi na saba, taifa la Uingereza lilipitia misuko suko mingi inayofanana na kwetu leo, hasa kuhusiana na mikwaruzo baina yaUtawala wa nchi na wawakilishi wa wananchi (Wabunge);

Kwa muda mrefu, Wabunge kadhaa nchini Uingereza walikuwa wakipinga vikali jinsi gani Mfalme alikuwa anaendesha nchi (King Charles I); Baada ya kuchoshwa na tabia hii ya wabunge, Mfalme akatoa amri WABUNGE WATANO ambao ndio walionekana ni wasumbufu zaidi, wakamatwe mara moja wakati kikao cha bunge kilipokuwa kinaendelea; Jaribio hili la mfalme halikufanikiwa kwani askari wa mfalme walipofika katika eneo la bunge walikuta wabunge husika wameshakimbia baada ya kutaarifiwa na raia wema waliokuwa na kiu kubwa ya mabadiliko; Lakini kwa vile wananchi walikuwa wameshachoshwa na utawala ambao haukuwa unajali haki zao za kisiasa, kijamii na kiuchumi, jaribio hili la mfalme likawa ndio kibiriti kilichowasha moto wa Vita Vya wenyewe kwa wenyewe vya Uingereza (The English Civil War) katikati ya karne ya kumi na saba;

Sasa ili kuepusha taifa lisiingie katika machafuko, hasa kufuatana na onyo kali la Mwalimu Nyerere Nyerere hapo juu, CCM tumebakiwa na fursa finyu sana ya kuratibu mageuzi ya kisiasa ili hata huko mbeleni yaje kuweka a fair playing field kwa vyama vyote vya siasa, hasa ikizingatiwa kwamba suala la CCM kuwa chama cha upinzani ni suala linalosubiri muda tu, hata kama chama tawala hakitakuwa Chadema; Kuna maeneo mengi ambayo tunahitaji kuyafanyia kazi, kwa sasa nitajadili mawili;

Kwanza ni suala la Kukamatwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema; Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania ya 1977, ibara ya (100) inazungumzia "Power and Privileges of Parliament" kama ifuatavyo:

100 (1) There shall be freedom of opinion, debate and in the National Assembly, and that freedom shall not be breached or questioned by any organ in the United Republic or in any court or elsewhere outside the National Assembly.

(2) Subject to this Constitution or to the provisions of any other relevant law, a Member of Parliament shall not be prosecuted and no civil proceedings may be instituted against him in a court in relation to anything which he has said or done in the National Assembly or has submitted to the National Assembly by way of a petition, bill, motion or otherwise.

Nadhani wengi tunaelewa umuhimu wa kinga hii kwa wabunge kwani nia yake ni kuwapatia wabunge uhuru na uwanja mpana wa kujadili bila ya uwoga masuala ambayo wao wanaona ni muhimu kwa maslahi ya taifa; Ni kutokana na kinga hii, ndio maana wabunge wengi wamekuwa hawachukuliwi hatua zozote za kisheria kwa kauli wanazozitoa bungeni; Lakini it gets tricky kidogo mbunge anapokuwa nje ya bunge kwani kwa kauli zilezile, anaweza kukamatwa na kufunguliwa mashitaka; Kuna umuhimu wa suala hili kufanyiwa marekebisho ndani ya katiba mpya, hasa kuepusha siasa na nguvu ya dola kutumika kuwaghasi na kuwatisha wabunge, ili kuwalinda kama inavyowalinda wakiwa ndani ya maeneo ya bunge; Maana yangu ni nini hapa:

Iwapo tuna nia ya kweli ya kuimarisha demokrasia ya uliberali nchini, basi kuna umuhimu wa kuongezea nguvu ibara ya (100) ya Katiba ili kuhakikisha kwamba kinga hizi kwa wawakilishi wa wananchi zinakuwa extended hata wakiwa nje ya bunge, hasa iwapo ni wakati Vikao vya bunge au vya Kamati za bunge vikiwa vinaendelea; Haina maana kwamba Katiba Mpya iwape Wabunge "an absolute immunity", bali nia ni kuepusha matumizi mabaya ya nguvu dola kukamata viongozi waliowekwa na nguvu ya umma kwa sababu za kisiasa, ikiwa ni pamoja na kuwazuia wasiwepo bungeni wakati mijadala muhimu inayogusa wananchi ikiwa inaendelea au wakati wa upitishaji wa miswada mbalimbali muhimu inayohitaji kura za wabunge;

Ingawa katika mazingira ya sasa kura bungeni zinapigwa kwa mayowe ya Ndiyo au Hapana, ni dhahiri kwamba huko mbeleni mfumo wa sasa utabadilika ili kupisha mfumo mpya (voting system); Chini ya mfumo huu, kukosekana kwa mbunge hata mmoja kwa sababu za ovyo ovyo, hasa kisiasa, kutagharimu sana wananchi; Ni muhimu CCM ikasimamia marekebisho haya kwa vile yatakuwa kwa manufaa ya CCM pia kwani ni jambo lisilokuwa na mjadala kwamba ipo siku CCM pia tutakuwa Chama Cha Upinzani Tanzania, hata kama Chama Tawala hakitakuwa ni Chadema;

Suala la mwisho ni kuhusiana na utaratibu wa kufukuza kwa nguvu ya dola, viongozi walioingizwa bungeni kwa nguvu ya umma (wabunge) kwa sababu za kisiasa bila ya kujali gharama zinazojitokeza kwa wananchi kwani kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, Mbunge ni mwakilishi wa watanzania wote, Mbunge sio Mwakilishi wa jimbo lake peke yake au Chama Chake Cha Siasa; Kwahiyo kuna umuhimu wa wadau husika kuhakikisha kwamba Ndani ya Katiba Mpya tunafuata mfumo wa Westminster ambapo Spika wa Bunge anaweza kumfukuza mbunge katika kikao for disorderly conduct ambazo zipo wazi, na sio za kupinda pinda kukidhi matakwa ya Kisiasa; Mbali ya disorderly conduct hizi kufafanuliwa kwa uwazi na lugha rahisi kwa wananchi kuelewa, pia katika mfumo wa Westminster, iwapo Spika analazimika kuadhibu wabunge, utaratibu uliopo ni kwamba Spika anaita jina la mbunge husika na kuitisha upigaji wa kura za wabunge wote za NDIO au HAPANA, na iwapo kura za NDIO zinashinda, basi mbunge husika anasimimishwa kuhudhuria vikao vya bunge kwa siku tano kwa kosa la kwanza, na siku ishirini kwa kosa la pili, huku pia akikosa posho zake za siku zote ambazo atakuwa amesimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge; Lakini iwapo kura za HAPANA zinashinda, basi mbunge huyo anaendelea kuhudhuria vikao vya bunge kama kawaida;

Itaendelea…
 
Good, huu ni ukweli...ila watatoa povu mpaka macho yatawatoka. Wamekaa na Moto ya kijinga eti "CCM YAJENGA NCHI...CCM INA WENYEWE..." kumbe matapeli yanayopewa baraka na serikali...
 
Kwanza Mchambuzi hakuna mwanaCCM atakayesoma makala yako yote! heading tu zitawakimbiza hapa kukukebehi!
Wengine tunawajua ni Ma Dr kabisaaa!
CCM wanavichwa vizuri kama wewe lakini hawawatumii kwasababu hawataki ukweli.
Kuna ndugu yangu amewahi kuwa kiongozi mdogo tu huko lakini makala zake za kukosoa chama chake zilimfanya akimbie nyumba yake mara tatu tena usiku mnene sababu ya vitisho.
Tunaipenda Tanzania na tutasimama na kila atakae kuwa mzalendo.
 
Ndugu yangu Mchambuzi kutoka Mtaa wa Ufipa Kinondoni Zipo aina tatu za Propaganda
1.Yellow
2.Black
3.White
Wewe upo namba 2,ni propaganda ya adui kujivika sura ya kirafiki na akakushauri!
Binafsi nimekugundua unatoka Mtaa wa Ufipa kwenye nyumba ya kupanga Kinondoni,washauri viongozi wako wa Chadema ambao naamini baadhi ni vichaa kama Godbless Lema,Dr Slaa ambae juzi alitaka kumzoea Profesa Baregu akampiga stop!
 
Ndugu yangu Mchambuzi kutoka Mtaa wa Ufipa Kinondoni Zipo aina tatu za Propaganda
1.Yellow
2.Black
3.White
Wewe upo namba 2,ni propaganda ya adui kujivika sura ya kirafiki na akakushauri!
Binafsi nimekugundua unatoka Mtaa wa Ufipa kwenye nyumba ya kupanga Kinondoni,washauri viongozi wako wa Chadema ambao naamini baadhi ni vichaa kama Godbless Lema,Dr Slaa ambae juzi alitaka kumzoea Profesa Baregu akampiga stop!

Uzuri ni kwamba nimeshajadili kwa kina aina yenu ya wana lumumba katika bandiko namba moja;

Lakini naomba nikuulize tu - Je, kauli ya Mwalimu Nyerere mwaka 1987 miaka nane kabla Chadema kuzaliwa alikuwa katika kundi gani la hizo propaganda? Kwani mada yangu msingi wake ni maneno ya Mwalimu 1987, ambayo yanazidi kunifungua macho, hata kama mshindani wa CCM ingekuwa ni Chama cha soka Tanzania (TFF);

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Ndugu yangu Mchambuzi kutoka Mtaa wa Ufipa Kinondoni Zipo aina tatu za Propaganda
1.Yellow
2.Black
3.White
Wewe upo namba 2,ni propaganda ya adui kujivika sura ya kirafiki na akakushauri!
Binafsi nimekugundua unatoka Mtaa wa Ufipa kwenye nyumba ya kupanga Kinondoni,washauri viongozi wako wa Chadema ambao naamini baadhi ni vichaa kama Godbless Lema,Dr Slaa ambae juzi alitaka kumzoea Profesa Baregu akampiga stop!

Wajinga na wehu ni sehemu ya viumbe wa Mungu wetu mwema.

MCHAMBUZI, amefanya uchambuzi basic na mwenye uhai na uwezo wa kusoma basi asome kwa faida ya chama cha Mapinduzi.
 
Ni ukweli usio pingika kwamba ccm inaangalia sana inapoangukia lakini haijishughulishi na kutazama wapi ilipojikwaa, imekubali kwenda kwa siasa za matukio inazolazimishwa kufanya na CDM na vyama vingine kama ilivyo sasa. ukiwaangalia mawaziri wanavyojibu maswali bungeni unashanga kama kweli wanajua wajibu wao lakini kwa muelewa utajua tatizo ni hawa wabunge tuliowachagua. huishii hapo tu unajiuliza chama hiki kina nahodha wa kuendesha jibu ni hakuna kila mtu anausukani hivo anaendesha anakotaka yeye Mlongo kwake, Kinana kwake, Mlugo kwake, Lowasa huko. unamaliza kwa kusema kumbe hawa watu wote kuanzia rahisi hadi mjumbe wanashirikiana kuhujumu chama.

Vijana wa Lumumba wametawanyika katika social network kusifia hao wagawa ngawira wao wanaowaweka mjini kwa bei ndogo tu ya pipi na banzoka masikini wengine tumesoma nao tunajua hadi makwao nd ndugu zao walivyochoka huku wakisubiri ndoto za maisha bora zitimie. Miaka hamsini ya uhuru imepita vijana tumebaki kushabikia uozo baadala ya kuwa walinzi na wadadisi wa mambo yanatuathiri. vyuo vyetu chini ya utawala wa ccm vimezalisha vijana waoga wasiojiamini na wameingia katika mfumo mbovu wa kuhujumu uchumi na maisha ya ndugu zetu. tukumbuke kwa vyovyote vile vijana ndio tutakao umia chini ya uozo huu familia zetu zimewekeza kwetu hatuwezi kusonga mbele kama mfumo uliojengwa na ccm utaendelea kuwepo.

Nimalizie kusema uwe mawana ccm ama la ukikubali kutumia tumbo kufikiri basi ujue umekubali utu wako kuupoteza na kuuchezea kama mwigulu. taifa hili lina maana zaidi ya vyama vyetu na vijihela mnavyohongwa, ikumbukwe kuna ghalama ya kila kitu, tukiamua kusema NO kuna ghalama vivyo hivyo Kusema YES. ni wakati huu kusema NO kwa hawa WATAWALA waliopoteza misingi ya UONGOZI. ccm sasa imekuwa zaidi ya kichaa mwenye rungu ambaye anaponda kila kitu anachokiona. wao watang'oa sana kucha na meno, watakandamiza sana haki za watu watafuja sana mali na watatamani walale juu ya dhahabu maana anasa za wao wachache wamesahau kuwa ni suruba kwa cc tulio wengi.

HAYA YOTE YANA MWISHO, NA MWISHO WAKE NI MCHUNGU NA WA FURAHA KWA KILA MTANZANIA. ITAZAME NAFSI YAKO NA MATENDO YAKO UMESIMAMA WAPI NA KWA MASILAHI YA NANI.
 
Mchambuzi uchambuzi wako umeuchambua vizuri na watanzania kila siku wanazidi kuamka kwa kasi hasa walio vijijini kwa sasa wanaamka kwa kasi ya ajabu na kukitishia maisha chama chako CCM, wao ndio wapiga kura na ndio wanao chagua rais wa nchi hii.

Mchambuzi Swali linakuja je Viongozi wako wamejiandaa vipi kukabiliana na hali hii ya kuondolewa madarakani na Watanzania kwa sanduku la kura ikiwa wakikataliwa na watanzania? Kwa jinsi inavyoenekana kwa sasa Kifo cha chama chako hakipo mbali sana na Kaburi na CCM inachosubiriwa kwa sasa ni kuzikwa.
 
Mchambuzi heshma kwako unafikiri vijana wa lumumba wanajishughulisha kusoma nondo kama hizi na hutawaona hapa wakati katibu wa itikadi na uenezi alitakiwa aje hapa afafanue lakini nae yuko kwenye kitengo cha propaganda.saizi imefikia hatua mtaani ukikosoa serikal unaitwa chadema,hivi huko ccm hakuna waliotimamu?jibu hapana ila unafiki.
 
Mkuu Mchambuzi, kwanza kabisa nikupongeze kwa kazi ngumu ya uchambuzi yakinifu uliyo ifanya, nidhahiri umetumia mda mwingi sana kukamilisha huo ujumbe, Mwenyezi Mungu akubariki.

Mkuu, ni matumaini yangu ya kuwa ujumbe umefika na Misukule wa Lumumba watausoma hata ki-moyo moyo na kuufanyia kazi.
 
Ni uchambuzi na ushauri mzuri sana, lakini tatizo ni kwamba ccm imeshakuwa 'mama haambiliki', sana sana utaishia kuitwa we msaliti. Mi naamini ccm ni sikio la kufa tu, its just a matter of time.
Btw, nina mashaka kama meno na kucha zako zitasalimika.
 
Mageuzi yanapokuja yanaangalia the most organized entity ndiyo itakayo-spearhead hayo mageuzi iwe ni chama cha siasa, chama cha wafanyakazi, taasisi ya kidini, CBO, NGO, jeshi n.k. Sasa CCM inafikiri kwa ku-oppress vyama vya siasa basi itachelewesha mageuzi, haijui kuwa mageuzi yanapokuja ni either yenyewe CCM ikubali kugeuka ili iendane na mageuzi au mageuzi yaiweke pembeni yaendelee na wale waliotayari kubadilika nayo. Sasa hatari iliyopo ambayo CCM itatusababishia ni pale ambapo mageuzi yatakuja halafu hakuna strong and much organized entity ya kuspearhead hayo mageuzi ndio hapo machafuko yanapotokea, kwa kuwa hata jeshi haliko organized ndio utashangaa hata sajenti au koplo wa jeshi anaenda TBC anatangaza yeye ndio military junta, kesho yake anauwawa anakuja kanali mwingine anajitangaza yeye ndio kiongozi
Mchambuzi nimekuelewa ila najua viongozi/watawala wako hawawezi kuchukua ushauri huu kwa sababu mbili, kwanza aina ya uongozi uliopo leo hii CCM hakuna mwenye charisma ya uongozi. Waliopo ni kundi la wasanii ambao kwa upeo wao finyu wanaangalia maslahi yao kama wao na ku-undermine maslahi mapana ya taifa kwa hisia kuwa watatawala milele hivyo hakuna siku watakayokuwa answerable kwa mambo wanayoyafanya. Ndege wanaofanana mabawa huruka pamoja, hebu angalia viongozi aliowachagua JK wengi wamefoji au kununua vyeti, wahuni na wezi wa wake za watu mpaka picha zao zipo kwenye mitandao, sas kwa hali hiyo unategemea wataweka nguvu kwenye maendeleo au propaganda za kufunika weakness zao.
Ukitaka kuliona hili vizuri waangalie watu wawili kikwete na lowassa. Ndio maana walishindwa kukaa zizi moja kwa mda mfupi tu. JK na EL ndio watu waliokuwa wana oversee selikali ya 4 ilipoingia. JK ni msanii /muhuni wa mjini/tapeli wakati EL pamoja na kuwa na character za usanii ila ana charisma ya uongozi. Sasa walipokuwa kwenye serikali EL aki-spear head uongozi mwenzake analeta mizaha na usanii mwisho wakatofautiana ikabidi mmoja atoke.
Tatizo la lowassa siyo kwamba alikuwa hajui kuwa Kikwete ni mtu wa mizaha na msanii tu, alichokuwa hakijui ni kuwa JK ni msanii kwa asilimia 100 hana hata chembe ya uongozi. Sasa Lowassa baada ya kutambua madhaifu hayo ya JKwakati tayari wameshachukua uongozi wa n chi akafikiri solution ni yeye kuongoza mwenyewe hasa kwenye mambo ambayo yanahitaji quick response. Sasa Jk alipoona Lowassa anaonyesha uongozi sehemu muhimu bila kumshirikisha yeye na anapata umaarufu akaingia wivu ndio ugomvi ulipoanza.
 
Uzuri ni kwamba nimeshajadili kwa kina aina yenu ya wana lumumba katika bandiko namba moja;

Lakini naomba nikuulize tu - Je, kauli ya Mwalimu Nyerere mwaka 1987 miaka nane kabla Chadema kuzaliwa alikuwa katika kundi gani la hizo propaganda? Kwani mada yangu msingi wake ni maneno ya Mwalimu 1987, ambayo yanazidi kunifungua macho, hata kama mshindani wa CCM ingekuwa ni Chama cha soka Tanzania (TFF);

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Mchambuzi mbona umeniwahi nilichokuwa nakifikiria, hebu check bandiko langu namba 15, nimeliongelea hili, Muda utakapofika wa wananchi kupata mageuzi hawataangalia hayo mageuzi anayaleta nani hata yakitokea msikitini watayakubali, Kinachotakiwa ni kuwa na strong organization za kitaifa ili mageuzi yatakapokuja yakute zipo organization za kitaifa ili zibebe agenda ya mageuzi. Otherwise yanaweza yakafika yakakuta kuna vyama vya kufa na kuzikana vya kikabila ndio viko strong ambavyo definitely vitatugawa tu mwisho wa siku.
 
Mchambuzi,
Nimeisoma mara mbili hii makala naweza kusema labda "nimeielewa kidogo". Kitu ambacho kiko wazi, Tanzania kama taifa lina bahati kubwa sana kuwa na mtu kama mchambuzi, ni mchambuzi wa kweli tu anayeweza ku-link kumbukumbu za miaka zaidi ya 400 iliyopita, 25 iliyopita na kuielezea kiufasaha kabisa katika mazingira ya leo. Nitashangaa sana kama "agents" hawaifanya makala hii isomwe na watu muhimu kabisa katika Taifa hili ambao ni:- Rais, WM, Marais wawili wastaafu, Mkuu wa Majeshi, Mkuu wa UWT na IGP kwa mapenzi mema kabisa yaliyojadiliwa humu. Lets assume wale waliotoa habari za kukamatwa kwa wabunge kwa amri ya mfalme Charles I na hivyo waondoke zao (nadhani walikuwa ni askari pia). Kwa Tanzania ya leo, watu hao wanapatikana kwa wingi katika kada nyingi za utumishi wa umma ISIPOKUWA katika vyombo vya Polisi na Jeshi (aidha wachache au hakuna); (rejea mazingira ya Lema Arusha). Lakini pindipo nako huko Jeshini na Polisi, hususan polisi watakapopatikana kwa wingi, basi mengi ya uliyoyachambua hapa yatatokea muda mfupi tu. Kwanini? Kwa sasa, serikali inafanya kazi kuu moja tu (ya kukanusha ukweli unaopenyezwa nje ya serikali kupitia kwa watumishi wake). Kuvuja kwa taarifa hizo ni ishara kuwa watumishi wake nao wamechoka mwenendo wa utendaji wa serikali yao hasa chama cha CCM. Kwa sasa polisi wanalalamika sana ila chinichini (ukifanya utafiti kupitia malindo ya mabenki na ofisi kubwakubwa ambapo polisi na private security guards wanakuwa pamoja utalijua hili). Serikali inatumia mbinu za "wafalme wa kizamani" kujenga imani kwa majeshi hususan wa ngazi za juu na kuwasahau wadogo na jukumu lao kwa wananchi(Rejea tunzo za watumishi waliotukuka zilizotolewa hivi karibuni). Haya yote hayana mwisho mwema isipokuwa mwisho mwema ni huu uliouchambua mchambuzi,shukrani.
Mungu akulinde na azidi kukuongoza.
 
Mh! Ngoja kwanza nipite nitarudi.

Bora urudi kweli aisey, ni aibu hapo baadaye kutengeneza taifa la wakimbizi, msiwe watu wa kuaamrishwa tu hata ujinga. Tuachaneni na ushabiki wa vyama, panapotokea hoja ya kweli tuipe haki yake. Je hali ya maisha ya wananchi haionyeshi kukata tamaa? hili ndilo swali na hoja ya msingi ya mchambuzi, kwamba serikali ya chama chako ichukue hatua stahiki za kutoa haki inayostahili japo kwa kiwango hicho kidogo, hivi leo hii, ukipanda daladal shida, ukinunua ki-vitz chako unaongeza na bajeti ya trafiki, maji hakuna, umeme tabu, vyakula havishikiki, kodi za nyumba usiseme, elimu ndiyo hiyo kama unavyoiona, hospitalini hakuna iliyo afadhali, gap la walionacho na wasionacho linazidi kuongezeka, njaa ndiyo inatamalaki nchi nzima. Hivi kweli 2013 bado Tanzania na eneo tulilonalo tunazidi kufa kwa njaa? lakini nyie wenzetu wa Lumumba wala hamuyaoni haya yote. Mnatia pamba masikioni tu. Haya, Mwenyezimungu awalipe jazaa yenu.
 
Back
Top Bottom